Nyimbo Swahili_Congo

1, 2, 3, 4, 5, 6, 7, 8, 9, 10, 11, 12, 13, 14, 15, 16, 17, 18, 19, 20, 21, 22, 23, 24, 25, 26, 27, 28, 29, 30, 31, 32, 33, 34, 35, 36, 37, 38, 39, 40, 41, 42, 43, 44, 45, 46, 47, 48, 49, 50, 51, 52, 53, 54, 55, 56, 57, 58, 59, 60, 61, 62, 63, 64, 65, 66, 67, 68, 69, 70, 71, 72, 73, 74, 75, 76, 77, 78, 79, 80, 81, 82, 83, 84, 85, 86, 87, 88, 89, 90, 91, 92, 93, 94, 95, 96, 97, 98, 99, 100, 101, 102, 103, 104, 105, 106, 107, 108, 109, 110, 111, 112, 113, 114, 115, 116, 117, 118, 119, 120, 121, 122, 123, 124, 125, 126, 127, 128, 129, 130, 131, 132, 133, 134, 135, 136, 137, 138, 139, 140, 141, 142, 143, 144, 145, 146, 147, 148, 149, 150, 151, 152, 153, 154, 155, 156, 157, 158, 159, 160, 161, 162, 163, 164, 165, 166, 167, 168, 169, 170, 171, 172, 173, 174, 175, 176, 177, 178, 179, 180, 181, 182, 183, 184, 185, 186, 187, 188, 189, 190, 191, 192, 193, 194, 195, 196, 197, 198, 199, 200, 201, 202, 203, 204, 205, 206, 207, 208, 209, 210, 211, 212, 213, 214, 215, 216, 217, 218, 219, 220, 221, 222, 223, 224, 225, 226, 227, 228, 229, 230, 231, 232, 233, 234, 235, 236, 237, 238, 239, 240, 241, 242, 243, 244, 245, 246, 247, 248, 249, 250, 251, 252, 253, 254, 255, 256, 257, 258, 259, 260, 261, 262, 263, 264, 265, 266, 267, 268, 269, 270, 271.

 

1.                       Wimbo 1

Wimbo 1 — kipande 1

 

Tunakuabudu Baba Mungu

Wewe uishie nuruni

Unapambanua mbingu

Twakusanyika mbele yako

Wana wa pendo lako kubwa

Tunasifu jina lako,

{Tunakuheshimu,

Muumba wa vyote

Aleluya ! utukufu,

Kwake Mungu na Mwokozi

Aleluya !}

Wimbo 1 — kipande 2

Wewe ulituangazia,

Mwenye enzi, Baba wa neema,

Kupitia Mwana wako

Kwake tunakubariki,

Twakuabudu, tunakusifu

Na kukutukuza hapa,

{Tunakuheshimu,} etc.

2.                       Wimbo 2

Wimbo 2 — kipande 1

Tuimbe wimbo takatifu

Wakusifu Mwana wa pekee,

Milele Mwana wa Mungu

Kwa kufa na kuishi kwake

Alifunua neema kubwa

Njia  nzuri ya mbinguni

Sifa na heshima

Kwa yesu Mwokozi

Aleluya ! utukufu,

Kwako Bwana !

Aleluya! Aleluya.

Wimbo 2 — kipande 2

Yesu tunakuheshimu

Utakayebaki milele

Wimbo wa wakombolewa.

Uliumizwa tuokoke

Ulichubuliwa tupone

Tuishi kwa ufufuko

Sifa na heshima

Kwa Yesu Mwokozi etc.

3.                       Wimbo 3

Yesu ukombozi wetu

Kwa teso ulitupatia

Ukombozi wa milele

Bwana mwenye utukufu

Ndani yako tuna amani,

Na ushindi na baraka.

Mwokozi muzuri

Uketiye juu

Kwa uzuri

Na heshima

Twakuabudu

Tutakukuza milele.

