Nyimbo Swahili_Congo
1, 2, 3, 4, 5, 6, 7, 8, 9, 10, 11, 12, 13, 14, 15, 16, 17, 18, 19, 20, 21, 22, 23, 24, 25, 26, 27, 28, 29, 30, 31, 32, 33, 34, 35, 36, 37, 38, 39, 40, 41, 42, 43, 44, 45, 46, 47, 48, 49, 50, 51, 52, 53, 54, 55, 56, 57, 58, 59, 60, 61, 62, 63, 64, 65, 66, 67, 68, 69, 70, 71, 72, 73, 74, 75, 76, 77, 78, 79, 80, 81, 82, 83, 84, 85, 86, 87, 88, 89, 90, 91, 92, 93, 94, 95, 96, 97, 98, 99, 100, 101, 102, 103, 104, 105, 106, 107, 108, 109, 110, 111, 112, 113, 114, 115, 116, 117, 118, 119, 120, 121, 122, 123, 124, 125, 126, 127, 128, 129, 130, 131, 132, 133, 134, 135, 136, 137, 138, 139, 140, 141, 142, 143, 144, 145, 146, 147, 148, 149, 150, 151, 152, 153, 154, 155, 156, 157, 158, 159, 160, 161, 162, 163, 164, 165, 166, 167, 168, 169, 170, 171, 172, 173, 174, 175, 176, 177, 178, 179, 180, 181, 182, 183, 184, 185, 186, 187, 188, 189, 190, 191, 192, 193, 194, 195, 196, 197, 198, 199, 200, 201, 202, 203, 204, 205, 206, 207, 208, 209, 210, 211, 212, 213, 214, 215, 216, 217, 218, 219, 220, 221, 222, 223, 224, 225, 226, 227, 228, 229, 230, 231, 232, 233, 234, 235, 236, 237, 238, 239, 240, 241, 242, 243, 244, 245, 246, 247, 248, 249, 250, 251, 252, 253, 254, 255, 256, 257, 258, 259, 260, 261, 262, 263, 264, 265, 266, 267, 268, 269, 270, 271.
Tunakuabudu Baba Mungu
Wewe uishie nuruni
Unapambanua mbingu
Twakusanyika mbele yako
Wana wa pendo lako kubwa
Tunasifu jina lako,
{Tunakuheshimu,
Muumba wa vyote
Aleluya ! utukufu,
Kwake Mungu na Mwokozi
Aleluya !}
Wewe ulituangazia,
Mwenye enzi, Baba wa neema,
Kupitia Mwana wako
Kwake tunakubariki,
Twakuabudu, tunakusifu
Na kukutukuza hapa,
{Tunakuheshimu,} etc.
Tuimbe wimbo takatifu
Wakusifu Mwana wa pekee,
Milele Mwana wa Mungu
Kwa kufa na kuishi kwake
Alifunua neema kubwa
Njia nzuri ya mbinguni
Sifa na heshima
Kwa yesu Mwokozi
Aleluya ! utukufu,
Kwako Bwana !
Aleluya! Aleluya.
Yesu tunakuheshimu
Utakayebaki milele
Wimbo wa wakombolewa.
Uliumizwa tuokoke
Ulichubuliwa tupone
Tuishi kwa ufufuko
Sifa na heshima
Kwa Yesu Mwokozi etc.
Yesu ukombozi wetu
Kwa teso ulitupatia
Ukombozi wa milele
Bwana mwenye utukufu
Ndani yako tuna amani,
Na ushindi na baraka.
Mwokozi muzuri
Uketiye juu
Kwa uzuri
Na heshima
Twakuabudu
Tutakukuza milele.
Tukuzwa Baba wetu (bis)
Uliyetuandalia makao juu mbinguni
Umetowa wokovu (bis)
Wastahili shukrani ya mapendo na kusifu
Tukuzwa Mwana Kondoo (bis)
Kwakuokowa kundi ulikufa msalabani
Ukashinda shetani (bis)
Mukombozi wa ajabu sifa ni kwako milele.
Kweli tukuzwa Bwana (bis)
Pokea pekee nguvu, kuzo, heshima na, ufalme.
Milele na milele (bis)
Tutaimba wokovu, ushindi wa wema wako.
Pendo lako latukusanya
Kando ya Kristo pamoja
Vinywa vyetu vinatukuza
Pendo lako la milele
Utukufu ni wako Baba !
Sifa kwa mapendo yako !
Watoto wako wakusifu hapa,
Wakingoja makao mazuri.
Kwa neema, fumbo ya Mungu
Ulitaka tangu mbele,
Kutuingiza Baba wetu,
Katika uheri wako
Utukufu ni wako Baba, etc.
Kutaka kwa mapendo yako
Hakungeweza tosheka,
Bila kupata mbele yako,
Wakombolewa kamili
Utukufu ni wako Baba, etc.
Salama, mema, mbingu yako,
Tumevipata kwa Yesu ;
Punde atatuita kwa ushindi,
Kwake tutainuliwa
Utukufu ni wako Baba, etc.
Mungu twainamisha nafsi
Mbele ya mapendo yako;
Timiza mahitaji yetu;
Fanya Yesu aje mbio
Utukufuni wako Baba, etc.
Tukuze Mungu wa mapendo
Wa amani kwa wimbo safi
Aliye kwa wema fahari
funguwa njia ya mbingu
Kwa neema iliyo bora
Na sisi wabarikiwa,
Hai kwa moyo wa furaha
Tuinuwe nyimbo zetu.
Mioyo yetu yakutukuza
Mwenye uwezo na pendo
Sisi tunakutegemea
Kwa sasa na kwa milele.
Nguvu, wema, neema, uwezo
Ndani yako vinasifu
Na kanisa kwa uhakika
Lakungojea urudi.
Kwa Yesu tunatoa
Zabihu za sifa zetu
Kwa Yesu tunaabudu
Malaika vilevile
Mungu ubarikiwe tunapokusanyika
Tulikuwa zambini
Sote wana wa gazabu
Ukatuweka huru
Ndani yako tuna Baba
Mungu ubarikiwe tunapokusanyika.
Na tumepewa Yesu
Na umetuweka kwake
Ndani yake tuliitwa
Kupewa taji milele
Mungu ubarikiwe tunapokusanyika.
Alituahidiya
Mwana aja kututwaa
Kwenye makao ya juu
Tupendapo kumungoja
Mungu ubarikiwe tunapokusanyika.
Hivi tutakukuza
Katika kuzo na nuru
Na tutasema tena
Na Kanisa lako lote
Mungu ubarikiwe tunapokusanyika.
Asifiwe Mwokozi
Na Mwana pekee wa Mungu
Alikuja duniani,
Kuokoa wenye zambi
Ee Yesu utukuzwe milele na milele. (bis)
Ee Mwana ulikuja
Kufa kifo cha aibu
Ukashinda kaburi
Kwa uwezo wa milele
Na Ulivunja nguvu za
Kwa pendo ulikunywa
Kikambekichungu
Na ukatupatia
Kikombe cha ukombozi
Ee yesu utukuzwe milele na milele. (bis)
Sifa kwako kanisani
Kwa pendo lako nzuri !
Mwenyewe ulilinunua,
Ni lako bila mwisho.
Nyumbani mwa Baba yako
Punde utalileta ;
Likingaa nuru yako
Utalileta kwako.
Sifa kwako kanisani !
Kuna muda wa taabu,
Mbele yakukubaliwa
Pasipo tena chozi
Nyumbani kwenye uzima,
Ulioshinda kifo,
Bibi arusi akishangaa
Atabariki Kondoo.
Sifa kwako kanisani !
Sifa kwa Mukombozi !
Unajiunga na sisi,
Kifuani watubeba.
Siku nzuri inakuja,
Tukuonyeshe kwa yote ;
Utukute bila taka,
Tukikushuhudia.
Sifa kwa Mwana – Kondoo Mwokozi
Ndani yake kifo kilishindwa
Adui aliona nguvu yake
Vilevile kaburi inamutii
Utukufu kwako Yesu
Utukufu Bwana Yesu
Na kuzimu kumeshindwa
Ushindi (bis).
Vile Kristo alikataliwa
Na kukaa mbinguni aki’ngaa
Na Kanisa lisilo julikana
Karibuni litavikwa utukufu
Utukufu kwako Yesu
Utukufu Bwana Yesu
Na kuzimu kumeshindwa
Ushindi (bis).
Yesu uliahidi kurudi
Kututafuta punde yu waja
Na wafalme katika utukufu
Tutaimba sote wimbo wa ushindi
Utukufu kwako Yesu
Utukufu Bwana Yesu
Na mauti imeshindwa
Ushindi (bis).
Tuonapo juu, sifa unayovikwa
Na tunakuabudu, tukikutazama,
Sifa iangazayo, Yesu yakuzunguka
Inatukumbusha msalaba na haya.
Na kwa ule woga, pia huzuni mkubwa,
Kwa taji kichwani, miiba na zihaka,
Kwa haya ya damu dunia ilikupa,
Jibu, Bwana Yesu, Sifa yako juu.
Uliachwa mtini, ukikunywa kikombe,
Bila yeyote wakukusaidia ;
Sasa watukuzwa juu ya kiti cha enzi,
Na kwa sifa yako, mbingu zitangaze.
Uso wake Mungu, kwa saa ile kubwa,
Ulikugeukia, wewe Mwanawe,
Kichwa chako Kristo, kimeivikwa taji,
Inayotangaza sifa zako juu.
Ee Mwokozi Mwema ! Unayeabudiwa !
MwanaKondoo pekee unayestahili,
Hapa na mbinguni, yote ikutangaze
Nguvu na uwezo, na ukubwa wako.
Wimbo wakutukuza kwa sifa ya Baba
Unatoka kwetu, tulio wapendwa,
Wimbo wa milele ulioanza duniani
Umutukuze Baba na Mwana wake !
Kwa aliye tuokoa
Kwa damu’katusafisha
ufalme na ukuu ni vyake
MwanaKondoo astahili
utajiri, heshima, nguvu,
mamlaka, hekima, na sifa. (bis)
Tutukuze pendo, uwezo wa Mwokozi,
Kujishusha kwake na utiifu tele
Alija akashinda maadui wetu ;
Kwa msalaba wake – aliwamiliki. (bis)
Tutukuze wema wa Mfalme wa uzima :
Kwa ajili yetu aliteswa msalabani ;
Na kwa kifo chake alitukomboa ;
Tumepata kuwa – watoto wapendwa. (bis)
Tutukuze haki kamili ya Mwokozi ;
Alishinda nguvu za yule adui wetu ;
Alishinda kifo na alifufuka ;
Tumepata sifa – yake kwa milele. (bis)
Tutukuze ukubwa usiyo na mwisho
Wa yule aliyetoa uzima wake.
Akuja akingaa, na kwa macho yetu
Tutamutazama – milele mbinguni. (bis)
Ku’ngaa kwa Sura kamili ya Mungu
Mwana wa milele muabudiwa
Sifa kwako wewe ustahiliye
Kuheshimiwa na wote milele.
Ulishuka ili uwe zabihu,
Kwako tu Mungu akatukuzwa
Utakatifu, upendo, haki yake
Msalaba ukavikuza vyote.
Sasa umeinuliwa kwa Mungu
Karibu na ukubwa mbinguni
Twakuona na utukufu mwingi
Mwana wa watu uliyefufuka.
Twakuabudu wewe ambaye taji
Lakumbusha mateso ya kifo
Bwana Yesu tutakusifu wewe
Tukikizunguka kiti cha enzi
Watoa neema na kuzo
E Bwana Mungu wetu, katika Yesu !
Ubarikiwe na wateule wako
Wenye uheri kukuamini. (bis)
Ulitupatia neema,
iliyotupa usalama moyoni :
Wenye heri tutaingia mbinguni
Kunapo’ngaa uso wako. (bis)
Wewe watuwekea sifa
Iliyo ya MwanaKondoo mbinguni
Tutakuwa naye katika uheri,
tunda la kazi ya msalaba. (bis)
Mungu wa neema na sifa !
Wapendwa wako wanaye Roho wako,
Kwa jina la Yesu tunakuabudu
Yeye ni ukombozi wetu. (bis)
Kuabudu, kubariki na kufurahi
Kushangilia ushindi wa Bwana Yesu
Ni sehemu tuliyoitwaa kwa imani.
Jina lako lisifiwe, Neema yako
Iliyotujia katika uzuri
Tulikuwa gizani sasa uso wako
Waleta mishale ya nuru mioyoni.
Tupo wana wako, jina nzuri la Baba
Latujaza heri, hakika, amani
Roho wako mhuri, mwangaza na Mwalimu
Na karibu nawe tumekubaliwa.
Ni mapendo yako, kifo, uhai wako
Vilivyotuletea hii sehemu
Kila moja wetu asisahau kamwe
Kwamba tulitakaswa ili tumukuze.
Ukamilifu usiyoweza kusemwa
Wa uwezo, mapendo, hakiba’siyokwisha, – isiyokwisha
Mwana wa Mungu milele !
Utukufu wa mbinguni
Kwa amani yako, Kanisa lako pe ndwa
Lainama kuabudu (ter)
Wakaa ee Yesu, kwa kuume kwa Baba
Ukivikwa uwezo, nuru, utukufu – na utukufu
Mungu wetu (bis)
Mioyo zetu (bis)
Yainama mbele yako kwa kutii
Pia kukuinua. (ter)
Mbinguni kwa kiti cha Baba
Twakuona ee Mwokozi
Pumzikoni vile nuruni
Una uwezo na ku’ngaa
Kazi ya neema imekwisha:
Umekaa patakatifu ;
Juu utukufu umepewa
Watawala juu ya vyote.
Twashinda kwa ushindi wako
Yesu Mwokozi muweza,
Juu katika utukufu
Umetangulia wako !
Tuna tumaini la mbingu,
Linalokutegemea
Tuna uhakika wa roho
Ni Musingi wa imani.
Sifa kwa kichwa cha kanisa!
Bibi arusi mupendwa
Pande zako punde atakaa,
Akibariki milele
Wewe Bwana mwenye uzuri
Tutakaofurahia,
Na pendo lako la ajabu
Litakuwa siku zote.
Mungu wa pendo na neema!
Twafurahi kukutana
Mbele ya uso wako mzuri
Kuabudu na kubariki
Na Katika salama yako
Kweli Upewe ibada,
Iletayo mashukurani,
Marashi : jina la Yesu.
Bwana ingia nafsi zetu
Na wema wako wa ajabu,
Utuwashie moto wako
Wa pendo lako Ee Bwana ;
Ndipo sifa zitatokea
Mioyoni mwetu kwa Roho
Ili tuimbe rehema zako
Na pendo ndani ya Yesu.
Tunapenda kuketi pale
Twawekwa na kazi yake
Na tunafuata nyayo zake,
Hadi mbinguni alipo
Ni pahali patakatifu
Ambapo mlango ni wazi
Sifa za waamini zapanda
Kwako kupitia Yesu
Umoja wa Kanisa wapendeza
Bwana Yesu, wakufurahisha
Kwa kulipenda ulijitolea
Wataka liwe nawe mbinguni
Roho yako Yesu yatukusanya
Karibu nawe katika pendo
Heri gani kukuabudu pamoja
Twatangaza kufa na kurudi
Ni kutamu ndugu wakikuabudu
Roho wako akiwa kiongozi
Katika nyimbo na maombi yetu
Tunayokutolea pamoja.
Ni kweli palipo uwepo wako
ukileta uhuru moyoni
kila mwamini katika amani
asikia nguvu, uhakika.
Na Itakuwaje kwa mukutano
Mbinguni kanisa litakuona
Furaha gani isiyo na mwisho
utukufuni likikuabudu.
Ulitualika, tena kwa siku hii
Mwokozi Muabudiwa ili tulishwe
Katikati ya jangwa, wajenga meza hii
Kumbusho la pendo lako. (bis)
Kando yako, Bwana,kanisa lazunguka
Kukumbusha kifo chako hadi urudi,
Twavunja mukate, tunakunywa kikombe,
Kumbusho la pendo lako. (bis)
Uovu wetu ulikulemea kichwani
Mzigo wa uchungu na muzito sana;
Lakini kwa amani, tunasherekea
Kumbusho la pendo lako. (bis)
Tukionja mkate huu, na kinywaji hiki
Vinaelekeza macho yetu juu.
Na Punde tutamaliza safari yetu
Tutatambua u pendo. (bis)
Asante Yesu, Mwokozi na Mwaminifu!
Bila kivli tutakuona mbinguni
Na tutatukuza, kwa sifa ya milele,
Ukubwa wa pendo lako. (bis)
Unatuonyesha, (bis)
Yesu, mateso yako, kwa ukombozi wetu
Ukumbusho tamu (bis)
Meza matakatifu, Mwokozi muabudiwa
Tukumbushe pendo, kifo na kurudi. (bis)
Mkate na kikombe (bis)
Unavyotupatia, kutoka neema yako
Ni alama ya kweli (bis)
Visemapo kwa kimya, na vyapasha milele,
Kwa kila mteule, pendo lako Yesu ! (bis)
Tuimbe pamoja (bis)
Neema ile nzuri, na pendo la ajabu,
Ya Mwokozi wetu ! (bis)
Pamoja na shukrani, tukuze kwa uwezo,
Sote kwa umoja, Kondoo aliyekufa. (bis)
Sifa kwa Kondoo ! (bis)
Aliyejitolea,
Akatupatia haki,
Kafungua mbingu ! (bis)
Malaika wakuabudu,
Pokea shukurani
Ya watakatifu Waliokuja kwako. (bis)
Mwokozi muzuri ! (bis)
Twapenda kukumbuka
Tukingojea kuzo
Ya kurudi kwako (bis)
Tunaitaka sasa,
Tutapelekwa huko
Katika milele, Tutaimba wema ! (bis)
Kondoo uliyetolewa !
Twatazama pendo lako,
Kifo pia ushindi wako
Kwetu tuliokombolewa.
Tunazunguka meza yako,
Twatukuza pendo lako
Tukikuabudu Mwokozi mupendwa!
Tunangojea kurudi kwako.
Sisi tulikuwa waovu,
Tukapata msalabani,
Salama na neema nzuri,
Nguvu na heri pamoja.
Tunazunguka meza, etc.
Umetuvika haki yako,
Tumesafishwa kwa damu,
Twakumbusha toleo lako,
Lililofungua mbingu.
Tunazunguka meza, etc.
Fanya mpendwa ! Uzima wako
Uangae ndani mwetu :
Kila moja akutukuze,
Uliye tujaza mema.
Tunazunguka meza, etc.
Mbele ya kiti cha baba
Akaapo kwa heshima
Jicho letu latazama
Uzuri wako Bwana
Utukufu ulio nao
Ndani ya ku’ngaa kwako
Watuangazia kweli
Ndani ya mioyo yetu.
Kungaa kwa uso wako
Siko kuvutiapo tu
Kwani neema yako kubwa
Yaangaa usoni mwako
Kwa neema ulishuka
Duniani mwa uasi
Ulipotuchukulia
Maovu hata zambi.
Nafsi yashangaa sana
Juu ya upendo huu
Ulio mukubwa sana
Hauna hata mpaka
Hivyo sisi twatamani
Kurudi kwako hapa
Ili tuone, tutamke
Makuu ya pendo lako.
Tukaribie na kwa nyimbo zetu
Mwana Kondoo mupendwa akuzwe
Alishinda na alifufuka
Tutangaze makuu yake yote
Sisi wenye : kupendwa na Kristo. (bis)
Alitufilia kama sadaka
Tukapokea upendo wake
Kwa kutuokoa katika
Alikubali fimbo za uhaki
Akafanywa : chukizo, laana. (bis
Twakuabudu sadaka ya toleo
Wewe ulitununua sisi
Tukumbushapo kifo, mateso
Tunangoja siku yakuonekana
Mbinguni : kama bibi arusi. (bis)
Tunasherekea kwa meza hii
Pendo la Kondoo uliyechinjwa
Kwako roho zetu zinalindwa
Zikionja salama na uheri
Na kwa bei ulivinunua : ulivinunua. (bis)
Mbele ya kiti cha neema
Twakuabudu Mungu wetu
Tukiingia patakatifu
Kwa njia ya Yesu Kristo.
Mkate wa juu ushibishao
Ni chakula chetu kweli
Ndani ya Yesu tumepewa
Uzima unaodumu.
Pa’li pa kikombe kikali
Ulichomunywesha, Mungu
Mwokozi mwema na mupole
Ametupa cha wokovu.