4.                       Wimbo 4

Wimbo 4 — kipande 1

Tukuzwa Baba wetu (bis)

Uliyetuandalia makao juu mbinguni

Umetowa wokovu (bis)

Wastahili shukrani ya mapendo na kusifu

Wimbo 4 — kipande 2

Tukuzwa Mwana Kondoo (bis)

Kwakuokowa kundi ulikufa msalabani

Ukashinda shetani (bis)

Mukombozi wa ajabu sifa ni kwako milele.

Wimbo 4 — kipande 3

Kweli tukuzwa Bwana (bis)

Pokea pekee nguvu, kuzo, heshima na, ufalme.

Milele na milele (bis)

Tutaimba wokovu, ushindi wa wema wako.

5.                       Wimbo 5

Wimbo 5 — kipande 1

Pendo lako latukusanya

Kando ya Kristo pamoja

Vinywa vyetu vinatukuza

Pendo lako la milele

Utukufu ni wako Baba !

Sifa kwa mapendo yako !

Watoto wako wakusifu hapa,

Wakingoja makao mazuri.

Wimbo 5 — kipande 2

Kwa neema, fumbo ya Mungu

Ulitaka tangu mbele,

Kutuingiza Baba wetu,

Katika uheri wako

Utukufu ni wako Baba, etc.

Wimbo 5 — kipande 3

Kutaka kwa mapendo yako

Hakungeweza tosheka,

Bila kupata mbele yako,

Wakombolewa kamili

Utukufu ni wako Baba, etc.

Wimbo 5 — kipande 4

Salama, mema, mbingu yako,

Tumevipata kwa Yesu ;

Punde atatuita kwa ushindi,

Kwake tutainuliwa

Utukufu ni wako Baba, etc.

Wimbo 5 — kipande 5

Mungu twainamisha nafsi

Mbele ya mapendo yako;

Timiza mahitaji yetu;

Fanya Yesu aje mbio

Utukufuni wako Baba, etc.

6.                       Wimbo 6

Wimbo 6 — kipande 1

Tukuze Mungu wa mapendo

Wa amani kwa wimbo safi

Aliye kwa wema fahari

funguwa njia ya mbingu

Kwa neema iliyo bora

Na sisi wabarikiwa,

Hai kwa moyo wa furaha

Tuinuwe nyimbo zetu.

Wimbo 6 — kipande 2

Mioyo yetu yakutukuza

Mwenye uwezo na pendo

Sisi tunakutegemea

Kwa sasa na kwa milele.

Nguvu, wema, neema, uwezo

Ndani yako vinasifu

Na kanisa kwa uhakika

Lakungojea urudi.


7.                       Wimbo 7

Wimbo 7 — kipande 1

Kwa Yesu tunatoa

Zabihu za sifa zetu

Kwa Yesu tunaabudu

Malaika vilevile

Mungu ubarikiwe tunapokusanyika

Wimbo 7 — kipande 2

Tulikuwa zambini

Sote wana wa gazabu

Ukatuweka huru

Ndani yako tuna Baba

Mungu ubarikiwe tunapokusanyika.

Wimbo 7 — kipande 3

Na tumepewa Yesu

Na umetuweka kwake

Ndani yake tuliitwa

Kupewa taji milele

Mungu ubarikiwe tunapokusanyika.

Wimbo 7 — kipande 4

Alituahidiya

Mwana aja kututwaa

Kwenye makao ya juu

Tupendapo kumungoja

Mungu ubarikiwe tunapokusanyika.

Wimbo 7 — kipande 5

Hivi tutakukuza

Katika kuzo na nuru

Na tutasema tena

Na Kanisa lako lote

Mungu ubarikiwe tunapokusanyika.

8.                       Wimbo 8

Wimbo 8 — kipande 1

Asifiwe Mwokozi

Na Mwana pekee wa Mungu

Alikuja duniani,

Kuokoa wenye zambi

Ee Yesu utukuzwe milele na milele. (bis)

Wimbo 8 — kipande 2

Ee Mwana ulikuja

Kufa kifo cha aibu

Ukashinda kaburi

Kwa uwezo wa milele

Na Ulivunja nguvu za giza na mauti. (bis)

Wimbo 8 — kipande 3

Kwa pendo ulikunywa

Kikambekichungu sana

Na ukatupatia

Kikombe cha ukombozi

Ee yesu utukuzwe milele na milele. (bis)

9.                       Wimbo 9

Wimbo 9 — kipande 1

Sifa kwako kanisani

Kwa pendo lako nzuri !

Mwenyewe ulilinunua,

Ni lako bila mwisho.

Nyumbani mwa Baba yako

Punde utalileta ;

Likingaa nuru yako

Utalileta kwako.

Wimbo 9 — kipande 2

Sifa kwako kanisani !

Kuna muda wa taabu,

Mbele yakukubaliwa

Pasipo tena chozi

Nyumbani kwenye uzima,

Ulioshinda kifo,

Bibi arusi akishangaa

Atabariki Kondoo.

Wimbo 9 — kipande 3

Sifa kwako kanisani !

Sifa kwa Mukombozi !

Unajiunga na sisi,

Kifuani watubeba.

Siku nzuri inakuja,

Tukuonyeshe kwa yote ;

Utukute bila taka,

Tukikushuhudia.

10.                  Wimbo 10

Wimbo 10 — kipande 1

Sifa kwa Mwana – Kondoo Mwokozi

Ndani yake kifo kilishindwa

Adui aliona nguvu yake

Vilevile kaburi inamutii

Utukufu kwako Yesu

Utukufu Bwana Yesu

Na kuzimu kumeshindwa

Ushindi (bis).

Wimbo 10 — kipande 2

Vile Kristo alikataliwa

Na kukaa mbinguni aki’ngaa

Na Kanisa lisilo julikana

Karibuni litavikwa utukufu

Utukufu kwako Yesu

Utukufu Bwana Yesu

Na kuzimu kumeshindwa

Ushindi (bis).


Wimbo 10 — kipande 3

Yesu uliahidi kurudi

Kututafuta punde yu waja

Na wafalme katika utukufu

Tutaimba sote wimbo wa ushindi

Utukufu kwako Yesu

Utukufu Bwana Yesu

Na mauti imeshindwa

Ushindi (bis).

11.                  Wimbo 11

Wimbo 11 — kipande 1

Tuonapo juu, sifa unayovikwa

Na tunakuabudu, tukikutazama,

Sifa iangazayo, Yesu yakuzunguka

Inatukumbusha msalaba na haya.

Wimbo 11 — kipande 2

Na kwa ule woga, pia huzuni mkubwa,

Kwa taji kichwani, miiba na zihaka,

Kwa haya ya damu dunia ilikupa,

Jibu, Bwana Yesu, Sifa yako juu.

Wimbo 11 — kipande 3

Uliachwa mtini, ukikunywa kikombe,

Bila yeyote wakukusaidia ;

Sasa watukuzwa juu ya kiti cha enzi,

Na kwa sifa yako, mbingu zitangaze.

Wimbo 11 — kipande 4

Uso wake Mungu, kwa saa ile kubwa,

Ulikugeukia, wewe Mwanawe,

Kichwa chako Kristo, kimeivikwa taji,

Inayotangaza sifa zako juu.

Wimbo 11 — kipande 5

Ee Mwokozi Mwema ! Unayeabudiwa !

MwanaKondoo pekee unayestahili,

Hapa na mbinguni, yote ikutangaze

Nguvu na uwezo, na ukubwa wako.

Wimbo 11 — kipande 6

Wimbo wakutukuza kwa sifa ya Baba

Unatoka kwetu, tulio wapendwa,

Wimbo wa milele ulioanza duniani

Umutukuze Baba na Mwana wake !