Kwa sauti ya malaika
Tukinyakuliwa juu
Tutamuimbia sifa zake
Tutamuona… siku nzuri !
Ukitutazama Mungu,
Tunazunguka meza hii,
Twafurahi kuwa kando,
Kutukuza neema yako.
Pendo lako ni uheri ;
Linafukuza woga kwetu
Na chini ya ukingo huu,
Mwokozi, hazina yetu.
Tumesafishwa kwa damu
Yesu, hatuna tena taka ;
Tulikuwa wapotevu,
Twafichama kifuani mwako
Hatutanyanganywa kwako
Hatutatikisika kamwe
Kwani tuna tumaini kuu
Pendo lako ni imara.
Kwa wakombolewa wako,
Ni kutamu kukukumbuka !
Tunakumbusha pamoja
Mateso na ushindi wako
Mukombozi, pendo lako,
Ambalo tuna uarabuni,
Linadumu mioyoni mwetu,
Hadi utakaporudi !
Neema ya mbingu ! hazina ishangazayo !
Tunajua Yesu na mkono wa mapendo.
Alitukamata kutoka zambini
Aleteye Mungu – waabudu wa kweli. (bis)
Mungu Mtakatifu aliona haki
Ndani ya Adamu wa pili akimtukuza :
Ni mupendwa wake, anayemutaka,
Kwa sheria yake – alimupendeza. (bis)
Mungu ulimtoa katika mapendo yako
Aliitimiza yote kwa kutukomboa :
Yesu, haki yetu, utakatifu wetu,
Tumepata kuishi – milele kwa yeye. (bis)
Fumbo ya milele isiyoeleweka !
Ulituchagua katika neema yako ;
Na sasa ; ee Mungu, Roho wako daima,
Atufunulia – Mwana wa mapendo. (bis)
Yesu sadaka ya Mungu
Ulishuka duniani
Ukafunga ile shimo
Itutengayo naye.
Ukavaa mwili wa mutu
Ukateswa kabisa ;
Kwa Kuokoa kiumbe
Ukapata uchungu.
Ni wewe hekima yetu
Uhai na salama
Kimbilio kwa mateso
Wokovu wa milele.
Ee Mwokozi mwaminifu
Twabaki ndani yako
Hadi uzima milele
Waishi tutaishi.
Kwa kutuokoa, Bwana wa uzima
Alisumbuliwa na kuaibiwa
Sifa kwake Mwana
Sifa kwako Kondoo
Pokea mioyo yetu, mshahara wako
Ulioupewa, kwa mlima kalvari.
Kifo chako Yesu, kikaosha zambi
Ukafunga shimo kwa miguu yetu
Sifa kwake Mwana
Sifa kwako Kondoo
Twakusifu Bwana, ulitupa amani
Heri, ukombozi kwa mateso yako.
Kututajirisha, mwenyewe mbinguni
Ukawa maskini, wewe Mungu mkubwa
Sfa kwake Mwana
Sifa kwako Kondoo
Pokea mapendo na heshima zetu
Viwe kwako Mungu pasipo mwengine.
Mema ya pendo lako Mchungaji wetu
Unatuandalia meza kila siku
Sifa kwake Mwana
Sifa kwako Kondoo
Wapendwa wako Bwana wanafurahi
Wakionja pendo na matunzo yako.
Kwa amani twafwata uriti wetu
Wewe ni sehemu yetu kwa milele
Sifa kwake Mwana
Sifa kwako Kondoo
Mukombozi Mungu, unayetupenda
Upewe nguvu, ufalme na heshima.
Milele na milele tutakusifu
Pendo lako kubwa na ushindi wako
Sifa kwake Mwana
Sifa kwako Kondoo
Pokea mioyo yetu, mshahara wako
Ulioupewa, kwa mlima kalvari.
Nani atatukuza, nani atatambua,
Pendo lililokushusha toka mbinguni
Kwenda Getsemane,...Golgota ya damu
Pale ulipochomwa mkuki na Mungu.
Siyo wale, Bwana, majeshi wa mbinguni,
Ama vile vyote ambavyo uliumba
Ama urefu wa bahari na mbingu,
Vitakavyotukuza upendo wako.
Yesu ! Pendo lako na neema yako nzuri,
Nani atavikuza ? ni sisi waovu tu
Uliofanya wafalme, makuhani,
Kwa ajili yao ulionja kifo.
Wakombolewa tu, kwa raha takatifu,
Wataimba wema wako na kubariki.
Uliwanunua, Ee Yesu, kwa damu
Watakuwa nawe milele mbinguni.
Twakuona ukiangaika
Ukinywa kikombe kile
Tunakuona ukijitoa
Mtakatifu kwetu waovu.
Kifo chako sadaka safi
Tukitazame daima
Damu yako ilituosha,
Ikatufungulia mbingu.
Pendo lako ni kubwa Kristo
Linagusa mioyo zetu
Ulifilia ulimwengu
Wewe ndiye Mwokozi wetu.
Wewe uliyetuandalia nafasi
Tukiwa na wewe, tutaishi hapo,
Twataka tukuza haki na neema yako,
Pendo la Mwokozi, pendo lako nzuri. (bis)
Ee Bwana ! twakuja mbele yako kabisa
Kuonja utamu, ushirika wako ;
Hata hapa chini, wewe huonekane…
Tunangojea siku ya mukutano. (bis)
Ni wakati halisi kwa kanisa lako,
Utaliingiza juu mbinguni kwako !
Kwa salama yako, litaijaa sifa
Kwa karamu hiyo, pahali pa mbingu. (bis)
Tungojapo, Bwana, twatumia duniani
Chakula hiki, cha mapendo unayo,
Twatangaza humo neema iokoayo,
Mateso na kifo pia kurudi kwako. (bis)
Kama Kondoo ulikufa, Yesu
Kwa zambi zetu, Mukombozi wetu
Pendo gani ? ni pendo la ajabu
Kwa kutuokoa, Yesu ukafa.
Kwa ule wakati zambi zetu
Zilikuletea azabu kali
Kwa kufa ukavunja minyororo
Ukatuletea neema, raha.
Amen ! Bwana ! Uwezo na sifa
Kwako heshima, hekima, ufalme
Tangu sasa tunasema na wewe :
Ubarikiwe Ee Mukombozi.
Mwana Kondoo uliteswa
Ukachukua taabu yetu
Na ukatufanya kwa Baba
Wafalme na makuhani
Pamoja tunakuheshimu
Twakusifu na kukuinua
Nguvu, ufalme pia kutii
Mioyoni tunakuabudu
Amen ! Amen ! Bwana ! Amen.
Ewe Kondoo takatifu
Uliacha sifa za mbingu
Kapokea taji ya miiba
Ukatukomboa sisi
Tunaimba wakati huu
Wimbo huu bora wa ushindi
Ee mbele ya kiti cha sifa
Tutaimba pendo lako
Kuja, Bwana, Amen ! Amen.
Upendo wa ajabu (bis)
Kunyenyekea sana
Mwana akachukua mwili
Kakubali laana (bis)
Na akasulubiwa
Kuokoa kiumbe chake.
Kristo Mwana wa Mungu (bis)
Aliyetufilia
Kafufuka kwa uwezo
Tutukuze ushindi (bis)
Ushindi wake Yesu :
Ni sifa na tumaini.
Yesu ametukomboa (bis)
Ndani yake tu hai
Tumuimbie kwa furaha
Bwana katika mbingu (bis)
Unaketi mushindi :
Sifa kwako kwa milele !
Twakuona utukufuni
Ee Mwokozi !
Tukionja ushindi wako
Mwenye nguvu
Milele pamoja na Mungu
Kwa kuume kwa Baba Mungu
Uliyeshuka duniani
Na upole.
Kwa sisi ukawa laana
Ee Mwokozi !
Ukateswa zaidi sana
Ee Mwokozi !
Damu ’katoka mbavu zako
Ukatuondolea zambi
Kwa kufa kwako tunaishi
Ee Mwokozi.
Tunakungoja toka mbingu
Ee Mwokozi !
Ulisema waja kututwaa
Yesu mweza !
Furaha isiyo na mwisho
Yakutazama sura yako
Na vile yakukufanana
Ee Mwokozi.
Yesu, neema, damu yako
Na musalaba wako
Kungaa kwa uso wako
Vyatupatia haki
Nafsi yetu yapumzika
Ndani yako Mwokozi
Wewe mwanzo na chemchemu
Ya uheri milele.
Mwokozi Mupendwa, ni wewe tumaini !
Ulitukomboa kutoka mauti :
Aleluya ! Aleluya ! (bis)
Kati pendo lako (ter)
tumefurahi kweli.
Umetusafisha toka zambi kwa damu,
Sifa ya mbinguni itatupokea
Aleluya !Aleluya ! (bis)
Tuna tumaini (ter)
kutoka kwa imani
Katupenda mpaka kufa
Mwokozi wa mapendo
‘Katushindia shetani
Hadi kwa ngome yake. (bis)
Namna vilikulemea
Pekee kwa saa ya
Kuachwa pia na hofu
Ya zambi zetu nyingi. (bis)
Sasa fujo ya mawimbi
Yaliyokufikia
‘katuletea pumziko
Ya kazi yako nzuri. (bis)
Kando yako wateule
Wako hapa duniani
Sasa wanaonja raha
Ya nyumba yake Baba. (bis)
Kondoo wa Mungu Kristo akafa
Mutini (bis)
Pazia pale ’kapasuka
Kwa muti (bis)
Kwa patakatifu sana,
Mbele ya Mungu twafika
Kwako Yesu uliyejitoa
Mutini (bis)
Uliinuliwa toka chini
Mutini (bis)
Ulikunywa kikombe chetu
Mutini (bis)
Kwa pendo ‘kakimaliza
Damu yako ilituosha
Tumeokoka kwa milele
Kwa muti (bis)
Hayani sifa zako ‘kangaa
Mutini (bis)
Yesu uliupata ushindi
Mutini (bis)
Milele upewe nguvu,
Heshima na sifa nyingi
Kwa sababu ulishinda
Mutini (bis)
Nyimbo za mbinguni
Ni nzuri sana
Vinanda na nyimbo
Jaeni mbingu
Kwa nafasi kubwa,
ule wimbo mpya
Daima waanza
Kando ya Kondoo.
Kwa kiti cha enzi
Tutakuona
Ukivikwa taji
Za kila aina
Na mikono yako
Inaonyesha
Ginsi uliteswa
Kwa musalaba
Neema ya milele !
Uliye chinjwa
Ukajitolea,
‘Kamwanga damu
Kwa patakatifu,
Uheshimiwe
Mungu Baba yako
Aabudiwe.
Nyimbo za mbinguni
Ni nzuri sana
Vinanda na nyimbo,
Vyajaa mbingu
Heshima na nguvu,
Kuzo milele
Kwa Mungu mushindi,
Na Kondoo wake.
Mwana wa Mungu, wa ajabu
Waonekana usoni
Upendo muzuri wa Baba
Hata sifa zake nyingi
Washika dunia mkononi
Uliitosha utupuni
Vyote vinaimba Hekima,
Na kuzo lako Muweza.
Mbele ya Baba kifuani
Wamupendeza daima
Mupo mumoja uwezoni
Mupo mumoja pendoni
Ulipenda, siri ya ajabu
Kutoka patakatifu
Kuja dunia yenye zambi
Ili ufe Mwana Kondoo.
Upendo, neema ya ajabu
Twakuona Mutu, Mungu
Kwa sanduku hadi kalvari
Ukifwata njia chungu
Mugeni, ulikataliwa
Hata na walio wako
Ukanywa kikombe kichungu
Shambani mwa Getsemane.
Ukabeba, Mwana Kondoo
Kwa saa za giza mutini
Hukumu ya makosa yetu
Pia gazabu ya Mungu
Ee Bwana tutakutukuza
Milele kule mbinguni,
Na roho zetu zitaimba
Pendo lishindalo kifo.
Pendo safi, kubwa, lake Mungu mukuu,
Kwakujifunua katoa Mwana wake
Duniani humu, gizani mwa zambi
Sisi tulikuona na tukakugusa.
Ulingaa kwa muti kwa saa tatu za giza
Zilizo funika dunia ya upofu
Mtu Mukamilifu Mwana Mtakatifu
Kaona kuachwa, hasira, mauti.
Ukateswa Yesu, Mwokozi na sadaka
Jicho lako kaona ile shimo ndefu
Wewe wa milele ukabeba mzigo
Uliokuwa juu yetu milele.
Kasema « imekwisha » na akatoa roho
Na pazia ya hekalu ikapasuka
Safi twaingia mbele yake Baba
Katika mwangaza wa uso wa Mungu.
Kwa pendo la juu ushindi wa kifalme
Musalaba wako wamutukuza Baba
Na watuokoa, wajaza vinywani
Mwetu na wimbo wa waabudu wa kweli.
Mwana wa milele, wa pekee wa Baba
Unamufurahisha Baba pale juu
Mbele ya nyakati ulipenda dunia
Ulimokuja na kujishusha vile.
Ulifurahiya kukaa na wanadamu
Mungu akakuumbia mwili ukakuja
Munyenyekevu ukazaliwa chini
Siri ishangiliwayo na malaika.
Uliye tazama kwa ndani taabu yetu
Tulipokuwa kati ile shimo kubwa
Ukatuponyesha Mwokozi wa ajabu
Damu yako kamwangwa na kutuosha.
Kristo uliye hai tunaimba ushindi
Mungu alikuvika nguvu na heshima
Ukaja kututafuta tuone sifa
Tuwe nawe milele katika heri.
Kondoo mutukufu, Mwokozi wa mapendo
Uliyetupenda na pendo la milele
Tunakuzunguka tukijaa furaha
Tunakuabudu, barikiwa milele !
Wewe unayetupenda,
Mungu wa pendo, neema !
Twaingia hata mbingu
Kukuabudu siku hii.
Jamaa yako yakutana,
Ee Baba mbele yako ;
Ndani ya Yesu kanisa
Uliliweka kando kwako.
Sifa gani kwa watoto
Kukutazama Mungu,
Na kuuimba ushindi
Wa Yesu aliyekufa !
Jamaa yako yakutana,
Ee Baba mbele yako ;
Ndani ya Yesu kanisa
Uliliweka kando kwako.
Neema gani Baba Mpendwa,
Kujua pendo lako,
Tukingoja duniani
Kurudi kwa mwanawe !
Anakuja : heri gani !
Kanisa lake imba
Punde utamufanana
Mukombozi na Muweza.
Kukupenda, kukujua
Na kupumzishwa nawe
Wewe rafiki na Bwana
Na kinywaji na mkate
Kuonja neema yako
Ya kifo chako Bwana
Twaonja utakatifu
Utamu gani kwetu.
Heri itushangazayo:
Wewe kuwa mchungaji
Msaada wetu kila siku
Na haubadiliki
Katika upendo wako
Ukashuka duniani
Kutafuta kondoo zako
Na kuzikumbatia.
Watujaza neema yako
Watujua kwa jina
Watuongoza njiani mwako
Tukienda mbinguni
Kwa unyonge na makosa
Wewe ni msaada wetu
Unataka kwa upendo
Kutusamehe sisi.
Yesu rafiki yetu mkubwa
Pendo gani !
Atupenda kushinda ndugu
Pendo gani !
Jamaa, rafiki, wanapita
Heri yaja na kutoweka
Moyo wake tu hauchoke
Pendo gani
Yu uzima wetu milele
Pendo gani!
Na kwa milele tutukuze
Kazi yake !
Kwa damu yake tumeoshwa
Alipotukuta jangwani
Kwa neema akatuokoa
Pendo gani !
Alijitoa kama zabihu
Pendo gani!
Anapenda kutubariki
Pendo gani!
Nafsi yetu imusikie
Kwa amani, kamwe, isiogope
Iishi karibu na Yeye
Kwa upendo.
Tayari kwetu pambazuko
Ya uheri usiokoma
Bwana kwa wakati kidogo
Tutakumbatiwa nawe. (bis)
Wakati utukimbizapo,
Tunakutumainia,
Punde taabu itakwisha,
Wewe ni pumziko letu. (bis)
Sifa nzuri kuzoni mwako
Utaonekana kwetu’,
Na Kwa kelele ya ushindi,
Yesu utatutwaa kwako. (bis)
Bwana Yesu, mwenye mapendo kubwa
Wewe, kungaa kwa sifa za Mungu
Uje Bwana! Tuone uzuri wako
Twakungoja, tukitazama juu.
Katuokoa, sisi ni kazi yako
Mbinguni tutakutumikia
Tutakuona, na kufanana nawe
Na milele tutakuabudu.
Aleluya, ni raha takatifu!
Arusi ya Mwana kondoo yaja
Kando yako tutaimba milele,
Ee mupendwa, ule wimbo mupya.
Yesu ! jina lako kwa nafsi aminifu,
Ni kubwa na nzuri !
Linatukumbusha pendo na neema yako,
Wokovu muzuri ! (bis)
Mwana wa aliye juu, wewe mpendwa wa Baba,
Sifa ya mbinguni !
Ulituletea, katika nuru yako,
Zawadi za Bwana. (bis)
Kwa wenye zambi, watoto wenye hatia
Wastahilio kufa,
Ulileta mema yapitayo fahamu
Na amani ya Mungu. (bis)
Nafsi zetu zimekuwa zako Mkombozi :
Tupo mali yako
Zaa ndani yetu moto wa pendo lako,
Tuishi kwa imani. (bis)
Utukumbatie, ee Mwokozi wa nafsi !
Utupe salama
Tuongezeye moto wa uhodari wema
Tuongoze milele. (bis)
Pendekezo letu ni kukukaribia,
Wewe Emanueli !
Pendo lako kwetu, chemchemu ya uzima,
Kweli ni daima. (bis)
Tukuzwa, Mwokozi ! pendo lako aminifu
Halibadiliki ;
Ulitupumzisha chini ya bawa lako,
Kwa milele yote. (bis)
Mbinguni tuna Baba mwema na mupendwa,
Aliyetoa agizo zamani :
Mungu mwenye nguvu ni tumaini letu,
Akiwa juu akinga watoto. (bis)
Alitupatia uzima wa mwanae
Akituokoa kwa damu yake
Alitutayarishia sifa milele,
Yesu pekee ni njia ya mbingu. (bis)
Hekima, neema na ufalme vyaambatana
Kutuongoza pahali pa heri
Matunzo yako kwetu Mungu yanadumu;
Usiku, mchana watutazama. (bis)
Musaada, nguvu kwa siku ya jaribu
Neema, msamaha, tegemeo,
Vyatoka kati roho yako kama muto
Usiyokoma na kukauka. (bis)
Kwa pendo kubwa hii, tukupe nini Baba ?
Utupe mioyo ya utiifu
Nyuso zetu ziangaze tabia yako
Roho wako apambayo wako. (bis)
Zizini mwa Yesu tule kwa uhakika
Tuonje neema kubwa ya mchungaji mukubwa
Tunywe maji yale yatiririkayo
Kutoka kiti kile cha pendo lake.
Tupumzike katika zizi yake nono;
Hatutaogopa hata zoruba kubwa;
Yesu ni kwa upande wetu daima :
Tubaki daima kando ya mchungaji.
kwa ajili yetu roho yake yawaka ;
Katika unyonge aonyesha fazili,
Unyonge wetu njoo uhodari wetu ;
Amtegemeaye anaweza yote.
Kazi ya milele, tutakapo pumzika
Bila mwishowako watakuabudu
Wakitupa taji juu ya miguu yako
Wakistaajabu na watainama. (bis)
Tutautazama uso wa Muabudiwa,
Uzuri wa Mwokozi, Bwana Arusi
Na tutavumbua fumbo isiyopimwa
Ya neema na mapendo bila mpaka. (bis)
Kwako pekee Yesu, kwa nuru yako nzuri
Wewe jua la haki liangazalo
Kanisa litavaakatika utukufu
Nuru
Utaona pekee lile unalotaka !
Tunda kamili la kazi ya msalaba
Utafurahia kazi ya nafsi yako
Mapendo yako Mungu yatatosheka. (bis)
Ndiyo, raha kubwa sana,
Uheri hapa chini,
Ni kufuata Bwana Yesu,
Hatua kwa hatua
kwa pendo atupendalo,
Hakuna kizuio ;
Alitununua kwake,
Ni wetu kwa milele
Pendo lake aminifu
Halitatukosea :
Ni kisima cha milele
Ambacho kitadumu.