12.                  Wimbo 12

Kwa aliye tuokoa

Kwa damu’katusafisha

ufalme na ukuu ni vyake

MwanaKondoo astahili

utajiri, heshima, nguvu,

mamlaka, hekima, na sifa. (bis)

13.                  Wimbo 13

Wimbo 13 — kipande 1

Tutukuze pendo, uwezo wa Mwokozi,

Kujishusha kwake na utiifu tele

Alija akashinda maadui wetu ;

Kwa msalaba wake – aliwamiliki. (bis)

Wimbo 13 — kipande 2

Tutukuze wema wa Mfalme wa uzima :

Kwa ajili yetu aliteswa msalabani ;

Na kwa kifo chake alitukomboa ;

Tumepata kuwa – watoto wapendwa. (bis)

Wimbo 13 — kipande 3

Tutukuze haki kamili ya Mwokozi ;

Alishinda nguvu za yule adui wetu ;

Alishinda kifo na alifufuka ;

Tumepata sifa – yake kwa milele. (bis)

Wimbo 13 — kipande 4

Tutukuze ukubwa usiyo na mwisho

Wa yule aliyetoa uzima wake.

Akuja akingaa, na kwa macho yetu

Tutamutazama – milele mbinguni. (bis)

14.                  Wimbo 14

Wimbo 14 — kipande 1

Ku’ngaa kwa Sura kamili ya Mungu

Mwana wa milele muabudiwa

Sifa kwako wewe ustahiliye

Kuheshimiwa na wote milele.

Wimbo 14 — kipande 2

Ulishuka ili uwe zabihu,

Kwako tu Mungu akatukuzwa

Utakatifu, upendo, haki yake

Msalaba ukavikuza vyote.

Wimbo 14 — kipande 3

Sasa umeinuliwa kwa Mungu

Karibu na ukubwa mbinguni

Twakuona na utukufu mwingi

Mwana wa watu uliyefufuka.

Wimbo 14 — kipande 4

Twakuabudu wewe ambaye taji

Lakumbusha mateso ya kifo

Bwana Yesu tutakusifu wewe

Tukikizunguka kiti cha enzi

15.                  Wimbo 15

Wimbo 15 — kipande 1

Watoa neema na kuzo

E Bwana Mungu wetu, katika Yesu !

Ubarikiwe na wateule wako

Wenye uheri kukuamini. (bis)

Wimbo 15 — kipande 2

Ulitupatia neema,

iliyotupa usalama moyoni :

Wenye heri tutaingia mbinguni

Kunapo’ngaa uso wako. (bis)

Wimbo 15 — kipande 3

Wewe watuwekea sifa

Iliyo ya MwanaKondoo mbinguni

Tutakuwa naye katika uheri,

tunda la kazi ya msalaba. (bis)

Wimbo 15 — kipande 4

Mungu wa neema na sifa !

Wapendwa wako wanaye Roho wako,

Kwa jina la Yesu tunakuabudu

Yeye ni ukombozi wetu. (bis)

16.                  Wimbo 16

Wimbo 16 — kipande 1

Kukuimbia Mungu, wa mapendo na kweli

Kuabudu, kubariki na kufurahi

Kushangilia ushindi wa Bwana Yesu

Ni sehemu tuliyoitwaa kwa imani.

Wimbo 16 — kipande 2

Jina lako lisifiwe, Neema yako

Iliyotujia katika uzuri

Tulikuwa gizani sasa uso wako

Waleta mishale ya nuru mioyoni.

Wimbo 16 — kipande 3

Tupo wana wako, jina nzuri la Baba

Latujaza heri, hakika, amani

Roho wako mhuri, mwangaza na Mwalimu

Na karibu nawe tumekubaliwa.

Wimbo 16 — kipande 4

Ni mapendo yako, kifo, uhai wako

Vilivyotuletea hii sehemu

Kila moja wetu asisahau kamwe

Kwamba tulitakaswa ili tumukuze.

17.                  Wimbo 17

Wimbo 17 — kipande 1

Ukamilifu usiyoweza kusemwa

Wa uwezo, mapendo, hakiba’siyokwisha, – isiyokwisha

Mwana wa Mungu milele !

Utukufu wa mbinguni

Kwa amani yako, Kanisa lako pe ndwa

Lainama kuabudu (ter)

Wimbo 17 — kipande 2

Wakaa ee Yesu, kwa kuume kwa Baba

Ukivikwa uwezo, nuru, utukufu – na utukufu

Mungu wetu (bis)

Mioyo zetu (bis)

Yainama mbele yako kwa kutii

Pia kukuinua. (ter)

18.                  Wimbo 18

Wimbo 18 — kipande 1

Mbinguni kwa kiti cha Baba

Twakuona ee Mwokozi

Pumzikoni vile nuruni

Una uwezo na ku’ngaa

Kazi ya neema imekwisha:

Umekaa patakatifu ;

Juu utukufu umepewa

Watawala juu ya vyote.