Ikiwa anapendezwa
Tumupende kabisa,
Ni sababu yeye pekee
Hatabadili pendo.
Uliyevunja vifungo
Yesu Kristo Mwokozi !
Katika haya na taabu,
Watufariji sisi
Kazi ya neema yako
Imetukamilisha;
Na tupo mshahara wako,
Yesu, Bwana arusi
Ulituponyesha sisi ;
Nafsi yetu, daima,
Ikutumikie wewe,
Ikikufurahia.
Twaishi kwako, chemchemu njema
Tufurahie nuru yako
Kukuona mbele ya Baba
Yesu, pumziko ya roho yetu.
Mungu alitutolea Yesu
Na kwake akaleta amani
Akapendezwa na uhaki
Deni yetu kweli imelipwa.
Tuna heri, Bwana wema wako
Umetufungulia mbingu
Na mukristo kwa utulivu
Aingia kwani ameokoka.
Kwa nini tusikupende Yesu ?
Uliyejitolea kwetu
Wewe ambaye pendo lako
Laja kila siku mbele yetu.
Watufunza, watufariji
Yesu ukiwa mbinguni
Kwani Roho na neno Lako
Vyabaki na wateule.
Twasikia sauti yako
Kupitia neno Lako
Roho wako hufahamisha
Agusa moyo na macho.
Kumbukumbu La pendo Lako
Lafikiawalio wako
Katika Jangwa watukuzwa
Twaonja mema ya mbingu.
Hilini Neno La uzima,
Kama tunda La Eskoli
Linalotupatia nguvu
Jangwani tulikulapo.
Muda kitambo kazi yake
Itakwisha kwa kundi hii
Tutakapo kuona nuruni
Tutazungumuza nawe.
Tuimbe, wandugu, wema wa Baba wetu
Wema wa ajabu !
Jina lake nzuri liinuliwe popote
Na watakatifu ! (bis)
Nani kuliko jamaa aliyochagua,
Atamutukuza ?
Malaika gani atasema vizuri
Mbele yake Mungu. (bis)
Tutukuze yule anayetutakia
Kuzo ya juu sana
Utukuzwe Baba, heshima iwe kwako
Kwa mapendo yako ! (bis)
Kwetu, wakristo, ni heri
Tutakapouona
Uso wa Yesu Mwokozi
Mbinguni juu ya vyote ! (bis)
Kuwa nawe juu mbinguni,
Tukifanana nawe,
Tukitamka na waheri
Sifa zako milele. (bis)
Kuwa nawe na kuonja
Uzuri, wema wako,
Wema wako raha yetu,
Furaha kubwa gani. (bis)
Kwani kwako ni pumziko
Tunalotumaini,
Ni mwisho wa kazi zetu
Nyumbani mwake Baba. (bis)
Tusikie Bwana arusi
Anayetuambia
“Ninaja! Mufarijike,
Hakuna fazaiko” (bis)
Bidii kwenu wasafiri!
Tunyanyuwe vichwa juu;
Haraka! Viuno vifungwe:
Wokovu ni karibu. (bis)
Yesu, Nguvu, Mwamba wangu
Mwokozi wangu mkuu
Adui hawataweza
Nikilindwa nawe.
Kwa Neema ulinisamehe
Umenipa mbingu
Ninazungukwa na nguvu
Imani yatosha.
Wewe ndiye Mukombozi
Na mwenye upendo
Wewe ni uheri, sifa
Na Mwokozi wangu.
Ndani yako, Yesu nakuja,
Kwake Mungu bila woga,
Mbele yake, bila taka yote
Nina kubaliwa kwake.
Ndani yako, ninapumzika;
Ninajua uwema wako,
Moyo wako ni kimbilio
Damu yako ilininunua.
Ndani yako, hakuna shaka
Jangwani nisijali,
Ulinipasulia njia,
Nalindwa na pendo lako.
Niko nawe kifo kikija,
Ninangoja bila woga :
Ninaishi uzima wako,
Nitaishi sawa na wewe.
Ni kwa Baba mwenye nuru
Kutokapo zawadi
Jibu maombi yangu,
Apenda kubariki.
Baba mwenye kurehemu,
Msaada wangu saa zote ;
Neema yako inanipa
Kujua pendo lako.
Pendo gani la ajabu
Nilipatalo kwako
Pendo lako kubwa sana,
Hazina ya mkosaji.
Nyumbani patakatifu
Ninakukaribia
Niishi wala nikufe
Mbingu ni wazi kwangu.
Sifa kwako, Baba Mungu
Kanipenda wa kwanza
Niko na samani kwako
Mimi ni mali yako.
Neno lako ni aminifu
Bwana halipite kamwe
Nafsi yangu iliaminiyo
Haitaogopa tena.
Ninajuwaee wazo nzuri
Miongoni mwa kondoo zako
Hakutapotea yoyote
Mchungaji uliahidi.
Wana wa pendo lako kubwa
Tupokifuani mwako
Hata dunia na kuzimu
Havitatutosha kwako.
Bwana wangu mwema
Uliniponya
Nipo mushahara
Kwa kazi yako
Nilikuwa mnyonge
Sasa ni wako
Neema yako nzuri
Kaniokowa.
Chunga kwa rehema
Nafsi milele
Katika furaha
Na usalama
Unishike mkono,
Nisilegeye
Nichunge daima
Karibu nawe.
Ee Mwokozi, mapendo ya ajabu,
Ee Mchungaji, nijuaye sauti !
Kwa Kondoo, katika pendo lako,
Ulikubali kufungwa mtini.
Nimechoka na kukosa bidii ?
Unionapo waniponya yote
Wanilisha na majani mabichi,
Wanitajirisha na zawadi.
Nina kiu ? Kandokando ya maji,
Waniongoza kwa uaminifu ;
Ninapata ndani yako kisima,
Cha kuninywesha hadi milele.
Wewe Yesu, nguvu ya nafsi yangu :
Kila saa naona pendo lako
Ulinitosha motoni milele,
Kunipeleka pahali pa juu.
Msalaba, mauti na neema yako,
Ni uheri wa kondoo zako ;
Ee Mwokozi ! Timiza na tukuza
Nguvu zako 'zaifuni mwangu.
Nitaimba sifa na mema yote
Ya wokovu na upendo wako
Ee Mwokozi ! U tumaini langu
Katika imani waniongoza.
Wakristo, tusifu na tukuze pamoja
Jina la Mkombozi !
Anatukusanya sisi wapendwa wake
Tutukuze Bwana. (bis)
Malaika wa Bwana anatuzunguka
Watoto wa Mungu,
Anawakomboa na kuwachunga pia
Katika hatari. (bis)
Tunaonja, Bwana, mbele ya uso wako,
Pendo lako la juu
Mutu wa uheri ni yule tu ambaye
Anakuamini ! (bis)
Ni ndani ya Mungu
Kwa tumaini lote
Mioyo yapumzika
Uvumilivu wako,
Rehema yako kubwa
Vinanionyesha
Matunzo ya pendo.
Ni kutamu kwangu !
Kuwa wewe ni Baba
Yu nami popote
Waniangazia neema
Wapokea maombi
Unanitazama,
Wanipa imani.
Salama na pendo
Furaha kamilifu
Ni vyangu milele
Naona mbele yangu
Njia nzuri ya raha
Ni ya utukufu
Yaenda mbinguni.
Bwana niongoze
Ukinishika mkono
Linda nyayo zangu
Mungu kwa pendo lako
Nguvu, hekima yako
Vinatuzunguka
Ni msaada wa nguvu.
Pendo kubwa na la milele
Lake Kristo
Damu yake ilimwangika
Kwami, muovu
Yaniokoa toka shida
Na kunipokonya mauti
Na kuchapa sura ya Yesu
Juu yangu.
Anisimamishaye mimi ?
Yesu kristo
Ahimizaye nafsi yangu
Yesu kristo
Yesu alisema : ninaamini
Nipige vita kumtukuza,
Ngao na ushindi wangu ndiye :
Yesu kristo.
Ninaenda kwa Baba yangu
Njia ni Yesu ;
Nina heri na raha tele
Kwake Kristo ;
Hata kama ndani ya ziki,
Moyo wangu una tumaini,
Ni kwa sababu niliamini
Yesu kristo.
Ninafurahi ndani yake
Yesu Kristo ;
Duniani, mbinguni naishi
Kwake Yesu
Punde, kwaheri vya dunia !
Mbali na ninyi nina bawa,
Kwenda makao ya milele
Kwake Yesu.
Nikufikilipo Bwana
Pia neema yako
Moyo wangu wafurahi
Kwani utakuona. (bis)
Hata kama ninachoka
Ninasonga mbele tu
Kama mahali pakavu
Kunakoota miiba. (bis)
Hata adui ni wengi
Kwa kunishambulia
Kwa mitego ya hatari
Wanizunguka sana. (bis)
Ninaweza kila siku
Kufuata njia yako
Na kwa pendo lako kubwa
Kuonja lifaalo. (bis)
Bwana, pumziko na Mwamba
Wokovu, haki yangu
Wanikaribia mimi
Wanipendeza mimi. (bis)
Yesu, Mukombozi wangu
Nijaze uhodari
Wezesha mtumishi wako
Akuwe mwaminifu. (bis)
Hadi siku wateule
Washindi ndani yako
Wakivaa kanzu nyeupe
Watakuona kuzoni. (bis)
Katika uzaifu
Tunaona juu
Na Mungu wa mapendo
Atulinda sisi
Hadi patakatifu
Njia iko wazi
Kwetu sisi ni Baba
Mungu wa salama.
Na katika mateso
Tunaona juu
Ambapo Yesu Kristo
Atashuka punde,
Mwokozi mwaminifu
Atatunyakua
Kanisa lakuita
Bwana Yesu kuja.
Tukuzwa Baba wetu !
Tukuzwa Kondoo !
Hakuna tena taabu
Tukitazama juu
Tupatie bidii,
Imani na pendo ;
Nafsi yetu ingoje
Kurudia kwako.
Mungu twakuabudu, uliye mukarimu,
Tukiwa gizani ulituangazia
Pendo lako kwetu,
Lilijaa mioyoni
Usalama wako, zawadi ya neema.
Radi za torati zilizima kabisa,
Mwana wako alipobeba upotevu
Na watoto wako,
Ni wenye ushindi,
Kwa mabaya mengi neema imelipa.
Pendo lako Bwana, linatufungulia,
Msaada wa Roho, hazina ya salama ;
Na kwa mema yako
Tumeshirikishwa
Kwa uvuli wako unatuficha sisi.
Tukifwata njia, utuongoze ee Yesu,
Na tupewe kungoja kurudi kwako
Tu wapendwa wako,
Twaenda mbinguni
Ambako jina zetu zimeandikiwa.
Sifa kwake Bwana, Mungu na Baba wetu
Anayetujaza mema kila siku
Atupenda sana kuliko mama mpenzi :
Pendo lake halilinganishwe kamwe.
Uliutangaza huu upendo bora
Ee Mungu wa pendo ! kwa zawadi nzuri
Ya Mwokozi wetu, Yesu, mwana wa pekee
Aliyesulubiwa tuhurumiwe.
Watujaza pendo, Mungu mwema, mhekima,
Mioyoni kwa Roho wako tulipewa ;
Yeye ni ndani yetu akishuhudia
Neema kwa Yesu iliyoturehemu.
Katika pendo hii, Mwokozi mwaminifu,
Utuchunge hadi utakaporudi
Utupe uhodari tuombe na tungoje
Wewe na tubaki katika pendo lako.
Tumutazamie Yesu,
Bado kitambo Mwokozi
Atarudi toka mbingu,
Katika kungoja kwa heri
Nafsi zetu ziwe tayari
Tuwe macho, tusilale
Wakristo, Mwokozi aja.
Mungu anatupenda
Na tufurahi !
Tunakumbatiwa
Na pendo lake !
Refrain :Tumusifu Yeye,
Tuonje mema
Tuimbe ushindi
Wa Mukombozi.
Ee Mungu Muweza !
Ona hitaji,
Wewe ndiwe Baba,
Unatujali.
Katika safari
Watufuata ;
Unatupa moyo !
Tunapochoka.
Roho wa neema
Atuhimiza,
Atuonyesha wewe,
Mwokozi wetu !
Tumaini letu,
Mungu wa pendo !
Tumaini letu
Ni wema wako
Tumusifu yeye, etc.
Tuende mbele kwa furaha tele,
Katika nyumba ya wenye heri,
Ambapo Yesu anatuombea,
Tuende mbele ndiyo inchi yetu
Tuende mbele tukifurahi
Katika nyumba ya wenye heri.
Nyimbo za pendo zitaimbwa juu ;
Nyimbo tamu za walio na heri !
Na tutashiriki kwa nyimbo hizo
Tutakapofika nyumbani mwetu
Tuende mbele kwa furaha tele
Katika nyumba ya wenye heri.
Toka mbingu twakungoja, Bwana,
Kwani sisi tupo mali yako.
“Kuja, Yesu” kanisa linaita ;
“Tupokee utukufuni mwako”
Pale tutafurahi daima :
Ndani ya nyumba ya wenye heri.
Heri, punde katika inchi mpya,
Tutaimba sifa zake Kondoo ;
Hakutakua msiba na kulia,
Wala zambi kwa fasi nzuri hiyo ;
Raha tele pamoja na Yesu,
Pendoni mwake tutafurahi !
Kamwe Mungu haache
Amtumainiye ;
Dunia ikinitesa,
Nina tegemeo.
Na huyu Mungu Mwema
Anachunga wake
Anawapa uzima,
Anawapa mema.
Najua ananipenda,
Nataka anitunze :
Vema kuliko mimi,
Ajua hitaji
Huyu Mungu wa pendo
Hataniachilia
Sivyo, kama mabaya,
Yakija yu nami.
Ee Mungu uso wako
Waangaza juu yangu,
Unipe neema yako
Niishi yote kwako.
Hadi siku yakuitwa
Kuingia kwako,
Unipe uaminifu
Wakukufuata.
Heri aliye na nia
Ya kumufwata Bwana !
Yesu anavuta
Kwa upole,
Yote yafwata Heri yake. (bis)
Muchungaji amwitaye
Anamuweka huru.
Ni mwaminifu
Ampa nguvu,
Na bidii mupya Ampatia. (bis)
Mkono wako wamukinga :
Anakutegemea.
Muovu akimtisha
Ila mbele
Mtego waanguka Mbele yako. (bis)
Heri aliye na nia
Ya kumufwata Bwana !
Yesu anavuta
Kwa upole,
Yote yafwata Heri yake. (bis)
Muchungaji amwitaye
Anamuweka huru.
Ni mwaminifu
Ampa nguvu,
Na bidii mupya Ampatia. (bis)
Mkono wako wamukinga :
Anakutegemea.
Muovu akimtisha
Ila mbele
Mtego waanguka Mbele yako. (bis)
Kamwe sitapungukiwa
Kwani Bwana ni Mchungaji
Ninaishi chini ya gongo
La asiyebadilika
Kweli Yesu ulinitia
Miongoni mwa kondoo zako.
Ulinipa salama yako
Najua ulinipenda
Nikipita katika moto
Najua sitaungua
Macho yako ni juu yangu
Ongoza yangu juu yako.
Bwana nikukaribiapo
Sioni woga yeyote
Neema yako ni mwamba mkubwa
Kimbilio haki kwangu
Ulinishika mkononi
Shetani hata nitosha.
Watoto wa Mungu tuishi
Tukiungwa katika pendo ;
Ni utayari wa milele
Wa wanao barikiwa.
Tukiwa tumenyweshwa pale,
Tuwe na nia moja tu ;
Tuendelee safarini,
Tukitazama Mwokozi.
Bwana uwashe moto wako
Utuongezee imani ;
Na kutokea mioyo yetu
Wimbo upande kwako juu !
Tufurahi wakristo ; (bis)
Bado kitambo Yesu,
Ndani mwetu atatukuzwa
Bwana utarudia, (bis)
Tutakutana nawe
Na tutaishi ushindi.
Kanisa ni ligeni
Sasa hapa chini :
Ni fasi ya unyonge,
vita, machafuko.
Ila kwa mkono wake,
Yesu atalitwaa
Mbinguni kwa ushindi,
Daima atakaa. (bis)
Pumziko ni karibu ;
Vita vitakwisha
Tuinue vichwa juu ,
Kwani Yesu aja.
Yeye Mwana wa Mungu,
Mwokozi milele,
Tukivuka dunia
Twatazamia juu,
Twatazamia juu.
Giza linatoweka;
Ee ndugu tuamke:
Muda kitambo sasa
Tutaona Bwana.
Na kwa furaha nafsi
Imufurahie
Kwa Roho wa uzima
Tuite “njoo Bwana”. (bis)
Siku gani tutaona
Kanana ya mbinguni ?
Juu ya mbingu mwasikia ?
kristo anatuita.
Na tutaishi naye,
zoruba itakoma
Tutaimba kwa milele
wimbo wa salama.
Refrain : Heri kamilifu, Uheri, uheri
Heri kamilifu, Pumziko ni Bwana
Kanisa litakapokusanyika mbinguni
Litaimba bila mwisho :
Sifa kwake Kondoo.
Wateule wataona,
utukufu wa Kristo
Wakiwa wamefufuka,
watamshuhudia
Wakisifu ushindi,
kazi ya musalaba
Pamoja kando ya kiti,
tutampa naziri.
Kama kule juu mbinguni,
mwenye zambi akitubu,
Malaika kwa umoja,
wabariki Bwana
Itakuwa furaha,
wakati kundi lake
Litakapo kombolewa,
nakushinda vyote.
Kanana ni fasi nzuri,
Ni inchi ya ahadi
Tukikusanywa na Mungu,
kwa upendo wake
Tutaimba milele
wimbo wa kufurahi
Utasikika mbinguni,
Milele daima.
Siku hiyo ya milele,
itaangaa asubui
Sote katika umoja
Na mapendo pia
Na tutasema tena
Na yule Muabudiwa :
Mwana Kondoo astahili
nguvu na mamlaka
Heri kamilifu, uheri, uheri, etc.
Neema yako kubwa,
Mungu wa pendo,
Yapita maisha
Kwa waaminio.
Refrain : Watoto wa nuru,
Tusifu Baba
Anayetupenda
Yeye ni pendo.
Neema yako Baba,
Kwa wateule,
Mbele yako wewe,
Na ndani ya Yesu
Neema yako ya juu
Kwa wasafiri
Ni tamu kabisa,
Mioyoni mwetu.
Duniani humu,
Mungu wa pendo,
Neema yafurika
Hadi kwa milele !
Watoto wa nuru, etc.
Kati wanyanganyi
Katika mateso
Alikufa
Mtakatifu pekee
Pale msalabani,
Alivunja nguvu
Ya muovu.
Yesu alifufuka
Alipanda juu :
Tulimuona.
Yesu ni Kiongozi,
Anatuongoza
Ana nguvu kweli
Tunajua.
Atatoka mbingu :
Na kutupeleka ;
Tuishi naye
Asema : « nakuja »
Tuchunge hazina
Tukeshe usiku
Tujiandae.
Yesu hadi leo,
Mbingu, kao lako
Tufundishe
Tukinge vitani ;
Tuongoze kwa lengo
Rahani, kilioni
Utuongoze.
Mungu, chunga wako ;
Wamimiye mema ;
Wahimize
Kukutumikia,
Na kukushukuru,
Wajingojee kwako,
Ni sheria.
Kupenda, kuabudu,
Kutangaza pote
Mbele yake ;
Kumupenda Yesu,
Kutangaza mema,
Kufwata bendera,
Ni mapashwa.
Niwapo na fasi mbinguni
Hapa chini nina amani ya roho
Mbali ya mawimbi na zoruba
Niwezapo pumzisha kichwa
Kifuani mwa Mwokozi
Juu nyumbani mwa Baba yangu
Ndani yako Yesu nina vyote
Vyote vya pa’li patakatifu
Bwana, uso wako, nuru yangu
Wanipa sifa na pendo.
Tunaweza kukufuata
Njiani mwako Yesu
Ulimopenda kuishi
Ukiwa mgeni kwetu
Ulikuwa pekee yako
Ukitenda mema tu
Katika njia hii nzuri
Yako mtu mkamilifu.
Hiyo njia yafungua
Mema,
Mungu mwenyewe atambua
Humo utakatifu
Hivi kwa neema yako
Twaweza kukufuata
Kwani ulituokoa.
Wabarikiwa wako.