Wimbo 18 — kipande 2

Twashinda kwa ushindi wako

Yesu Mwokozi muweza,

Juu katika utukufu

Umetangulia wako !

Tuna tumaini la mbingu,

Linalokutegemea

Tuna uhakika wa roho

Ni Musingi wa imani.

Wimbo 18 — kipande 3

Sifa kwa kichwa cha kanisa!

Bibi arusi mupendwa

Pande zako punde atakaa,

Akibariki milele

Wewe Bwana mwenye uzuri

Tutakaofurahia,

Na pendo lako la ajabu

Litakuwa siku zote.

19.                  Wimbo 19

Wimbo 19 — kipande 1

Mungu wa pendo na neema!

Twafurahi kukutana

Mbele ya uso wako mzuri

Kuabudu na kubariki

Na Katika salama yako

Kweli Upewe ibada,

Iletayo mashukurani,

Marashi : jina la Yesu.

Wimbo 19 — kipande 2

Bwana ingia nafsi zetu

Na wema wako wa ajabu,

Utuwashie moto wako

Wa pendo lako Ee Bwana ;

Ndipo sifa zitatokea

Mioyoni mwetu kwa Roho

Ili tuimbe rehema zako

Na pendo ndani ya Yesu.

Wimbo 19 — kipande 3

Tunapenda kuketi pale

Twawekwa na kazi  yake

Na tunafuata nyayo zake,

Hadi mbinguni alipo

Ni pahali patakatifu

Ambapo mlango ni wazi

Sifa za waamini zapanda

Kwako  kupitia Yesu

20.                  Wimbo 20

Wimbo 20 — kipande 1

Umoja wa Kanisa wapendeza

Bwana Yesu, wakufurahisha

Kwa kulipenda ulijitolea

Wataka liwe nawe mbinguni

Wimbo 20 — kipande 2

Roho yako Yesu yatukusanya

Karibu nawe katika pendo

Heri gani kukuabudu pamoja

Twatangaza kufa na kurudi

Wimbo 20 — kipande 3

Ni kutamu ndugu wakikuabudu

Roho wako akiwa kiongozi

Katika nyimbo na maombi yetu

Tunayokutolea pamoja.

Wimbo 20 — kipande 4

Ni kweli palipo uwepo wako

ukileta uhuru moyoni

kila mwamini katika amani

asikia nguvu, uhakika.

Wimbo 20 — kipande 5

Na Itakuwaje kwa mukutano

Mbinguni kanisa litakuona

Furaha gani isiyo na mwisho

utukufuni likikuabudu.

21.                  Wimbo 21

Wimbo 21 — kipande 1

Ulitualika, tena kwa siku hii

Mwokozi Muabudiwa ili tulishwe

Katikati ya jangwa, wajenga meza hii

Kumbusho la pendo lako. (bis)

Wimbo 21 — kipande 2

Kando yako, Bwana,kanisa lazunguka

Kukumbusha kifo chako hadi urudi,

Twavunja mukate, tunakunywa kikombe,

Kumbusho la pendo lako. (bis)

Wimbo 21 — kipande 3

Uovu wetu ulikulemea kichwani

Mzigo wa uchungu na muzito sana;

Lakini kwa amani, tunasherekea

Kumbusho la pendo lako. (bis)

Wimbo 21 — kipande 4

Tukionja mkate huu, na kinywaji hiki

Vinaelekeza macho yetu juu.

Na Punde tutamaliza safari yetu

Tutatambua u pendo. (bis)

Wimbo 21 — kipande 5

Asante Yesu, Mwokozi na Mwaminifu!