Mwili wetu ukiteswa
Sikitiko na taabu
Tunapoonja uchungu
Tukufuatapo, Yesu
Juu yako twatazamia
Katika uzaifu
Utakatifu wako.
Njia hii yaishia
Inchini penye sifa
Palipo uso wa Mungu
Na wa Mutu mushindi
Tukiwa wakamilifu
Kuzoni tutaabudu
Yesu tutakufanana
Tutashibishwa nawe.
Jangwani nifuatamo njia yangu
Kuelekea inchi ya kuishi,
Kusiwe kizuizo hata kazi
Kwani mbingu ni uriti wangu.
Mwokozi ni Kiongozi, tumaini
Nichunge na hatari ya siku.
Uniangazie kwa usiku
Unichunge pendoni mwako.
Kila asubui mapendo yako
Yanitumia kila siku mukate.
Jioni ninapolala salama
Wewe unahusika na kesho.
Mwamba wangu ! Maji
Yatiririka kuniondolea kiu
Kwa Roho wako unichunge
Moyo wangu usinungunike.
Hivi sasa mwisho wa njia yangu
Utaniletea pumuziko ;
ushuhuda hakika wa Bwana
Unanikinga na mawimbi.
Inchi yangu, ee inchi ya ahadi
Moyo wangu sasa wakusalimu
Katika raha tele takatifu
Jina lako Mungu lisifiwe.
Bwana pekee, nguvu, uzima wangu :
Hakuna awezaye kunitisha
Uwezo wake mkubwa :ngao yangu
Mutu hawezi kunishitua.
Hata kama kambi nzima ikuje,
Wajali na hiyo moyo wangu ?
Hata kama msaada ukikosa,
Nina Mwokozi mwenye uwezo.
Kama mama mpenzi akiniacha,
Sitapata msaada kwa mutu,
Muweza, Baba na muaminifu,
Ataniokoa akishika mkono.
Nafsi yangu, ukiwa matesoni
Ngoja kwa Mungu neema, msaada ;
Umutumainie pekee yake :
Mkono wake utakupa nguvu.
Kristo ndiye salama na wokovu ;
Nguvu yangu Kiongozi wangu ;
Pendo lake litanipa ushindi :
Siogopi, Yesu yupo nami.
Ee Bwana pendo lako,
Ee Mchungaji Mwema,
Wanizunguka mimi,
Nakingwa zikini.
Wanibeba moyoni,
Nichokapo mimi ;
Mkono wako wa nguvu
Wanishika mimi.
Mikono yako Bwana,
Ilitobolewa,
Iliumizwa na watu
Ulipotufia,
Na kwa mateso yale
Uyakumbukayo ;
Mikono ni tayari
Ili ibariki.
Mufano wa kufwata,
Moyo wa Mwokozi,
Mwaminifu msaidia,
Mkamilifu kweli,
Mpole wa kufuata
Bila hata woga
Nataka kuishi nawe,
Uliyenifia.
Nani atatuhukumu
Sisi wachaguliwa ?
Nani atatushitaki,
Tuliopata haki ?
Mwana wa Baba,
Alifufuliwa,
Avikwa nuru,
Alipanda juu.
Tukiwa tunasumbuka
Anatusaidia,
Na tunashinda zaidi
Ndani ya atupendaye.
Yesu alitukomboa
Toka kifo milele ;
Yeye ametufufua,
Anatuita mbinguni
Hakika tamu
Kuishi mbinguni !
Ni tumaini
Kwetu tuliopendwa !
Kwa mufalme wa milele,
Mkubwa, mwenye hekima,
Iwe heshima milele
Pendo, uwezo na sifa.
Tutaona siku gani
Siku yakuonekana
Kwa atokaye mbinguni,
Yesu Kiongozi wetu ?
Na siku nzuri,
Ya mwisho wa kazi !
Imani nzuri,
Na pumziko tamu !
Wakristo kwa muda mfupi,
Bwana wa utukufu
Atakuja kuwalipa
Wapiganaji ushindi.
Kuokolewa kutoka inchi
Ya utumwa, zambi, giza
Tunatarajia uriti
Tukiongozwa na Roho.
Huko hatutalia tena
Kazi, kiu vile njaa
Hakuna hatari, kilio
Ni amani, uheri tu.
Milele pamoja na Kundi
Upendoni kwa furaha
Tutakusifu kwa milele
Kondoo uliyetufia.
Kujeni wapendwa, tuchote kwa furaha
Amani na neema kwa chemchemu
Tutangaze mema, tuinue upendo
Wa Mwokozi anayetuponya. (bis)
Tutakutukuza, Bwana nyimboni mwetu
Tunaojua mapendo yako
Ulitutendea mambo mazuri
Tutakubariki siku zote. (bis)
Twakuabudu Yesu, Mwokozi wa mapendo
Uliyetuokoa kwa damu
Twaimba upendo wako hapa duniani
Mbinguni tutauimba daima. (bis)
Furaha gani, tunyakuliwapo
Yesu akirudi
Na milele Kanisa litakwenda
Mbali ya dunia. (bis)
Wakati mzuri, Kristo atatuleta
Karibu ya Baba
Tutakapotukuzwa mbele yake
Kristo atatuingiza. (bis)
Kutasikika kule juu mbinguni
Nyimbo za heri tu
Wote watatangaza neema yake
Pendo la Mwokozi. (bis)
Shuka mbinguni, tunakuhitaji
Twakupenda, kuja
Tangu zamani tunakungojea
Bwana arusi njoo. (bis)
Wateulewako
Katikavita,
Wakutapohapa
Unyongemwingi,
Mbinguniwabebwa
Moyonimwako
Eekuhaniwetu
Mukubwasana.
Ukijaanawema
Napendopia
Hautamsahau
Mukombolewa
Niwewemsaada
Katikavita
Unatutetea
Mungu Mtetezi.
Kwakilauchafu
Niwewepekee
Utusafishaye
Miguukwamaji
Wasema : mwamini
« Niigemimi
Mufanokamili
Mtumishimwema. »
Tundalaushindi,
Wakombolewa,
Watakuwanawe
Kuzonimwako
Nyumbanimwa Baba
Usonimwake
Tumepewakazi :
Nipendolako.
Neema gani Bwana, kuitwa ndugu zako
Na kuwa na amani, tukikungojea
Ulitufungua kutoka shida zetu
Haki yetu, pendo lako. (bis)
Ni wewe uliyetusafisha kwa damu
Na moiyoni mwetu, ukaleta amani,
Yesu, mkate wa juu, chakula cha mbinguni,
Kwako tupo wa milele. (bis)
Mshindi wa shetani na dunia
Bwana Yesu amefufuka
Na Kwa woga wa
Siku nzuri inafwata
Hakuna woga, ziki tena
Enyi taifa teule,
Pamoja na furaha tele
Tuimbe Yesu amefufuka.
Siku yaja ya raha kubwa
Mwili huu utainuka
Umepandwa muharibifu
Utafufuka kuzoni
Miili yetu ya uzaifu
Itakapobadilishwa
Yesu utaifananisha
Na mwili wako wa kuzo.
Tayari kwa uhai wako
Yesu tumefufuliwa
Ndani yako, kwa neema yako
Tumepanda juu mbinguni
Kwa kungojea siku yako
Itakayoonekana
Tukikutegemea wewe
Tunapiga vita nzuri.
Usiku kati kasikika
Sauti : « Bwana anakuja »
Mumuone Yesu akishuka :
Na tujiunge na yeye
Refrain : Kanisa lijitayarishe
Kwa saa hii ya kukutana ;
Ninakaribia siku kuu :
“Mutazame Bwana arusi!”
Tumaini la utukufu
Linatupatia bidii
Tarajio la heri kubwa
La kuonekana na Yesu !
Kanisa lijitayarishe etc.
Wanaolala mavumbini
Kama sisi watamsikia ;
Na huko, mbali ya dunia,
Watamukutana Bwana.
Kanisa lijitayarishe etc.
Ni kutamu kupenda Mungu Baba
Kumwendea sawa, bila woga
Kufanya kazi hapa duniani
Tukiongozwa na Roho wa Bwana.
Ni kutamu kupata kwa saa zote
Rafiki mpendwa na msaidizi
Kuwa huru kuingia mbele yako
Kupata msaada hatarini !
Ni kutamu kuwaza neema yako,
Kwa Uzaifu na ulegevu
Na kusema : Alitwaa fasi yetu
Akateswa kama Mwana Kondoo
Ni kutamu kuona sifa zako,
Bwana Yesu, na watakatifu,
Kungoja kwa salama siku yako
Ya ushindi bei ya imani !
Siku gani mbele ya kiti chako,
Watakatifu wametukuzwa,
Kila moja akivaa taji yake
Wataziweka kwa miguu yako !
Haki yako kamili,
Ee Mwokozi ni uzuri
Na kuonekana kwa heshima
Kwa aliye kombolewa.
Uliturehemu kabisa
Na tumepewa zawadi
Pia uhakika imara
Twangojea siku kubwa.
Kwetu taifa kamilifu,
Hakuna tena hukumu
Hakuna pia woga kwetu !
Mungu alitusamehe.
Yesu wewe ni haki yetu,
Wasema : “naja upesi”
Kanisa lote lifurahi,
Kukuona Mukombozi !
Tuimbe bila mwisho
Uwema wa Bwana :
Furaha takatifu
Ijae moyoni!
Wokovu milele
Ulitoka mbingu :
Tuna Mukombozi. (bis)
Uheri wa damani !
Upendo mukubwa !
Mungu asamehe muovu
Aliyemukataa
Kwa kutupumzisha,
Kwa kutupa amani,
Yesu alijitoa. (bis)
Kwa kiti cha neema
Tukiinua macho
Tutauona uso
Wa Mwokozi mwema.
Kwetu hadi mwisho
Anatuombea,
Yesu ni mushindi. (bis)
Kuiongoza njia
Ya wakombolewa,
Mioyoni mwao atuma
Mwanga wake wa juu
Roho atuongoza,
Neema yatufunza
Kweli takatifu. (bis)
Ndugu sote tusimame
Tuna Mwalimu hapa
Bwana arusi yu aja
Kristo ataonekana. (bis)
Karibu atatawala
Pamoja na kanisa
Punde atalivika taji
La sifa ya ahadi. (bis)
Usiogope kundi ndogo
Wewe mpendwa wa Baba
Msalaba wa Mwana Kondoo
Uwe bendera yako. (bis)
Dunia ikikuchukia
Chuki yake ni kuzo,
Pendo, tumaini, imani
Vitakupa ushindi. (bis)
Sifa kwa Yesu Mwokozi
Tunamutumainia
Heri anayemuabudu
Ndani ya moyo wake. (bis)
Tunainua, ee Baba mpenzi
Kwako mioyo yetu na mikono
Na maombi twakutolea
Pendoni safi na ukweli
Kama waabudu wa kweli.
Mbele yako twajisikia
Kama tumepewa Mwana wako
Wana wa neema yako ya mbingu
Tuna fasi rohoni mwako
Kama Yesu na rafiki.
Tumependwa jinsi tulivyo
Unyonge watusumbuwa sisi,
Na kuita mapendo yako.
kwa Roho tuliyeahidiwa,
Uzaifuni twabariki.
Tukipiga hivi mwendo huu,
Twaelekea kwako, Ee Yesu,
Ndani yako hazina yetu,
Maji ya chem.chemu ya mbinguni
Na mkate wa wateule.
Tangu asubui, mioyo yakubariki.
Mchana na usiku, tu mkononi mwako
kwa wana wako, wema wako haukomi
Tena watupenda bila hata kuchoka.
Tunaomba kwako neema ya ajabu:
Utulishe leo na mkate wa mbingu;
Tunajingojea kwa musaada wako;
Daima watufunika na mkono wako.
Roho wako Mungu atufundishe njia,
Kwa neno lako takatifu mioyoni!
Tukitiwa nguvu naye hakuna woga,
Na tupo washindi pamoja na Kristo.
Tupo wasafiri, wageni duniani,
Moyo wetu unahaja ya mbinguni.
Ni mbinguni mwako, Mungu na baba wetu
Tutakapoingia kwa pendo lako.
Utuchunge katika safari salama,
Hadi siku ya heri bila magumu,
Tutaonja pamoja uheri muzuri,
Wakati Yesu atakapo tupumuzisha.
Sifaidiki wala kupoteza
Jangwani humu sina chaguo :
Hakuna pori hata jani bichi,
Hakuna maji yakuninywesha.
Jangwani hakuna kimbilio,
Wala pumziko hata kidogo,
Kwa nini mimi nisimame bure
Ninapokaribia kufika?
Jangwani mimi ninajua njia :
Njia ya pendo, neema na imani,
Nitakayoifwata bila shaka,
Kwani Mwokozi aliipasua.
Njia ya nguvu ijaayo heri,
Ambamo yote ni salama tu ;
Iniongozayo toka duniani,
Ilinifike kwa Baba Mungu.
Bila tamaa, bila kazi na woga,
Umenifundisha kukaa pale,
Nitaonja, pale patakatifu
Pumziko karibu nawedaima.
Muchungaji, kwa gongo lako
Pendoni mwako twakaa ;
Unatutunza tuna vyote,
Watuita kondoo zako.
Bwana wangu, kama dunia
Inatawanya wapendwa…
Mkono wako muaminifu
Ulituumba mumoja.
Tupendane kwa pendo kweli ;
Kando yake tuwe mmoja
Roho, Mwana na Baba pia,
Kwa imani ni ushirika.
Kwa miguu kama Maria,
Kuacha saa zipite
Kwa kimya tukijisahau,
Yesu tukuache useme.
Kwa miguu katika taabu,
Ninapata, kwa mateso,
Pendo na musaada wako,
Unanifuta machozi.
Kwa miguu, kwa sifa zako,
Tumwange, Mwokozi Yesu,
Manukato yasiyo changwa
Ya chupa iliyovunjika.
Ibada ya wakupendao,
Marashi ya juu mbinguni,
Yaliyochungwa kwa saa kubwa
Ya toleo lililotosha.
Nibaki kwa miguu yako,
Hapa chini sauti yangu
Iiname kwa wimbo mbinguni,
Mwana wa Mungu aliyekufa !
Tuimbe, tuimbe katika wimbo safi
Pendo la Mwokozi
Neema yake amini
Siku zote ni mpya
Inaangaa sana
{Yeye mkubwa na muzuri
Tumsifu Bwana. (bis)}
Tuimbe, tuimbe katika wimbo safi
Pendo la Mwokozi
Kiti cha neema
Fasi ya hakika
Kwa mioyo yetu
{Yeye mkubwa na muzuri} etc.
Tuimbe, tuimbe katika wimbo safi
Pendo la Mwokozi
Yesu utukufuni
Ni ushindi wetu
Na heri yetu
{Yeye mkubwa na muzuri} etc.
Sifa, uwezo na nguvu
Heshima kwake Mungu
Upendo na shukurani
Kwake Yesu Mwokozi.
Mwokozi ulivikwa miiba
Damu yako’kamwangwa
Hata gazabu ya Mungu
Na Ikakulemea.
Kwako ee Yesu mateso
Kilio, kifo, kuachwa
Na kwa sisi ukombozi
Wokovu, usamehe.
Sifa, uwezo na nguvu
Heshima kwake Mungu
Upendo na shukurani
Kwake Yesu Mwokozi.
Wakristo tulichaguliwa
Kuishi huko mbinguni
Mbele ya muumbaji wetu
Tuimbe nyimbo za furaha
Tulisitahili gazabu
Na tulikufa zambini
Katika hali yetu mbaya
Yesu alituokowa.
Tumeokolewa na Yesu
Kwa kufa na kufufuka
Tukapate Roho wake
Zawadi ya pendo lake.
Ndani ya Yesu tuna Baba
Nasi tu watoto wake
Kwa neema yake kila siku
Twapata matunzo mema.
Pendo lake halina mwisho
Hakuna cha kututenga
Hata mbinguni na duniani
Anatupenda daima.
Kristo ametupa uriti
Wa mbingu kwa damu yake
Ni fungo nzuri ya furaha
Karibu naye milele.
Twakusifu kwa tumaini
Baba harikisha siku
Mwana mupendwa kwa uwezo
Atakapo tutwaa kwake.
Kazi imekwisha kwa Mwamba wa Yakobo
Alilolisema, atalitimiza.
Bwana atatushika mkono ! (bis)
Kwa kuwa ni Mungu, (bis)
Kwa kuwa ni Mungu makimbilio yetu.
Bwana anatupenda milele na milele :
Neema yake kwetu haina mupaka ;
Kwa lengo atatufikisha, (bis)
Ndiye tumaini, (bis)
Ndiye tumaini ndiye uheri wetu.
Maadui wetu anawajua wote
Atupigania na atatufungua ;
Atashindana kwa nguvu (bis)
Na waovu wote, (bis)
Na waovu wote watamukimbia Bwana.
Miili ya kufa itapata ushindi
Twajua karibu ataigeuza
Baragumu iliapo (bis)
Kwetu waamini, (bis)
Kwetu waamini tutaona sifa tu.
Tutukuze Mungu, aliye Baba wetu!
Bwana akiwa kwetu: tutashinda yote.
Hatutatengwa na yeye (bis)
Tushinde kwa Yesu, (bis)
Tushinde kwa Yesu tuishi kumupendeza.
Sikugani tutapata uheri
Wakukusanyika nawe daima
Na kukuona Mwokozi muabudiwa
Pahali pa amani milele.
Muda mfupi ututengao nawe
Watuongezeya tumaini
Saa zapita na asubui yaja
Karibu Bwana utatoka juu.
Miaka elfu kwako ni kama wazo
Kwetu sisi usikuwapita
Bwanani siku gani utakwisha ?
Siku gani nyota itaangaza.
Kwa kukesha, vita, mchoko, uzaifu
Tunangoja kuinuliwa naye
Sababu mioyonimwetu nyota hii
Yatuangazia nuru njema.
kungojea kutukuzwa milele
Kwatupa hamu yakukuona
Moyo wetu wakutaka ee Yesu
Leta jibu la tumaini hii.
Ee Bwana uliyejitoa msalabani,
Utujaze bidii tukutumikie
Kwa mali, mwili na roho
Tupe kutembea hata tupo wanyonge,
Tukikutazama, na kwa wewe mwenyewe,
Tuwe sote na ushindi.
Utupe kuonja namuna ni kutamu,
Kwa kila mutoto wa Mungu apumzikaye,
Kupenda na kutumika !
“Kwangu kuishi ni Kristo” : Huu uwe musimamo
Wa wakristo wote, kila moja aseme,
Na wote wafanye hivyo.
Kwa furaha na tumaini,
Nakuona Mwokozi wangu.
Najua pendo lako kubwa,
Laokoa mwenye zambi ;
Nakutumainia eeBwana
Wewe ndiwe heri yangu.
Ni mbinguni, kwa mwendo wangu,
Nitarajiapo mimi
Chemchemu hai yake Roho
Yaninywesha nichokapo
Hatarini, hazina yangu
Ni nguvu ya mkono wako.
Mchana, chini ya nuru yako ;
Usiku kifuani mwako,
Asubui waniangazia
Nakuniongoza njiani
Na kila mangaribi Baba,
Waandaa kesho yangu.
Mwisho wa safari yangu hii
Nauona ni karibu
Ninangoja kwa uhakika,
Uriti ulio mbinguni :
Hata nikiwa kaburini,
Nitafufuka kwa shangwe.
Juu ya kanisa lako lote,
Ulipendalo saa zote
Bwana katika neema yako,
Unalimimia zawadi
Waamini, kwa tumaini,
Wapiga magoti pote ;
Utatujaza tumaini :
Bwana utakuwa nasi.
Ee Bwana Yesu wakumbuka
Ahadi za Neno lako ;
Roho wako anafariji,
Na kuongoza wana wako,
Tutembeze nuruni mwako
Chunga moyo wetu kwako
Kanisa lako likiomba
Lifurahi ndani yako.
Mungu Baba, wewe ulinipenda
Wewe Bwana Yesu
Ulinipenda kuzidia mama
Apendavyo mtoto. (bis)
Nikupende, ee Mungu wa mapendo,
Ndiwe ulianza
Nikupende, unipatiaye nguvu,
Nguvu, mwamba wangu. (bis)
Chemchemu ya neema, ulinipenda,
Mwanzo wa wokovu
Ulinigeukia ! Kanipenda
Utanifikisha. (bis)
Nikupende : kamwe akupendaye
Hatabaki pekee
Ni kwa pendo lako ulinipenda
Langu litaishi. (bis)
Kwako uliye tufundisha
Neno lililo la kweli
Wewe ulitufahamisha
Pendo lako lidumulo,
kwako uwezeshaye mutu
Kuwa mtakatifu kweli
Katika nuru kubwa sana
Upendapo wako wawe,
Kwako wewe, kwa neema yako
Ulitutosha kwa muovu,
Ulituokoa na uwezo
Wa giza pia mauti,
Kwako Mungu na Baba wetu,
Uliyetubeba vema
Kati ufalme, hekaluni
Mwa Yesu, Mwana wa pendo,
Kwako utukufu, hekima,
Mungu wa pendo na kweli,
Kwako nguvu na utajiri
Katika milele yote !
Kwako, Bwana, mwenye ushindi
Uliotupa uheri,
Kwako, Yesu, tunakusifu ;
Tunakuabudu, Mwokozi.
Kondoo za Yesu, ziko pendoni mwako,
Zinamutambua na kufwata sauti ;
Aziongozaye azipa mazuri ;
Aliweka pendo lake ndani mwao.
Hawapungukiwi kitu zizini mwake ;
Kando ya mchungaji, hawaogopi kitu.
Alinda kondoo, kifuani mwake ;
Jicho lake nzuri lawafurahisha.
Duniani tufani
Ikiunguruma
Inanishituwa :
Nakuogopesha
Mimi sitaogopa :
Yesu yuko nami,
Hata uwepo wake
Wafukuza woga.
Na nikiona giza
Maishani mwangu
Unaitawanya,
Ee Mwokozi mwema !
Juu ya wingu lote
Hakika nakuona :
Unanitia moyo,
Wanijaza heri.
Na nishindwapo mimi
Katika hatari,
Nipo mkononi mwako
Muchungaji mwema
Kwa pendo lako njema
Mimi sitatengwa
Nafichama bawani,
Sitashituliwa.
Kikombe kinajaa :
Najua pendo lako,
Na neema yako nzuri
Itanifuata
Kati safari yangu,
Mimi mgeni hapa,
Wewe, uriti wangu
Haubadiliki.
Chemchemu nzima,
Wokovu wetu,
Damu ya Kristo ilimwangwa.
Kuteswa kwake,
Kujitolea,
Ndiyo wokovu wa muovu.
Furaha kubwa !
Kristo ni njia
Ifikishayo kwa lengo.
Yesu asamehe ;
Hakuna mutu
Asiyemupa wokovu.
Uheri ni kwako, Mwokozi wa mapendo.
Ulitufundisha wimbo wakufurahi ;
Na kwa wema wako, tunaishi sisi,
Na wataka milele kutubariki.
Tumepata sisi muchoko duniani,
Tulipokuwa watoto wa kasirani ;
Tulipokimbia neema yako Yesu.
Tulipotea zaidi duniani.
Ukaonekana, kavunja minyororo ;
Pendo lako kubwa likatosha hukumu.
Kwa imani neema ikatufunza
Yakwamba tuna salama naye Roho.
Mapendo makubwa yatuambia kwamba,
Sisi tuna deni yakukusifu wewe,
Ongoza mioyo ili itazame
Mbinguni utuwekeapo hazina.
Bwana anatuita :
Tumuendee !
Ni mwema, mwaminifu,
Tegemeo ;
Wokovu atoao,
Hautanyanganywa.
Pamoja na huruma,
Abariki.
Pendo lake ni kubwa :
Mukombozi
Kajitoa mwenyewe
Kwa muovu.
Pale musalabani
Alipenda kufa ;
Mutegemee nafsi,
Abariki.
Wokovu, salama !
Habari ya furaha
Kwa watu waovu !
Yatuponya mioyo
Na kidonda kichungu,
Yatuliza woga. (bis)
Wokovu, msamaha !
Tuimbe maneno haya
Popote duniani !
Tuungane pote
Na waamini wote
Kukuimbia Bwana ! (bis)
Wokovu, salama
Yesu, mateso yako
Yalileta heri ;
Tunakushukuru
Ewe mwenye huruma
Ee Mungu Mwokozi. (bis)
Sifa kwa Kondoo !
Heshima na uwezo
Kwa mwenye mateso
Aliyetufia
Juu ya musalaba !
Twakuabudu, Bwana ! (bis)
Bwana Ulinipenda, mbele nuru iwe
Juu ya dunia uliyoiumba
Vile nyota ya mwanga kutembea muchana
Na kutoa uzima juu ya dunia yote
Mungu ulinipenda. (bis)
Mungu ulinipenda, wakati msalabani
Yesu ‘kaonekana akijiachilia
Kwa kuniokoa toka moto wa milele
Mwana wako alichukua zambi zangu zote
Mungu alinipenda. (bis)
Tanipenda milele!Shetani na dunia
Hawatazuia Kamwe hili pendo.
Kwa uwingi wa zambi, neema ikawa nyingi
Pendo langu lijibu kwa pendo lako Mungu.
Wewe wanipenda. (bis)
Sifa yako Mungu, yaangaa katika Neno
Kwa watoto wako, hazina damani ;
Ni sauti ya rafiki, na tegemeo ;
Ni barua ya pendo kutoka mbingu.
Tunaposoma, nafsi yashibishwa daima
Mioyo imepumzishwa na mizigo
Ndiyo chemchemu inayotoa uzima,
Muto wa neema kwa maji ya wokovu.
Ninyi musumbukao duniani humu,
Ninyi ambao mioyo yachoka kweli,
Muje wote na mupate hapa salama
Kutoka katika injili na pendo.
Sikieni wote habari njema ;
Yesu akafa kwa kutuokoa !
Anaemwamini ana uzima :
Wokovu ni zawadi ya Mungu. (bis)
Wenye zambi, katika taabu yenu,
Mukishindwa kutazama Mungu,
Njooni kwa Kristo anaonyesha Baba,
Kwa upendo a katoka mbinguni. (bis)
Ee, pokeeni neno hili nzuri
Roho anaambiya moyo wako.
Ni Yesu peke mponya na mfariji :
Njooni wote kwa mwokozi wetu. (bis)
Kwa nia moja, wapendwa wako
Waimba sifa, pendo lako kubwa
Mashauri yako yote ni nguvu imara
Na nia zako hazitageuka.
Siku yaja, Ee Mungu wa kweli
Dunia, mbingu zitakapokimbia
Ila watakatifu wako wa neema
Watasimama imaramilele.
Siku yaja ! Kuja Bwana Yesu
Kuja kuishi wokovu kuzoni
Namauti yamezwe na ushindi
Kusanya wateule juu mbinguni.
Mwana mpendwa ufurahishaye
Upendotele wa Baba yako
Ukawa mtu na kwa kujitoa
Tumejua upendo wa Mungu.
Chanzo cha mwangaza wa milele
Jua la Mungu liangazalo
Kwa mwangaza wako tunazaliwa
Giza ya mioyo yetu yatoka.
Ukusanyaye waovu wote
Mwana wa watu ukatundikwa
Damu yakoni kisima daima
Chaosha milele aaminiye.
Chanzo cha sifa na utukufu
Mwana Kondoo unayeangaa
Dunia yote yakuhimidi
Taifa lako lakuabudu.
Kukuona uso kwa uso,
Na Kusikia pia
Sauti iliyotutunza,
Na inayotuongoza ;
Kukufuata pamoja,
Tukivaa nguo safi,
Iliyo kama teluji
Ingaayo kwa jua ;
karibu, hakuna giza !
Karibu nawe, Bibi
Ataonyesha uwezo,
Neema pia uzuri.
Ni tunda la pendo lako !
Watu watamuona,
Amezungukwa mwenyewe
Na pendo la milele.
Bila kuelewa pendo,
Tunapiga magoti,
Kwani musalaba wako
Ulilishusha kwetu.
Utimilifu wa Bwana
Kwa muhuri wa Roho,
Kwa raha na uhakika
Watunywesha, twashiba,
Siku isiyo na wingu,
Tuitarajiayo,
Wakati tutakutana
Kukupenda ee Yesu !
Utakapokuja, Yesu, kwa nguvu
Walalao watafufuliwa,
Kwa muda mchache watanyakuliwa,
Mbele ya Baba watafikishwa.
Sisi tulio hai duniani,
Hazina ifichwayo uliyopenda,
Usiku tukikesha na kuomba,
Tunakungoja kama mwokozi.
Kujuta, kulia na kuteseka,
Havipo pale juu mbinguni :
Panajaa uepo wako, Yesu ;
Vyote ni salama na pumziko.
Pale ndani ya nyumba yake Baba
Kuna taifa la waabudu,
Kando yako kuliko duniani
Tukiwa wafalme, makuhani.
Ukuu wa upendo wa ajabu,
Uangazao neema na kweli !
Ulitembelea mutu mutumwa,
Duniani alikataliwa.
Ukaacha kuangaa kwa milele,
Ukashuka tumboni mwa kifo,
Msalabani, ee Bwana wa uzima,
Ukapigwa juu ya zambi zetu.
Tujipe moyo, tuinue vichwa ;
Ndugu, Bwana, Arusi atakuja !
Atualika kwa karamu milele :
Na tutapumzika pendoni !
Jina nzuri liangazalo,
Duniani mujaamo giza,
Katika kuangaza kwake,
Mungu asiyeonekana !
Jina
Na mwenye huruma kwetu,
Achukuaye, mtumwa mtashi,
Mzigo wa mateso yetu ;
Jina kubwa lenye uwezo
Jibu la imani yetu ;
Likusanyalo wateule,
Kando yako duniani ;
Jina ambalo, Mungu Baba
Ataweka juu ya vyote ;
Mbele yake, mbingu, kuzimu,
Dunia vitainama.
Jina mupya, sehemu kubwa
Ya wateule washindi,
Jina kanisa litabeba,
Milele mbinguni mupya ;
Jina la Yesu bila mpaka,
La Mungu mwenye uwezo,
Na la Mwana, Kondoo mwokozi,
Na mtu aliyefufuka ;
Jina la nyota ya asubui,
Jina la nyota ya mchana,
Sifa kwako, Jina la nuru,
Na pendo, libarikiwe !
Uliyetufundisha wimbo wa furaha
Mioyo yetu yajibu kwa wito wako
Tusisahau kamwe unyonge wetu sisi
Ili tutangaze vema upendo wako
Na kusifu wema wako udumuo
Tulikuwa mbali nawe, tukiteseka,
Tulikuwa gizani, bila msaada,
Punde kwa macho yetu tuliiona nuru ;
Yesu akatufunulia Jina la Baba
Na wema wako unaodumu daima ;
Ee Mungu Mwokozi, ambaye neema yako
Haikujizuiza kutusaidia,
Shauri zako nzuri, kwa njia nzuri pia,
Tutakutukuza kwa wimbo wa milele,
Na tutausifu wema wako daima !
Kwenye kiti cha enzi cha Mungu Mkuu,
Roho zangoja utukufu,
Wakifurahia pia,
Ushindi wa Mwokozi wao.
Kutoka kwa kundi lake,
Alilopendelea sana,
Wimbo waanza hapa chini :
Usifiwe, usifiwe.
Tukiwa mwili mumoja,
Tusifu mfalme wa uzima
Aliyefufuka mbele;
Ile wakati wa taabu
Mzigo wa mabaya yetu
Ukalemewa Mtakatifu
Wakati uliachwa na Mungu :
Usifiwe, usifiwe.
Yeye ni Kuhani Mkuu
Akaaya katika nuru,
Na Mwokozi wetu pia,
Anatutetea kwa Baba.
Ametuweka muhuri,
Tunaye Roho wa uzima
Kwa yeye Kanisa lasema :
Usifiwe, usifiwe.
Upesi kwa Bwana Arusi
Kwa ahadi ya kuaminiwa,
Aja na kutupeleka.
Tutakuwa naye milele,
Tukiimba wimbo mpya
Katika urizi mbinguni.
Ndipo tutasema daima :
Usifiwe, usifiwe.
Pendo lako latukusanya
Sisi ni wapendwa wako
Kwa Roho twakuja pamoja
Kukuabudu Mwokozi !
Uepo wako ni mema kuu
Pendo lako linadumu,
Unawapa uwapendao
Pumziko, heri, salama.
Moyo wetu wakutukuza
Sauti zetu, siku hii,
Zinatangaza kazi yako,
Sifa na kurudi kwako.
Ua za utukufu zimefunguliwa
Kwenye wateule, wakiinuwa ushindi,
Pamoja na Yesu Bwana na Mfalme !
Mbingu yapaza sauti ya furaha
Usiku umekwisha ; kilio na huzuni
Imetoweka, hapatakuwa kifo !
Sauti itawaita kutoka mbinguni,
Kwa furaha kubwa, mabikira wapita,
Na taa mkononi pamoja na Bwana wao ;
Na sababu walikuwa waaminifu,
Awafungulie makao ya milele,
Na kuingizwa karamuni daima.
Anakuja toka utukufuni,
Kristo, aliyekufa mutini :
Na watakatifu wamshangilia,
Waliosikia sauti yake, –
Aleluya ! Aleluya ! –
Wataandamania Mfalme.
Mubarikiwa wa tumaini,
Akingaa anatoka mbingu.
Wapendwa wake waliosumbuka,
Watafurahi pamoja naye.
Aleluya ! Aleluya !
Mwana wa Mungu aonekana.
Mumuone kuzoni ana alama
Za mateso aliyopata.
Akizungukwa milele na sifa,
Wakombolewa watamuabudu.
Aleluya ! Aleluya !
Aja, Bwana, Arusi, Kondoo !
Bibi arusi anakuita, Bwana ;
Yeye na Roho wasema : Kuja !
Kuja tukuone utukufuni,
Na uangae, ndani ya wako !
Aleluya ! Aleluya !
Ndiyo, Bwana ! – Watujibu : « Naja ».
Yesu, Mwana mpendwa wa Baba,
Ulishuka hadi kwetu,
Kwa watoto wote wa nuru
Jina lako nilikubwa !
Hakuna aliye kama, Yesu,
Wewe pekee ndiwe kweli ;
Yote ndani yako ni pendo,
Ukubwa, uzuri pia,
Tangu hapa chini kwa moyo,
Mwaminifu tuishi kwako,
Kwa bidii twakutolea,
Kuzo ya imani yetu !
Watumwa wa zambi, tuliishi duniani
Tulipotea bila tumaini
Ukatutazama katika giza kubwa
Kwa kutusaidia ukatoka juu.
Ukashuka hadi kwa msalaba wa haya.
Ulipopatwa na gazabu ya Mungu
Kuachwa na kifo vikapita juu yako
Na ukapigwa na hukumu ya Mungu.
Tumeokolewa kwa neema ya ajabu
Tukipendwa nawe twaenda mbinguni
Tuna usalama na kazi yako pia
Ilituletea njia ya pumziko.
Kwa wimbo wa pendo na wa shukrani pia
Nafsi zetuzainuka kwako Bwana
Tunangoja siku ya kuokolewa kwetu
Inayoangaa kwa macho ya imani.
Yesu akatoka mbinguni,
Akaja, Akaja,
Na akajitoa mwenyewe,
Kwa kifo, Kwa kifo,
Kwa sifa akapanda mbinguni
Kwa Baba, Kwa Baba.
Ukaapo kwa kiti cha enzi
Nakuona, (bis)
Mwana uliyelaumiwa
Kwa muti, (bis)
Baba akakufanya kuwa
Mufalme. (bis)
Kwa sasa tutakuona
Kwa macho, (bis)
Twataka, ee Mwokozi wetu
Mtukufu, (bis)
Tukutumikiye kwa pendo
Zaidi, (bis)
Nyayo zetu zionekane
Duniani (bis)
Tukikufuata kwa amani
Duniani, (bis)
Majaribuni na furaha,
Na vita. (bis)
Mapambazuko ni karibu
Hakika, (bis)
Hewa yalilia mlimani
Na mbali, (bis)
Juu ya milima asubui ni
Karibu ! (bis)
E nuru kamilifu
Isiyo haribika
Watakatifu watakapofurahi
Uheri wa ajabu,
Uso muabudiwa
Utawaangazia kati salama ! (bis)
Kwa milele nuruni
Nyumbani mwake Baba!
Giza itatoweka mbele ya mchana
Mbali ya dunia
Nafsi yetu yote
Itaonja pumziko karibu naye. (bis)
Sifa kwako Mwokozi
Yesu na kwa kazi yako
Wachaguliwa wako
Kwa juhudi na salama
Wakusanyika hapa kutangaza upendo.
Kwa furaha ya roho
E sadaka ya kuchinjwa
Mwana Kondoo mshindi
Twakumbuka kifo chako
Pamoja tunaimba kazi ya ukombozi.
Kukuinua Mwana wa Baba
Wimbo wa mbingu na dunia
Utapanda patakatifu
Milele, Milele.
Uso wako ‘tatuangazia
Rohoni mwetu kwa neema
Wewe pekee utatawala
Milele, Milele.
Wako watapasha habari
Za kifo chako cha toleo
Za ushindi ulio hai
Milele, Milele.
Kanisa mshuhuda wa sifa
Litaimba neema yako
Kwako wewe mufalme wake
Milele, Milele.
Ee Yesu ! (bis)
Mungu mkuu wa mbinguni,
Wewe mwenye sifa tele,
Shina la utukufu,
Kanisa linakuabudu
Ulilojipatia
Kwa damu ! (bis)
Ee Yesu ! (bis)
Utuongoze Bwana.
Unavyotaka ni vyema
Na si muzigo kwetu ;
Upendo washinda woga
Milele. (bis)
Bwana, yawezekana mtu wa mavumbi,
Mwenye zambi kama mimi,
Awe mwana wako na kukuita Baba,
Atiwe karibu yako ?
Ndiyo, kwa mipango ya pendo lako kubwa,
Ulipenda kutuokoa
Ukamwacha Mwana hukumuni
Akipigwa hata kifo.
Mpendwa wako Yesu akufurahishaye,
Ajuaye mambo yako,
Akajitoa mwenyewe kuwa sadaka
Atuokoe wenye zambi.
Kizuri gani cha kuona kwa milele
Isipokuwa msalaba
Wa Mfalme wa uzima wakati wa giza
Mungu akihukumu zambi.
Malaika wanashangaa wakitazama
Na kusema kwa magoti
Kwa hofu takatifu fumbo la ajabu
La kujishusha kabisa.
Nasi tuliyookoka, jamaa teule
Ulitakalo karibu,
Hatutaweza kabisa kusifu pendo
Matunda ya kazi yako !
Bwana ukagunja kichwa
Ukabeba mzigo
Kwa kunilipia deni
Ukajitolea
Mimi si lemewe tena, Sina mzigo tena ! (bis)
Na kikombe cha hasira
Kilikufurikia
Ulikinywa hadi mwisho
Kipo wazi kwangu
Teso lako, lalamiko ni wokovu wangu ! (bis)
Kwa kufa, ukaniponya
Nilikufa nawe
Mshindi, ukanifungua
Ninaishi kwako
Kuja kwako mawinguni ni sifa na wewe ! (bis)
Nyota iangazayo
Gizani mwangu
Fimbo kiongozi
Mkate chakula
Kisima cha maji
Taa nionayo
Pale ngambo nzuri
Yote ni wewe.
Hakuna mwengine
Kama wee Yesu
Nionapo shida
Wanifariji
Tumaini njema
Msaada wangu
Salama, uhakika
Vyatoka kwako.
Utakapokuja
Nitasikia
Mwito wa sauti
Iniitayo juu
Ninaleta nini ?
Hakuna adui
Wafungua mlango
Wanipa vyote.
Mbingu ilitembelea dunia
Emanueli amekuja
Mungu alijifanya mutu
Kanisa limuabudu.
Pendo lipitalo fahamu
Mwana wa Mungu, muumba
Alitujia, wenye zambi
Kama vile mtumishi.
Pendo kubwa, linyenyekevu
Lilishuka chini sana
Mwana wa mutu kajitoa
Kufilia dunia hii.
Manukato isiyochangwa
Wako watakutolea
Marasi ya kusifu kwetu
Ni Yesu pendo lako.
Mbingu ilitembelea dunia
Emanueli amekuja
Mungu : mutu, fumbo ya ajabu
Kanisa limuabudu.
Kwa unyenyekevu mkubwa
Twakufwata zikini
Yesu ulizarauliwa
Ukiwa msaidizi
Pendo lako ni msaada
Na huruma, kamili
Juu ya watu wabaya
Likamwanga mema tu.
Roho yako ya mapendo
Yafungua hazina
Mungu mwenyewe atambua
Humo utakatifu
Nasi tukijazwa neema
Tu watoto wa Mungu
Tunaweza kukufuata
Njiani kwa upendo
Hayani na uchunguni
Sikitikoni pia
Mwili wetu uuguwapo
Mfano wako Mwokozi
Utatupatia moyo
Hata tu wazaifu
Kukufuata kikamili
Katika uutu wako.
Muda kitambo tutakaa
Karamuni mbinguni
Wako watakapo kuona
Mwana Kondoo wa Mungu
Tukivaa utukufu
Tukiwa kuume kwako
Yesu tukikufanana
Kweli tutashibishwa.
Ee Mwokozi mwema.
Kanisa leo
Linakutamani.
Uje upesi !
Nyota ya mbinguni,
Moyoni mwetu,
Utukufu wako,
Usifiwe !
Tukiwa mbinguni,
Tutapendezwa
Na zawabu yetu !
Njoo Bwana Yesu !
Na kanisa lako
Kwa siku ile
Litapokelewa
Huko mbinguni !
Twaimba mapendo mazuri yake Yesu
Inatosha kwetu, hii hazina nzuri,
Tuu ya ulimwengu unaojaa nuru,
Yanaonekana, mapya kila siku.
Pendo hili nzuri, linapita kuzimu,
Na linapanda juu kuliko mbingu.
Tangu umilele, mbele dunia kuumbwa,
Bwana, ka Tupenda ! Tunakubariki !
Mahali pa heri, ukijaa na sifa,
Wewe wa milele umevikwa kungaa,
Muumba muweza, upewaye ibada,
Pekee ulishuka kati ya waovu,
Ili u Tulete nyumbani mwake Baba,
Ukiacha haki zako na kuonewa.
Muchungaji mwema, kaona taabu yetu,
Uka Tutafuta ! Tunakubariki.
Ulifwata njia yako pekee yako,
Ukitoa hazina za wema wako,
Ukitoa neema : Hiyo ni siri kubwa !
Kwa upofu wake, mutu alikukataa :
Kazarauliwa bila kuficha uso
Kwa lengo hilo kuu la mapendo yako,
Hakuna chakuzuia kazi ya neema yako ;
Bwana, ka Tupata ! Tunakubariki.
Saa ilifika ! Siku hiyo ya giza
Katika njia ngumu, kabeba msalaba,
Kichwa chako, Yesu, kilivalishwa miiba,
Na uka Tukanwa pia kulaumiwa !
Uliachwa kwetu kwa muti wa Kalvari,
Kapata uchungu, azabu juu yetu.
Uliazibiwa sana juu ya zambi ;
Uka Tuokoa ! Tunakubariki !
Twataka tuimbe maishani mwetu mwote
Pendo hili nzuri, lipitalo vyote !
Na tukigeuzwa kwa nguvu ya milele,
Tutaifikia siku ya uamsho,
Macho yetu sisi yatakuona kuzoni,
Ee Yesu, Mwokozi, uu Rafiki wetu,
Wako kwa miguu, wata Tupia taji,
Wakikuabudu ! Tunakubariki.
Yesu anapenda,
Yeye mwenyewe
Kutubeba.
Yesu aja,
{Matumaini
Ya waamini !} (bis)
Huko nyumbani
Mwa Baba yetu,
Tuingie
Na furaha
{Katika nuru
Ya mbinguni !} (bis)
Kazi imekwisha ;
Makao yapo.
Kifuani
Bwana arusi
{Tulaze sote
Vichwa vyetu !} (bis)
Na itulie,
Bila mwengine
Ila wewe,
Na kuweza,
{Nyuma ya vita
Kukuona !} (bis)
Wewe uliye,
Ee Bwana mtukufu,
Kwa hakika
U milele
{Ni kuelewa
Pendo lako !} (bis)
Usikie kanisa pendwa
Bwana aja
Taa zetu ziwe tayari
Bwana aja
Saa sita za usiku hizi
Hatujaona hata mutu
Aangazia mioyo yetu
Bwana aja.
Tunaisikia sauti
Ona Bwana
Hakuna giza na kukesha
Ona Bwana
Na sasa hivi baragumu
Yatualika kwa karamu
Asema : « kanisa tayari ? »
Ona Bwana.
Furaha ikasikika mbinguni
Wakati sauti ya muweza
Ilipo towa nuru.
Alipoumba mbingu kwa mkono
Akionyesha uwezo wake
Akaumba ulimwengu.
Furaha ikasikika mbinguni
Hapa chini, Yesu, Emanueli
Akazaliwa mnyonge!
Malaika waliimba sifa,
Salama duniani, sifa juu
Walijaa raha tele.
Furaha ikasikika mbinguni
Mwenye zambi asikiapo sauti
Ya Mwokozi akiita
Zambi zake zimeondolewa
Yesu amupa uzima, salama
Anamulinda kifuani.
Furaha gani na shangwe juu
Wakati waamini wa milele
Watakuja kuketi
Karibu na Yesu kwa furaha
Wataimba pendo lake njema
Na neema yake nzuri.
Chemchemu ya nuru, uzima
Ya neema kwa imani
Pumziko, uheri, salama
Tulipata ndani yako.
Chemchemu ya pendo iliyo mpya
Kutoka patakatifu
Watujaza chemchemu nzuri
Na uwepo wa milele.
Heri aliye karibu na mto
Amepandwa muti hai
Wanywa maji na unaota
Wakomaa kwa milele.
Wazaa matunda, wasitawi
Wapata nguvu kabisa
Heri yule, hapa duniani
Anywaye kwa chemchemu hii.
Chemchemu ya neema hai
Mwaminifu, muchungaji
Pendo lako halina mwisho
Wewe haubadiliki
Hata kama twajaribiwa
Na kushambuliwa pia
Unapatia nafsi zetu
Tumaini, imani, pendo.
Mwisho wa vyote ni karibu
Vizuri havisitawi
Umilele wakaribia
Majaribu ya dunia
Yatageuka kuwa mema
Ya pumziko ile kubwa
Imani pia tumaini
Vitakwisha, upendo la !
Ninaleta sifa nikitazama
Mbingu, hii kazi yako ya ajabu,
Mawingu, mwezi na nyota zote
Ulizoziweka kwa mustari.
Nasema mwenyewe nikishangaa :
Mtu ni kitu gani, ee Mfalme mkuu
Ili uweze kumukumbuka
Na neema yako kumuarifu ?
Akafanywa chini ya malaika
Wanaozitangaza sifa zako
Ukamvika utukufu pia
Hata kuzungukwa na heshima.
Umemupa kutawala viumbe
vilivyoumbwa kwa mkono wako.
Katika mipango yako, Bwana,
Vyote vitakuwa chini yake.
Eh kuja Bwana
Kwani dunia hii
Ijaamo zambi
Kwa roho yangu
Haitaleta
Pumziko, amani
Asubui yaja
Kuja kunitwaa
Ninakuhitaji
Pumziko langu.
Kondoo mwema
Nitakutazama
Ukingaa neema
Na usalama
Upendo wako
Paradizoni
Nyumba yake Baba
Atanimwangia
Nuru yake pole
Pumziko langu.
Pumziko njema
Kutoka pendoni
Utafurahisha
Hata milele
Heri ijayo
Kukubariki
Na kukufanana
Utanipa vyote
Mwokozi mupendwa
Pumziko langu.
Pendo la Mwokozi, kisima kishukacho
Kinanituliza, (bis)
Hakuna kiwezacho kufunga maji
Nitaonja daima uzuri wako Bwana
Pendo la Mwokozi. (bis)
Pendo la Mwokozi, watosha nafsi yangu
Pumziko, uheri, (bis)
Nina vyote kwako, naota moto wako
Nitavumilia jaribu na kemeo
Pendo la Mwokozi. (bis)
Pendo la Mwokozi, nitatazama wazi
Utukufu wako, (bis)
Nyumbani mwa Baba, kwa mwisho wa safari
Nitakutazama na kukuza milele
Pendo la Mwokozi. (bis)
Nyumbani mwa Baba, tutakuwa pamoja
Ee Yesu Mwokozi uliye jitoa
Niwe nawe Mungu wa upendo na nuru
Milele na wewe ! (bis)
Mjini mtakatifu sifa yako yaangaza
Wako wanakutazama kwa imani
Nitaonja tunda ya neema yako kubwa
Milele na wewe. (bis)
Ee Mwokozi, wewe uzima,
Na nilipokukimbia,
Sauti yako ikaniita
Kwa karamu ya Mufalme.
Na tangu sasa, mbele yako,
Umeniosha kwa damu,
Ninaonja neema nzuri
Ya Mungu Mwokozi wangu.
Kwa wakati huu wa magumu,
Kwa kunipatia nguvu
Na kuniongoza kwa ukingo,
Muchungaji wanitunza.
Mabaya yasongapo mbele,
Tukungojapo urudi,
Ninakubariki kwa pendo,
Matunzo ya pendo lako.
Punde, nyumbani mwake Baba,
Utatupokea sisi,
Ili tuone siri kubwa
Ya neema na pendo lako.
Na sasa malangoni mwako,
Pamoja na kundi lako,
Nitasifu katika nyimbo
Sifa zote za Kondoo !
Heri gani kukujua
Usiye badilika
Mwokozi, mwalimu wangu
Musaidia, mchungaji.
Sitapungukiwa kamwe
Wajibu mahitaji
Nalindwa na gongo lako
Ninajiacha kwako.
Katika bonde la giza
Unanikaribia
Nina farijika mimi
Kuwa karibu nawe !
Kwa pahali pa mbinguni
Nitaingia hapo
Ili nikuone nuruni
Mchungaji wa uwezo !
Heri gani kukujua
Usiyebadilika
Mwokozi, mwalimu wangu
Mchungaji wangu mwema !
Katika jangwa kubwa
Bila njia kamwe,
Anayeniongoza,
Naye alipita
Kwa Baba ananileta
Ni furaha yangu
Hakuna kitu hapa
Cha kunishawishi.
Ninamutegemea
Namfuata kwa bure,
Wala kwa kupoteza,
Akinifaidia ?
Vitu vya ulimwengu
Vyataka nifunga
Uwezo wake mkubwa
Wanitoa hapo.
Heri aliye huru,
Njiani mwa mbingu
Ninaungana sasa
Kwa wimbo milele
Uchungu na tatizo,
Havitetemeshi.
Jaribio linajaa
Matokeo mema.
Kwa njia ya saa moja
Ninapotembea,
Kama nanungunika
Nitakata tamaa ?
Sivyo, neema yake
Ndiyo kimbilio,
Gongo na fimbo yake
Vitanifariji.
Yesu chakula changu
Nilacho duniani,
Nikipiga hatua
Unanipa nguvu.
Kwakufanana nawe,
Nitakutazama
Katika utukufu
Na nitakusifu.
« Nakuja upesi : ngojeni kuja kwangu »
Asema Mkombozi aliyetupenda.
Aleluya ! Aleluya ! (bis)
Kuja, Bwana Yesu, (ter)
Juu ya wingu nyeupe.
Dunia na mwili, mpinzani wetu mkubwa,
Maadui wote, umetushindia ;
Aleluya ! Aleluya ! (bis)
Kuja, Bwana Yesu, (bis)
Tunayetumaini.
Hapa duniani tupo majaribuni,
Ila juu mbinguni hakuna tatizo
Aleluya ! Aleluya ! (bis)
Kuja, Bwana Yesu, (bis)
Kutwaa Kanisa lako.
Tumwendee nani ? dunia hii ni mbovu
Kao la shetani, jangwa danganyifu
Twataka kujenga nyumba zetu mchangani ?
Hapana, si hivyo uheri ujavyo.
Tumwendee nani kwa kupata ujuzi
Wa Mungu wa kweli, wa nuru na pendo ?
Nani atatoa salama, uhakika,
Tunapotembea na tukilemewa ?
Tumwendee nani ? chemchemu mpya daima
Inayotuliza kiu ya mioyo,
Neno lako, Bwana, uzima wa milele :
Tunalinywa tukikuabudu wewe.
Tumwendee nani ? Sauti yako tamu
inatuambia : Musiwe na hofu :
unatufariji, waondosha machozi
Tumwendee nani ?, wewe pekee tu.
Twavuka bahari mbio,
Tu wenyeji wa mbingu.
Mapambazuko yakuja
Mchana waonekana.
Mutazame : bado ngambo
Yaonekana mbali ;
Rafiki tujipe moyo
Pumziko ni hakika.
Tufani ikitutisha
Tusiogope hatari ;
Safarini tupo naye
Abiriya wa juu ;
Shimo saliti la wimbi,
Fasi ya kuzamisha,
Bwana anaikomesha ;
Na sasa tunavuka.
Ni furaha kubwa gani !
Tutakapomuona,
Na wakati pendo lake
litatuvika sisi !
Mutazame bado ngambo
Yaangaza asubui ;
Rafiki tujipe moyo,
Tumepata pumziko !
Moyo wangu watamani kuwa nawe daima
Nikipupa natamani wakati utarudi
Ninaimba na wako:
”Amina ! Bwana kuja !”
Wewe ni hazina yangu,
Ni wewe nihitajiye.
Ayala atakavyo kunywa
Sana maji ya mito,
Hivyo katika jangwa hii
Nakutamani wewe,
Ninaimba na wako:
« Amina ! Bwana kuja ! »
Itakuwa siku gani
Nitakapo kuona wewe ?
Kufurahia neema,
Kutukuza mapendo,
Kukuona uso kwa uso,
Kuwa nawe milele
Yanituma kusema:
« Amina, Bwana kuja ! »
Ujibu kwa ombi langu,
Kwani ninakuhitaji.
Ndugu, tujipe moyo !
Punde tutaona
asubui ingaayo :
Kwa pwani ya milele
Sisi tutafika. (bis)
Hapa chini zoruba,
Hapa chini ziki,
Hatuna pumuziko :
Fasi yakujikinga
Kwa mioyo yetu. (bis)
Kwa moyo mutiifu
Ni bandari nzuri ;
Ni pumuziko kimya,
Na Kimbilio kimya
Kwa nguvu ya Mungu. (bis)
Ndugu, tujipe moyo !
Punde tutaona
Asubui ingaayo :
Kwa pwani ya milele
Sisi tutafika. (bis)
Kwa moyo mkunjufu, kwa nafsi ichokayo
Yesu, kwa mapendo ni pumziko tamu,
Pumziko idumuyo neemani mwake
Iliyotutafuta na kutupumzisha.
Twapata pumziko tunapogunja vichwa,
Muabudiwa wetu, kwa nira ya pendo,
Twafundishwa nawe pia na neema yako,
Kubeba muzigo tukiuvumilia
Pumziko ya mbingu ! Tumeipata hapa
Tukifuata njia, inayoangaza,
Ituongozayo kwako katika nuru,
Kwenye pumuziko letu wakombolewa.
Nafsi usiogope wakati wa mateso
Bwana ni mwamba na nguvu yako pia
Inua macho juu : ni ukombozi wako
Hatakuacha kamwe : ee nafsi tulia.
Yanipasa vita, kujaribiwa pia
Kusafishwa kama zahabu chomboni,
Kupitia moto ama kuvuka mito,
Yu Mwokozi wangu, kiongozi, hazina.
Na sitaogopa shetani na dunia
Hawataninyanganya mchungaji wangu.
Hapo kwa amani naonja pendo kubwa ;
Ninalindwa toka hatari daima.
Inchini mwangu, kule kwako
Roho ananiongoza
Bila woga ninakufwata
Kila siku hadi mwisho
Anipa nguvu pia moyo
Kati njia ya mbinguni,
Punde kwa mwisho wa safari,
Nitakuona Emanueli.
Ila katika njia hii,
Fujo haitanizuru,
Kwa kimya nafsi yasikia
Sauti ya Roho wako.
Bwana utuongoze, fungua njia zetu,
Mungu wa salama,
Tuna karibu nawe chemchemu ya furaha,
Wakati wowote. (bis)
Tunapojikuta, tukikosa msaada,
Hatari ikija,
Tunakukimbilia pale ulipo wewe,
Bwana utuongoze. (bis)
Bwana utuongoze, tukiwa na ushindi
Tupumzike kwako,
Tuongozwe na wewe katika utukufu,
Kwa imani yetu. (bis)
Bwana ninapotazama
Kazi ulizofanya,
Mbingu ni hekalu lako
Lifunikalo watu.
Nionapo jeshi kubwa
Nyota za juu mbinguni,
Ushikazo kwa uwezo
Katika njia zao.
Mimi kweli ni mudogo
Si kitu mbele yako,
Najisikia munyonge,
Ee muumbaji muweza.
« Imekwisha. » ni kazi ya neema
Ushindi wapandisha sauti
Mwenye kufa akainamisha kichwa
Alishinda. Imekwisha.
Aliteswa. Yeye akajitoa
Mungu akamufurahia sana
Akakuzwa naye akamupa sifa
Mkamilifu. Imekwisha.
Mupotevu katika umaskini
Kaondoshwa zambini na Yesu.
Malipo makali akayatoa
Aliteswa. Imekwisha.
Kutoka juu Mungu akapasuwa
Ile pazia njia ikawekwa,
Mpya mupaka kwa makao mbinguni
Kwa milele. Imekwisha.
Mbingu mupya hata dunia mupya
Vyote vitaimba sasa kwa upendo.
Sifa kwa Mungu, na Mwana, na Baba !
Kwa milele. Imekwisha.
Sasa, sifa zako zafwata,
Uchungu uliyopata
Mbinguni kwa wakombolewa,
Waonekana Mtukufu. (bis)
Mwili wetu, hema legevu,
Twateseka, twalemewa
Twatarajia jengo letu
Tutakalo vaa kuzoni. (bis)
Kupitia chozi na teso
Twakusikia toka juu,
Julisho la heri ijayo,
Lisemalo : « Ninakuja ». (bis)
Kwa upendo na tumaini
Jibu la wachaguliwa
Lapanda kupitia Roho :
« Amen, kuja, Bwana Yesu ! » (bis)
Ulipohukumiwa,
Kati ya waovu,
Fimbo za haki yake
Zilikulemea.
Kosa lako ni gani ?
Kwa nini kupigwa ?
Kondoo takatifu,
Hukuwa na kosa.
Ulikuja kuokoa;
Watu wakakataa,
Na yote tumekuwa
Ilionekana.
Dunia ilikutesa,
Ikakuzarau,
Katika ziki kubwa,
Moyo kavunjika
Saa ilipofika
Ukaachwa pekee,
Mungu Mutakatifu
Akakuacha wewe.
Siri ishangazayo,
Wewe mpenzi wake,
Ukapata gazabu
Yake kali sana.
Mwokozi Muabudiwa,
Kafungwa mutini,
Ukafia waovu,
Kaondosha zambi,
Kavumilia teso
La makosa yetu ;
Katufungua sisi,
Katupa salama.
umemaliza kazi
Mungu ametosheka,
Umeivikwa taji,
Ushindi kamili.
Kwako sifa uwezo,
Heshima ukuu,
Hata mashukurani
Kwa milele yote.
Mwana wako, ee Baba wetu,
Juu mbinguni na duniani,
Yeye ni furaha yako,
Yesu akajitoa kwetu
Mupendwa wako kila siku,
Amepewa heshima kuu ;
Tunaona kwa uso wake
Kukingaa utukufu,
Uonyeshao neema yako,
Ufunuo wako wote.
Mbele ya dunia kuumbwa,
Uliweka kando, kwa neema,
Mwana Kondoo bila taka.
Alipata hukumu yetu,
Na hapo manukato bora
Yalipanda mbele yako !
Mupendwa wako, kajitoa,
Katimiza mpango wako ;
Msalabani, akamaliza
Kazi, akakutukuza.
Ametukuzwa hekaluni,
Kuume kwako, Baba wetu,
Ameketi na ushindi.
Punde 'tanyakua Kanisa
Alilinunua kwa bei
Talipeleka mbinguni.
Kando yake, kwa utukufu
Litangaa sifa zake
Na litaimba kwa ushindi
Katika milele yote.
Mungu, tunatangaza sifa,
Za aliye shuka hapa
Kuanza historia yetu,
Akikutii kwa yote. (bis)
Ni jambo lakukupendeza,
Mwana wako muabudiwa !
Ndani yake tunatazama
Sifa zako bila mwisho. (bis)
Alikuwa mwenye huruma,
Mnyenyekevu, msaidia ;
Alipokuwa akitembea
Alikuwa mkubwa
Katika kufa na kuishi,
Alikupendeza wewe,
Alipokuja, neema tele,
Kutumika na kukufa. (bis)
Alikataliwa duniani
Mutu alimsulubisha
Ingawa alikutukuza
Ulimutukuza vile. (bis)
Punde katika neema yako
Tutapata pumuziko,
Tutauona uso wake,
Nakumuabudu milele. (bis)
Kunakuja, Bwana, siku katika kuzo
Tutakapoonyeshwa mbele ya Baba ;
Na utafurahia tunda la ushindi,
Tutakapo kuzunguka. (bis)
Tukiwa kuzoni – Bibi arusi amevikwa –
Kwa karamu yako, utatuingiza,
Utatuketisha ulipotayarisha,
Utakuja kutulisha. (bis)
Malangoni pa juu, mwisho tungojeao,
Ambapo milele ulitaka watu,
Tutautazama uso wako muzuri,
Machapa mkononi mwako. (bis)
Tutakapoona utajiri wa neema,
Hazina ambayo isiyo na mwisho,
Sifa na muhuri wa ahadi za Mungu,
Yesu, utazifunua. (bis)
Asifiwe Mungu ! Na wewe Mwana wake,
Usifiwe Mwana wa watu, Kondoo !
Bwana, tupatie kuangaza duniani
Picha za patakatifu. (bis)
Siku ya huzuni, Mungu akakuacha !
Siku ya haya na mchanganyiko,
Ukalipa pahali petu, Bwana,
Bei ya ukombozi wetu.
Ulitafuta pendo, mapatano,
Ila wako hawakukujali
Walikuzihaki na kukukana
Haukupata hata mfariji.
Ulinyamanza katika mateso,
Wakati mbele yako maadui
Walipokuwa wakikutukana
Lawama ikakuchana moyo.
Ulipo kunywa kikombe kikali
Ulisema : « Yote imekwisha ».
Mushindaji ! Mikononi mwa Baba,
Kwa salama, ukatoa roho.
Mwokozi mwema, juu ya malaika,
Mungu, akitosheka, alikuinua,
Toka duniani, twaimba sifa,
Na kwa magoti tunakuabudu.
Twakuabudu, Bwana wa sifa,
Uliye tukuzwa juu ya mbingu.
Tunatangaza, Mungu mshindi
Jina tukufu daima,
Tunakutukuza, wewe pekee yako,
Sifa kwako juu mbinguni.
Mfalme, uvikwaye uwezo,
Utarudi ukiangaa,
Ulikuwa hapa, matesoni,
Ulikataliwa na watu !
Utukufu kwako
Kwa Wewe mwenyewe,
Sifa kwako kwa milele.
Ee Yesu, Bwana wa uzima,
Ulipigiliwa mtini,
Katika mateso makubwa,
Ulikufa musalabani !
Utukufu kwako
Milele yote,
Nyimbo na mioyo vipande.
Ukiangaa kwa nuru kubwa,
Utaonekana wazi,
Mbinguni hata duniani,
U Mufalme, Kristo Bwana.
Hivi nafsi zetu,
Zinakutangaza
Mwana wa Mungu, Mkombozi.
Barikiwa, Mwokozi mwema
Uliye tutembelea
Ukifunika utukufu
Hata kufanana mutu.
Wewe mubebaji wa mbegu
Ulizipanda kwa chozi,
Ukapata mateso, Yesu
Katika kujitolea.
Mbegu ya ngano udongoni,
Ikifa, iandikwavyo,
Haitabaki pekee yake
Ila itazaa matunda.
Mavuno sasa ni tayari
Mbele yako, mupandaji ;
Utarudi, ukiimba raha,
Ukiyashika masuke.
Utaonekana kwa sifa
Sisi Tukikuzunguka,
Sisi matunda ya ushindi,
Tukikusanywa milele.
Wana wa neema ya Mungu
Twaweza kuja kwa Baba,
Tukifurahi mbele yako,
Tukikutukuza wewe.
Kwa Yesu Kristo, tumaini
Ni vema tukuletee
Ushuru wa mashukurani
Tukuinuwe pamoja.
Ilitumeza milele,
ukatuangazia pia
Na tukapewa amani
Kazi ya neema imetimia,
Tunaona Mukombozi
Akivaa utukufu tele
Alipotutangulia.
Tunda la ushindi milele
Yesu ametuokoa
Twamuona utukufuni
Ambapo umempokea
Tukuabudupo hekaluni
Tuingiapo kwa imani,
Mungu Mweza, Baba wetu
Twainama mbele yako.
Punde, mbinguni, kwa vizazi,
Tukiimba wimbo mupya,
Wakombolewa wataabudu
Mbele ya Mwana Kondoo.
Wakifurahi mbele yake,
Na kushangalia Yesu,
Na Watatangaza uwezo
Nakusifu wema wake.
Twastaajabia ufunuo wa Baba,
Kwa Mipango ya Mungu Mwokozi,
Aliyefanya uumbaji mupya
Mpango wa moyoni
Mbele zambi iingiye duniani,
Kondoo alikuwa mbele yako,
Baba milele, hekima ya ajabu
Shauri la fumbo !
Yesu kajitolea kwa zabihu
Akaleta salama kwa damu ;
Apitiaye Kwake aona Mungu,
Kwake wampokea
Utukufu kwa Yesu malimbuko,
Aliyefufuka na ushindi !
Ameketi juu, ni furaha yako
Adamu wa mwisho.
Ulimwengu wote unateseka
Siku moja utakuwa huru ;
Kristo ndiye chanzo cha ukombozi
Toka ubatili.
Mungu ndani ya yote, tumaini !
Salama ya muji mtakatifu !
Utajaza wako na uepo wako,
Siku ya milele.
Tukikuabudu sasa duniani,
Mwana Kondoo mushindi atukuzwa,
Twakusifu, Mungu na Baba wetu,
Kwa zawadi yako.
Huru kwa furaha, watoto kwa Babao,
Kwa ushirika wako, wapendwa wako,
Waweza kuonja, katika nuru yako,
Utamu wa upatanishi wa neema.
Twafika mbinguni, umetukubaliya,
Pamoja sote twaja kukuabudu,
Tukikutolea shukurani kwa Yesu,
Sifa ambayo pendo lilitupatia.
Ulitaka wana pamoja naye Yesu:
Baba, ulituleta kwako milele
Na uzima wetu ni ndani ya mupendwa,
Yesu mbinguni, Mutu aliyefufuka.
Sote ndani yake, tunakuabudu wewe,
Tukitangulia siku ya milele,
Tutamufanana Kristo aliyetukuzwa,
Milele mbele yako katika heri.
Nani aweza kueleza,
Mateso ulivumilia
Kwa pendo vile utiifu,
Ukuongozao Golgota,
Na huzuni yako ya ajabu,
Ulipokuwa ukiomba,
Mwokozi kwa mateso yako,
vitani mwa Getsemane !
Kutangulia saa ile,
ulipata woga, taabu,
Ukiomba, ikiwezekana,
Kikombe kikupitiye.
« Ila mapenzi yako yawe ! »
Kukubali kwa ajabu
Kwa Mwokozi asiye zuizwa,
Yote kwake ni kamili !
Ulija kutukuza Baba,
Hadi kifo ukafika ;
Ndani yako alifurahi,
Mpendwa wake mnyenyekevu.
Twakutolea sifa, Bwana ;
Tukiona bidii yako ;
Tutakutukuza milele
Nakujitolea kwako.
Twainua, Mungu, Mwana wa pendo lako,
Ulimupenda milele na milele ;
Kwa kukutukuza, alijitoa yeye :
Ili ayatimize mapenzi yako.
Mwana wa milele, ni mukubwa zaidi,
Kama vile Mungu, alipewa vyote,
Ila akajishusha, na akanyenyekea,
Alikutukuza, hadi msalabani.
Mwana wa watu alihangikwa mutini,
Sadaka iliyopita katika moto,
Mupendwa wako akajitoa mwenyewe
Zabihu kamili, kwake Baba Mungu.
Ulitosheka na hii sadaka nzuri
Ya Mwana Kondoo, bila hata taka :
Kujitoa kwake, na utiifu wake,
Ni manukato ipandayo juu kwako.
Alipojitoa, sadaka takatifu,
Kristo alikuonyesha wewe vema,
Kwa Mungu wa haki anayeomba sifa,
Alilitukuza pendo lako nzuri.
Tumefufuliwa, tu wapendwa kwa yeye,
Baba, twazitukuza shauri zako.
Twafungwa na mpendwa kwa neema yako nzuri
Twakuabudu sasa pahali pa juu.
Kwa anayetupenda, na aliyeosha zambi zetu kwa damu, kwa damu tu ;
– na akatufanya tuwe ufalme, wa makuhani wa Mungu Baba ; –
Tumupe heshima, kwake pia nguvu, katika milele.
Amen ! Amen !
Tupatie Bwana
Utakatifu
Tuwashie moto,
Ututulize ;
Leta tumaini
Tuwe imara
Tukivumilia
Kila jaribu.
Tupe kutazama
Mwana Kondoo,
Mfano na msalaba,
Kaburi lake,
Neema aminifu,
Mapendo yake,
Utukufu wake,
Kurudi kwake.
Kwa machozi yetu
Watusaidia,
Watuvika sisi
Silaha zote.
Na katika nuru
Tutembee nawe,
Hata tukiomba,
Twaishi sisi.
Tufundishe sisi
Kwa kazi yako,
Na tuwe tayari
Usoni mwako
Tuimbe na kushuka,
Kwa bidii kuu ;
Mioyo ifanane
Wako, Mwokozi.
Yesu atuletea
Wokovu waamini ;
Asema : « mimi mlango,
Muingiye kwangu ».
Kutuongoza kwa Baba,
Alifa mutini,
Na sasa duniani
Twamjua sauti.
Kwa kondoo apendazo
Yeye ni Mchungaji :
Azilinda mwenyewe
Hata kuzikinga.
Azipapo uzima
Ni milele yote ;
Uwezo wake mkubwa
Ni ukingo wao.
Hakuna atakaye
Nitosha mkononi ;
Mwokozi atuongoza
Katika njia nzuri.
Aonapo unyonge,
Atuhakikisha,
Na matunzo ya pendo
Anatuzungusha.
Tuonje kwa uepo wake
Muchungaji mkubwa,
Uwingi wa uzima
Atupatiao ;
Tukimutegemea,
Twatembea huru,
Na tuufurahie
Uepo wake nasi.
Hakuna duniani, muji unaodumu,
Ambamo twaweza kaa, (bis)
Makao duniani ni hema bila nguvu
Iangushwayo na upepo.
Hakuna duniani, muji unaodumu,
Muji wetu ni mbinguni, (bis)
Punde tutasikia sauti ya nguvu,
Sauti yakuondoka.
Hakuna duniani, muji unaodumu,
Tutaupata baadaye, (bis)
Tuungojeapo, imani yauleta
Mioyo yaufurahia.
Punde muda mdogo, wa kazi na kungoja…
Milango itafunguka, (bis)
Muji wa Mungu hai, wa juu, udumuo,
Makao ya wateule.
Neno lako ni utajiri,
Ni kweli iliyo hakika,
Tayari kwa unyonge wetu
Katika ukubwa wake.
Mungu, Neno lako laficha
Hazina damani
Kwani Roho afunua humo
Yesu, njia moja ya juu.
Neno lako, ujumbe hai,
Unaoleta uheri,
Salama, raha na bidii
Tumufwatapo Mwokozi.
Neno lako ni nuru safi,
Ituongozayo sisi
Ili tuweze, Baba Mpendwa,
Kukutukuza duniani.
Neno, kwa Mwanako mwenyewe
Linataka kutufunga,
Lionyeshapo sifa zote
Za Mwokozi, Bwana wetu.
Atakuwaje unyongeni
Mtoto wako,
Asipoweza, zikini,
Kujikinga
Kwa pendo lako aminifu,
Mungu mwema,
Anaweza ishi bawani,
Akilindwa.
Ni mgeni hapa duniani
Haogopi.
Mungu wa pendo na nuru
Amuongoza
Na uepo wako muzuri,
Ee Mwokozi !
Ni msaada wake kwa mateso
Yamujiapo.
Avukapo maji marefu,
Yuko nawe;
Salama tamu umupayo
Yampa nguvu.
Ni uheri kando ya Baba,
Atakuona,
Na uso kwa uso nuruni,
Ataabudu.
« Neema yakutosha ». Neno lilo tamu !
Latosha kwa yote kuenda hadi mwisho,
Tangulio nzuri ya heri ya ajabu
Tutakayoonja kando yako, Yesu.
« Neema yakutosha ». Kati unyonge wetu,
Twawezeshwa, Bwana, Twapata msaada ;
Unatupa nguvu hata katika taabu,
Unapotutunza na mapendo yako.
Kwa neema yako, nyumbani mwake Baba,
Tutaweza kuonja baraka zako,
Tukikumbuka, juu, siku, hapa duniani,
Ulimotujibu : « Neema yakutosha ».
Kwa siku za jaribu,
Vita, na mateso,
Mkononi mwake Baba,
Tumwange machozi,
Hivi tusife moyo,
Tumutegemeye.
Tufunzwe kwa magoti
Na Mungu Mukubwa.
Aruhusu mateso
Ili atubariki ;
Kamwe mukono wake
Hautatuvunja.
Tawi asafishalo
Ni lile apendalo,
Ili duniani humu
Lizae matuda.
Adibisho aminifu
Lake Mtakatifu,
Ambamo neema ya juu
Yazaa matunda !
Wafundisha duniani
Watoto wapendwa
Tukuzwa, Baba mpenzi,
Kwa matunzo yako !
Ee Bwana, gizani kubwa,
Twakuhitaji wewe ;
Tunaonja mema mengi
Kupitia imani.
Huruma yako penzi
Yatuzunguka kila saa,
Moyo wetu wafurika…
Ila hatukuone.
Twakujua bila shaka,
Yesu, kuliko mbele
Ulipofwata safari,
Yakwenda msalabani.
Kanisa lakuhesabu,
Siyo hapa, duniani,
Ila mbinguni, kwa Baba,
Ambapo utatokea.
Imani, jicho la nafsi,
Yapanda juu ya mbingu,
Bibi arusi atazama
Mwokozi mutukufu.
Akishangaa anaabudu,
Akutamani urudi :
Kwa heri yake akosa
Kuwa nawe milele.
Hivi twaweza kungoja
Siku hiyo na nzuri,
Ambapo sauti yako,
Itafufua wafu,
Nakukusanya wahai,
Itatimiza yote
Na tutakwenda pamoja ;
Bwana, tutakuona.
Kwa ahadi zako, Mungu,
Wako wanapumuzika.
Msaada wao, nguvu yako,
Neema yako, mwamba wao.
Ulitupa yote, Mungu,
Katika Yesu, zawadi.
Kwake twafika mbinguni,
Kwake tunakubariki.
Utuwezeshe kupima
Ukubwa wa pendo lako,
Na sasa, bila kuchoka,
Tunaimba wema wako.
Unifunze, Bwana,
Kila siku ;
Linda moyo wangu
Kando yako.
Kati njia nzuri
Nitembee mimi,
Nikikutazama,
Ee Mwokozi !
Bwana, matesoni,
Unifunze ;
Juu ya bahari,
Niongoze.
Katika
Unanitazama,
Unaniongoza :
Siogope.
Roho wako, Bwana,
Anifunze
Niweze kuishi,
Kwako Bwana.
Pote hadi mwisho,
Kwa uwezo wako,
Nibaki mkononi,
Mwako Bwana.
Nani akujuaye,
Mungu milele,
Bwana na Mwalimu,
Mutakatifu ?
Wewe ni mukubwa,
Kuliko mbingu,
Na hakuna kitu
Kikupitacho.
Mbali yako Bwana
Mutu ametengwa ?
Hapana, neema
Ilimtafuta.
Mungu bila mpaka,
Asiyeguswa,
Unatualika
Kukukaribia.
Moyo wako, Baba,
‘Katoa Yesu,
Yesu ndiye nuru,
Pia wokovu.
Kwa damu atakasa
Uovu wetu;
Twapata kuishi
Hadi milele.
Zawadi hii kuu
Ni kwa waamini ;
Ni sehemu gani
Kuwa watoto !
Tunaimba hadi
Kule mbinguni,
Tukikushukuru,
Mungu wa pendo.
Kwa Mungu, tulia nafsi yangu ;
Yesu yupo, daima na wewe.
Matesoni, majini hata moto,
Pendo
Mungu akikufunza na kukupima,
Anakuongoza kwenye heri.
Pumuzika, ukimutumaini,
Muachie Yesu matunzo yako.
Zamani yeye alikusaidia,
Atabaki Kiongozi, Mwokozi.
Itatuliza mawimbi yote.
Pumuzika, Mungu hakusahau,
Saa yaja Yesu akujapo.
Utafahamu mateso ya maisha,
Utaona kwamba ni baraka.
Hivi Imani yako imuheshimu
Mungu aliyekupenda wewe.
Sifa kwako Mungu, ulitaka duniani
Waabudu wa kweli wamzunguke Baba !
Kwa kundi lako zamani ulifichama,
kwa damu ya Yesu twakaribia.
Yesu ndiye musingi wa kanisa lake,
Jiwe kuu na hai, alikataliwa,
La samani kwako, la mshangao kwetu.
utukufu, kwake nyumbani mwa Baba !
Tunakusanyika, sisi kwa jina lake,
Wote kwa nia moja, wakuimbia wewe.
Ni hekaluni humu kao la Roho,
Sifa, Ee Mungu, yapanda na kuJaa.
Baba, tutajua, tukiwa mbele yako
Ulivyomupenda kila muteule,
Tutashukuru neema yako milele
Tulioipokea katika Yesu.
Bila mipango yako hatungeliishi
Kwa imani tunapokea wokovu ;
Tunasifu neema yako bila mwisho
Iliyotuchagua kuwa mbinguni.
Mpango ajabu wa Mungu mwenye hekima :
Kuwa na Yesu katika utukufu !
Tumetayarishwa kufanana na yeye
Katika pendo lako toka milele ;
Hazina kubwa katika fumbo la Mungu
Tutakaloweza kujua daima,
Tukifurahi katika nyumba ya Baba :
Ee Baba, jina lako liinuliwe !
Sifa ni kwako, Ulifufuka !
Kwako ni ushindi
Milele yote !
Ukingaa nuru,
Na malaika
Alitosha jiwe
La kaburini
Refrain : Bwana mtukufu,
Walio wako
Waimba ushindi
Milele yote.
Salama kubwa,
Yesu yu hai !
Furaha yajaa
Mioyo yetu !
Tukijaa furaha
Twaweza, Bwana,
Tangaza daima
Kwamba yu hai !
Bwana mtukufu, etc.
Tumeketishwa
Kando ya Mungu,
Punde, neema gani !
Utatoka juu.
Wavikwa zahabu,
Mwokozi Mkubwa,
Kitini mwa enzi,
Waheshimiwa,
Bwana Mtukufu, etc.
Yesu amefufuka, utukufu kwake !
Alitokea wake, nao hawakuamini.
Kuona mikono, mbavu ; kugusa machapa,
Ndipo walisikia sauti hakika.
Kasema : « Amani kwenu » ! na kwa uepo wake,
Wakajaa kushangaa, na furaha kubwa.
Kati wawili, watatu wanaomuabudu,
Yupo kama zamani kwa wamukuzao.
Kristo alishinda kifo : nguvu za milele !
Tunatukuza, Bwana, kazi yako nzuri.
Sadaka ilitosha kwa Mungu mwenye nuru ;
Ushindini twaona sifa yake Baba.
Baragumu italia utakapokuja
Kanisa litajibu kwa sauti yako.
Tukiwa na mwili mpya, tutakufanana,
Tutakuona, Kondoo, Mukombozi wetu.
Yesu, Mukombozi wetu, Bwana wa uzima,
Toka kifo na woga, wewe wafungua.
Kifo, ushindi wako, nguvu yako vipi ?
Pamoja twakuabudu, Bwana mutukufu.
Kwa imani, twaweza yote
Kwa Mungu wetu Mukubwa ;
Ni jicho lionalo mbali,
Mkono ushikao vipawa,
Na ni utamu uonjao,
Matunda mbele ya siku ;
Inapoivuka jangwa kuu,
Imestarehe nyumbani.
Yapigana bila silaha,
Kupoteza ili ipate,
Kuimba ikimwanga machozi,
Ikiteswa, yatawala ;
Kupanda, ikiona bondeni
Kwa mbali, shamba lakomaa ;
Inatii na kuweza pia,
Imani hii ina haki.
Tangu mababu wa zamani,
Bendera ilipepea ;
Mtazame jeshi kubwa lile
Ambalo lina Kichwa juu ;
Lina historia ndefu
Na hiki kizazi chetu,
Labda, kitaiona sifa,
Nakuvikwa taji lake.
Imani kubwa ya hakika :
Dunia, mauti vyashindwa ;
Sababu ya msimamo wake,
Ni msalaba wake Yesu.
Bado kidogo, mawinguni,
Wakristo, tutasafiri ;
Imani itabadilishwa,
Na tutamuona Yesu.
Kuna njia ya amani na
Nuru, usalama pia
Tunayopitia duniani
Tukiwa na moyo huru.
Ni nyembamba na takatifu
Huko mbali ya dunia !
Upendo wafukuza woga
Hapo Yesu alipopita.
Ni njia ambayo, duniani
Yatufungulia pendo,
Na uso wake unaangaza
Nuru yazidi daima.
Mpaka wakati tutafika
Mbele ya kiti cha enzi,
Nyumbani munamojaa nuru
Ya Mwana wa Mungu wetu.
Kama bikira katika mufano,
Bwana Yesu, sisi tunalala !
Wengi wako, wasahau mufano,
Wamekuwa rafiki za dunia
Lakini wote wanahamakiwa,
Twakuita tukipiga magoti !
Ufukuze kutokujali kwetu,
Tuamshe, Bwana, tuamshe !
Tukitafuta mambo ya dunia,
Tumesahau mara na mara
Neno lile, ee kristo, lililo muhimu,
La kuketi na kukusikiliza !
Ila Roho wako asema nasi
Kwamba unakuja, Bwana arusi !
Kwa ujasiri, twatamani uje :
Tuamshe, Bwana, tuamshe !
Ikifichwa katika udongo mbaya,
Bwana, talanta haikutoa !
Kando yetu, nuru yetu zaifu
Haikuangazia usiku.
Tunaweza kwa saa ile ya mwisho,
Kuzaa matunda na kutumika
Hadi siku ya kuingia kwako.
Tuamshe, Bwana, tuamshe !
Yesu Mwana wa pendo lako,
Ana bei gani Baba !
Analisha imani yetu,
Na utawa, siri kubwa.
Njiani mwa dunia hii,
Yeye alikutumikia.
Toka sanduku kwa Kalvari,
Alikupendeza wewe.
Mwana wako alifunua
Neema, kweli, yako Mungu ;
Alikutambulisha wewe,
Hivi ukaonekana.
Uzima wake ni sadaka,
Kifo, manukato bora
Ya Mtu mtakatifu kwa asili,
Mutiifu mkamilifu.
Amevikwa na utukufu,
Furaha yako, pumziko,
Alituandalia mwenyewe
Fasi pamoja naye juu.
Nguvu, tegemeo ni gani ?
Ukingo, mwamba wa mkristo ?
Na heshima yake ni gani
???
Hatarini, matesoni ?
Ni lile Neno la Bwana.
Upanga mkali ni upi
Wa kuhukumu waovu,
Uliovunja silaha nzito,
Utengao viungo vya mwili,
Ufunuao siri zote ?
Ni lile Neno la Bwana.
Nani avumaye vema,
Nyakati zituliazo ?
Nani aimbaye tumaini,
Mapendo pia na salama,
Siku za huzuni, taabu ?
Ni lile Neno la Bwana.
Neno lake liwe kwangu,
Chemchemu na ngao yangu,
Silaha ya kupiganisha,
Nguzo ya roho inayochoka !
Niwe daima mushindi
Kwa lile Neno la Bwana !
Twakungoja, Bwana, kuliko hata zamu,
Twakesha usiku, twangoja asubui ;
Kuamka kwa ndani ya mioyo miaminifu,
Nyota yaangaza kutoka mbinguni.
Umekataliwa sasa umeinuliwa,
Siku ile wewe waitarajia
Karamu ya Kondoo, Bwana arusi, yaja,
Twakuelekezea naziri za pendo.
Na kanisa lako, lakuabudu, ee Bwana,
Lahitaji kuwa nawe na kukuona.
Ndani yake, Roho anaamusha kabisa
Wimbo wa imani na wa tumaini.
Kuja na utwae hazina hii mbinguni
Iliyo duniani ikikungojea,
Ukiweka juu ya taji ya zahabu,
Lulu nzuri sana, linaloangaza !
Kando yako, Mungu,
Kando yako
Sauti ya imani :
Kando yako
Hata katika taabu
Ijaayo kama muto,
Niwe Kando yako
Mungu wangu !
Kando yako Bwana,
Kando yako
Nishike zikini,
Kando yako
Hata mateso mengi
Yafanya kazi yake,
Unilinde mimi,
Kando yako !
Milele na wewe
Kando yako
Unisaidie,
Nihimize
Shetani angurume,
Nipo pendoni mwako
Milele na wewe,
Kando yako.
Kando yako Mungu,
Njiani tuu !
Unilinde wewe
Unishike.
Msafiri, jipe moyo!
Safari inakwisha.
Kando yako Mungu,
Kando yako.
Mungu Mukuu ! Unaniona vema ;
Ulinijua, toka mbinguni.
Nawezaje kimbia nuru yako
Jicho lako lanifwata pote.
Nikitembea wala kusimama,
Tazama popote wanishika ;
Na nikiwa tayari kwa kusema,
Umejua nitakayo yasema.
Nikitaka kukimbilia mbali,
Na shimoni kutafuta
Kupanda juu : Pote, Mungu wa nuru,
Utanipata kwa mwanga wako.
Kwa imani, nafika mbele yako :
Kwa pendo,Yesu alinikomboa ;
Nimepokelewa usoni mwako,
Nikiwa nimesafishwa mimi.
Unipime, ee Mungu muaminifu,
Unitazame, unitakase ;
Niongoze katika njia yako
Ukinipatia kukusifu.
Kuna chombo baharini,
Kwa wakati muzuri ;
Ikiendelea mbele
Kwa njia ya amani.
Kwa gafla upepo ukaja,
Wingu zikatoweka
{Na zoruba kunyanguka
Zaleta woga kweli.} (bis)
Kweli mashaka ni mengi
Ya wasafiri hao ;
Na katika uzaifu
Wana imani ndogo
Kuna asiye waacha
Hata akisinziya,
{Ni lazima kumuamusha ?
Si rafiki mupendwa ?} (bis)
Ee Bwana hautujali ?
Sasa twaangamia !
Wewe unaweza vyote,
Twakusihi utuokowe !
Akaja karibu nao
Kukemea upepo !
{Na akaihamakia
Imani yao ndogo.} (bis)
Mara nyingi maishani,
Upepo unavuma,
Hata Yesu akituombea
Na kumaliza shida.
Tutegemee upendo :
Yeye habadiliki ;
{Kila siku ni mchungaji
Wa kondoo mashakani.} (bis)
Mukimbizi ! bila makimbilio,
Wakimbia Mungu bila sheria,
Wataka kuonja Injili, salama ?
Mupotevu, rudia nyumbani !
Saa zapita, umilele wakuja ;
Ni wakati wakuokolewa ;
Usimame na ukitumaini,
Mupotevu, rudia nyumbani !
Kuja ili upate kanzu nzuri,
Na uponyaji wa maovu yako.
Ingia karamuni kwa furaha ;
Mupotevu, rudia nyumbani !
Munaokosa salama,
Muje, Yesu aitoa ;
Upendo na wema wake,
Havifukuze mutu
Aingiapo moyoni
Analeta uheri
Woga inakimbia :
Sifa kwake Yesu !
Ninyi munaosumbuka,
Muje, Yesu awapenda ;
Kwa kusaidia wanyonge,
Alikuja mwenyewe.
Aingiapo moyoni,
Analeta uheri ;
Hakuna fazaiko :
Sifa kwake Yesu !
Ninyi mutetemekao
Munaogopa kufa,
Muje, Yesu Mukombozi
Alishinda mauti.
Na yeye tutaishi,
Naye tutatawala,
Kifo hakitakuwa :
Sifa kwake Yesu !
Habari njema moja
Yasikika,
Yesu anakuita ;
Kuja kwake !
Ukiogopa sheria,
Kwa makosa yako,
Bila woga, kukawa,
Njoo kwa Yesu !
Muone pale Kalvari
Akikufa,
Kajitoa mwenyewe
Msalabani.
Kwa damu ioshayo
Mutu mupotevu,
Umutumainiye !
Njoo kwa Yesu !
Na kwa rehema yake
Yesu atoa.
Apatia muovu
Musamaha.
Fanya haraka sasa,
Muda unapita
Leo siku ya neema,
Njoo kwa yesu !
Kuja, usizuizwe,
Kuja sasa ;
Wokovu ni tayari ;
Yesu angoja.
Ukitaka Kuamini,
Umesamehewa,
Waweza imba : sifa
Kwake Yesu.
Yesu yupo, akuita :
Ataka heri yako
Jibu kwa sauti yake,
Ni Mungu Mukombozi.
Refrain : Njoo kwake, njoo kwake !
Kuja kwa Yesu leo.
Kwa nini wamungojesha ?
Na ni tangu zamani
Wakataa kumusikia ;
Usikawe ! Yu hapo.
Njoo kwake, etc.
Yupo, akitoa mema,
Musamaha wa bure,
Salama isiyopita,
Mbingu pia uheri.
Njoo kwake, etc.
Ni wakati ! wa uzima milele,
Sasa Mwana wa Mungu anakuita.
Ni Yesu ! Mujibu !
Kuja, uingie !
Kwa karamu chumba kiko tayari ;
Waalikwa waenda kwa siku kuu.
Njoo pia, mujibu !
Kuja, uingie.
Ni wakati ! Mulango yuko wazi,
Kwa Mwokozi njia ni wazi sasa.
Njoo pia, mujibu !
Kuja uingie.
Kesho ! Wajua nini iletayo !
Wengi kwa bure watagonga mlango !
Milele kutengwa !
Kuja uingie.
Usingoje kujibu kwa neema,
Leo kunabaki tena nafasi.
Sasa, kuja kwake !
Kuja, uingie.
Sauti inakuita,
Leo njiani sikia,
Ambamo washusha kichwa,
Pasipo kuona mwisho.
Refrain : Kuja kwa Mungu asamehe,
Utapata uheri.
Mungu hafukuzi mutu !
Ni Mungu Mukombozi.
Leo Yesu akuita,
Neema yake, zawadi ;
Atahukumu muasi
Akataaye msamaha
Kuja kwa Mungu asamehe, etc.
Na hadi kwa musalaba
Yesu alikutafuta ;
Alikubali hasira
Kwa kuziondosha zambi
Kuja kwa Mungu asamehe, etc.
Hii sauti inadumu :
Amini Yesu leo !
Nafsi yako, kwa imani,
Ipumzike juu yake !
Kuja kwa Mungu asamehe, etc.
Yesu anagonga mlangoni :
Fungua ! Fungua leo !
Akuletea wokovu :
Fungua ! Fungua leo!
Akuletea neema ;
Anataka aketi kwako ;
Muda unapita mbio ;
Fungua ! Fungua leo !
Fungua, anasamehe
Fungua ! Fungua leo !
Pokea alitoalo :
Fungua ! Fungua leo !
Achana na ubatili
Ataka akufungue ;
Ahadi zake ni kweli !
Fungua ! Fungua leo !
Mwana wake Mungu alikuja duniani,
Kutafuta na kuokowa wapotevu ;
Atakufungua na huu muzigo wa taabu
Unamjua ? (bis)
Unajua mateso yake kwa Kalvari,
Na yaliyomupata juu msalabani ?
Kupitia kifo, unajuwa malipo,
Ya maovu ? (bis)
Wajua samani ya damw'isafishayo
Nani aweza tosha zambi zako zote ?
Wajua kwa Mungu, damu isafishayo :
Ni salama ? (bis)
Kama haujaona neema na nguvu
Ya Mwana Kondoo aliyetundikwa,
Njoo upesi na upate ukombozi kamili.
Umuamini ! (bis)
Pokea musamaha, wokovu na kuishi
Vinavyopatikana katika damu
Umfuate hapa kwa njia barikiwa
Ya mbinguni ! (bis)
Umjibu Mwokozi anayekualika ;
Na uonje furaha ya wateule ;
Jibu leo hii, saa zinapita mbio…
Umuamini ! (bis)
Kama mukijua Mwokozi wangu !
Ni rafiki Mzuri na mupenzi
Ajiunga nami, ananiombea.
Oh ! Ninataka awe vile kwenu.
Refrain : Mwokozi awapenda,
Mutafute kwake
Rafiki mupendwa,
Na Kimbilio.
Mukijua salama nimepata
Iliyoletwa na Mwokozi !
Salama ya juu siyo ya duniani,
Yatiririka kutoka Golgota.
Mwokozi awapenda, etc.
Na mukijua tumaini tamu
Linalotoka kwake Mungu !
Sauti yake yatuliza taabu,
Jicho lake linaleta furaha
Mwokozi awapenda, etc.
Mutakapojua pendo la Yesu,
Mutakapoonja nira yake,
Musifiche hazina hii wenyewe,
Lakini mutangazie wengine !
Mwokozi awapenda, etc.
Muji ule, mtakatifu !
Nani atauingia ?
Nani atakubaliwa,
Pahali pale pa juu ?
Mwenye zambi, ameoshwa
Kati damu ya Yesu,
Aingia milangoni :
Yeye ametakaswa.
Akijaa na furaha,
Ataingia humo,
Kufurahia daima
Yesu na pendo lake.
Ataona utukufu
Wa Kondoo wa Mungu ;
Na ataimba ushindi
Wake milele yote.
Sifa kwa atupendaye !
Kwake nguvu, ushindi !
Utukufu kwake Yesu
Milele na milele !
Kuja kwa Yesu akupendaye,
Alijitoa mutini ;
Ataka kukupokea wewe ;
Atega mikono.
Refrain : Siku nzuri, Mwokozi mwema,
Tukikutegemea mkono,
Katika nyumba yake Baba
Tutatembea sisi.
Ni kwa sasa akuitapo;
Pendoni mwake ni heri
Mugeukie moyo muasi ;
Atakuokoa.
Siku nzuri, Mwokozi mwema, etc.
Muda wapita, saa zaisha ;
Sisi hatujui ya kesho ?
Yesu ni hapa muktanoni ;
Akutega mkono !
Siku nzuri, Mwokozi mwema, etc.
Kuja uliaye
Njoo kwa Mwokozi.
Kwa saa za giza
Mwambie taabu ;
Sema bila woga :
Na Bwana Yesu
Asikia shida.
Acha kulia !
Kuja ! kwa mapendo
Rafiki huyu
Atosha huzuni,
Shaka na muchoko
Afariji mioyo
Ilemewayo.
Umuamini yeye
Acha kulia.
Kwa nafsi zaifu
Utangaze pia
Neema kamili,
Pendo la Mungu.
Sema aamini
Jina la Yesu.
Kwake ni furaha :
Hautalia !
Duniani na mbinguni
Hakuna jina tamu,
Jina ninalolipenda
Kama lile la Kristo
Jina kuu ! Jina kuu
Lililo lake Mwana !
Jina kuu ! Jina kuu
Ni lake Emanueli !
Iwe mtu mukubwa gani,
Hata awe mufalme,
Hata apewe jina gani,
Yesu ni mkubwa kwangu.
Jina kuu ! Jina kuu
Lililo lake Mwana !
Jina kuu ! Jina kuu
Ni lake Emanueli !
Kwa mateso, anatuliza ;
Aponya muzaifu ;
Na analeta bidii
Kwa moyo uteswao.
Jina kuu ! Jina kuu
Lililo lake Mwana !
Jina kuu ! Jina kuu
Ni lake Emanueli !
Analeta raha kubwa
Moyoni mwa muovu !
Hakuna hapa duniani
Uheri kama huu.
Jina kuu ! Jina kuu
Lililo lake Mwana !
Jina kuu ! Jina kuu
Ni lake Emanueli !
Muje kwa Bwana wa uzima,
Muje kwake Bwana Yesu !
Anawaalika leo ninyi
Kwa Neno na Roho wake
Refrain : Ategemeaye wema
Wake hawezi kutupwa,
Wake hawezi kutupwa.
Yesu Kristo ni haki yetu,
Ametufungulia mbingu ;
Kwani pale musalabani
Alijitoa kwa zambi.
Ategemeaye wema etc.
Muje basi kwa uhakika
Mpate uzima, salama ;
Mukiwa mumeokolewa,
Mtapata heri milele
Ategemeaye wema etc.
Yeye ni mwamba imara,
Kwangu ninayechoka,
Kama kinga yenye nguvu
Ya Mungu mawimbini.
Refrain : Mwamba wangu, ngome yangu,
Ni kimbilio langu,
Msaada matatizoni,
Ni Yesu Mukombozi.
Bahari inanguruma ;
Wimbi lanizunguka :
Juu ya Kristo, mwamba wangu
Tumaini na imani.
Mwamba wangu, ngome yangu, etc.
Kwa bure wimbi lavuma
Hakuna hata mwanga ;
Wa salama mawimbini,
Mwanga wafwata giza.
Mwamba wangu, ngome yangu, etc.
Katika hatari kubwa,
Umepata hii kinga ?
Ushike mkono wa nguvu
Wa Yesu Mukombozi
Mwamba wangu, ngome yangu, etc.
Ninapumzika kwako,
Ee Yesu Mwokozi !
Tena yafaa nini
Kwa mtu mwenye zambi ?
Akiongozwa na nuru,
Alindwa pendoni,
Kwenda nyumba ya Baba
Kwenda kila siku,
Refrain : Ninapumzika kwako,
Ee Yesu Mwokozi !
Tena yafaa nini
Ili aonje heri ?
Kwa nyakati mbaya
Unabaki nami,
Ukinipa bidii
Waongeza imani ;
Ni kati moyo wako
Unaponificha ;
Na kwa bure shetani
Ataka anitoshe.
Ninapumzika kwako, etc.
Kwako nina ushindi,
Salama, uhuru ;
Nitakusifu wewe
Katika milele.
Kama heri ipitayo
Yaweza komeshwa,
Neema yako yatosha
Kwa kui na kufa !
Ninapumzika kwako, etc.
Njoo, wewe mpotevu
Njoo kwa Mwokozi
Ona mkono wake
Na kuushika
Anakualika :
Umusikie ;
Kama unasita,
Ona msalaba.
Alikukomboa
Alikufia ;
Pokea neema
Kwa imani tu.
Utapata kuishi
Milele yote ;
Njoo, anasamehe
Kwa damu yake.
Mwokozi apenda
Muwe pamoja.
Akutambulisha
Pendo lake kuu
Kuja kwa imani ;
Umtegemeye,
Awe tumaini
Na mema yako.
Wewe una tangu leo
Tumaini lililo hai ?
Umepata kwa uhakika
Tegemeo kwake Yesu ?
Ninaye Mwokozi ;
Anatosha kwangu
Ninaye Mwokozi
Tumaini langu ni kwake.
Kama wewe umechoka,
Na furaha ikitoweka
Ni nani atakufariji ?
Rafiki yako ni nani ?
Ninaye Mwokozi ;
Anatosha kwangu
Ninaye Mwokozi
Kweli Neno lake ni tamu
Kwa leo na hata jana,
Ukihuzunika vikali,
Ukichukizwa na maisha,
Unategemea nani ?
Ninaye Mwokozi ;
Anatosha kwangu
Ninaye Mwokozi
Nategemea pendo lake.
Ungalipata nafasi
Katika mikono ya Yesu !
Na kupokea neema yake !
Rafiki, njoo utaishi.
Ninaye Mwokozi ;
Anatosha kwangu
Ninaye Mwokozi
Heri yule amtazamaye.
Kuja kwake, akuita,
Akuita leo.
Siku nyingi uliasi :
Leo kuja kwake.
Akupenda, akupenda,
Akupenda leo.
Hata kwa unyonge wako,
Leo kuja kwake.
Asamehe, asamehe,
Asamehe leo.
Pokea wokovu wake ;
Leo kuja kwake !
Aondosha, aondosha,
Zambi zako leo.
Hii ni siku ya neema ;
Leo kuja kwake.