Bila kivli tutakuona mbinguni

Na tutatukuza, kwa sifa ya milele,

Ukubwa wa pendo lako. (bis)

22.                  Wimbo 22

Wimbo 22 — kipande 1

Unatuonyesha, (bis)

Yesu, mateso yako, kwa ukombozi wetu

Ukumbusho tamu (bis)

Meza matakatifu, Mwokozi muabudiwa

Tukumbushe pendo, kifo na kurudi. (bis)

Wimbo 22 — kipande 2

Mkate na kikombe (bis)

Unavyotupatia, kutoka neema yako

Ni alama ya kweli (bis)

Visemapo kwa kimya, na vyapasha milele,

Kwa kila mteule, pendo lako Yesu ! (bis)

Wimbo 22 — kipande 3

Tuimbe pamoja (bis)

Neema ile nzuri, na pendo la ajabu,

Ya Mwokozi wetu ! (bis)

Pamoja na shukrani, tukuze kwa uwezo,

Sote kwa umoja, Kondoo aliyekufa. (bis)

23.                  Wimbo 23

Wimbo 23 — kipande 1

Sifa kwa Kondoo ! (bis)

Aliyejitolea,

Akatupatia haki,

Kafungua mbingu ! (bis)

Malaika wakuabudu,

Pokea shukurani

Ya watakatifu Waliokuja kwako. (bis)

Wimbo 23 — kipande 2

Mwokozi muzuri ! (bis)

Twapenda kukumbuka

Tukingojea kuzo

Ya kurudi kwako (bis)

Tunaitaka sasa,

Tutapelekwa huko

Katika milele, Tutaimba wema ! (bis)

24.                  Wimbo 24

Wimbo 24 — kipande 1

Kondoo uliyetolewa !

Twatazama pendo lako,

Kifo pia ushindi wako

Kwetu tuliokombolewa.

Tunazunguka meza yako,

Twatukuza pendo lako

Tukikuabudu Mwokozi mupendwa!

Tunangojea kurudi kwako.

Wimbo 24 — kipande 2

Sisi tulikuwa waovu,

Tukapata msalabani,

Salama na neema nzuri,

Nguvu na heri pamoja.

Tunazunguka meza, etc.

Wimbo 24 — kipande 3

Umetuvika haki yako,

Tumesafishwa kwa damu,

Twakumbusha toleo lako,

Lililofungua mbingu.

Tunazunguka meza, etc.

Wimbo 24 — kipande 4

Fanya mpendwa ! Uzima wako

Uangae ndani mwetu :

Kila moja akutukuze,

Uliye tujaza mema.

Tunazunguka meza, etc.

25.                  Wimbo 25

Wimbo 25 — kipande 1

Mbele ya kiti cha baba

Akaapo kwa heshima

Jicho letu latazama

Uzuri wako Bwana

Utukufu ulio nao

Ndani ya ku’ngaa kwako

Watuangazia kweli

Ndani ya mioyo yetu.

Wimbo 25 — kipande 2

Kungaa kwa uso wako

Siko  kuvutiapo tu

Kwani neema yako kubwa

Yaangaa usoni mwako

Kwa neema ulishuka

Duniani mwa uasi

Ulipotuchukulia

Maovu hata zambi.

Wimbo 25 — kipande 3

Nafsi yashangaa sana

Juu ya upendo huu

Ulio mukubwa sana

Hauna hata mpaka

Hivyo sisi twatamani

Kurudi kwako hapa

Ili tuone, tutamke

Makuu ya pendo lako.


26.                  Wimbo 26

Wimbo 26 — kipande 1

Tukaribie na kwa nyimbo zetu

Mwana Kondoo mupendwa akuzwe

Alishinda na alifufuka

Tutangaze makuu yake yote

Sisi wenye : kupendwa na Kristo. (bis)

Wimbo 26 — kipande 2

Alitufilia kama sadaka

Tukapokea upendo wake

Kwa kutuokoa katika giza

Alikubali fimbo za uhaki

Akafanywa : chukizo, laana. (bis

Wimbo 26 — kipande 3

Twakuabudu sadaka ya toleo

Wewe ulitununua sisi

Tukumbushapo kifo, mateso

Tunangoja siku yakuonekana

Mbinguni : kama bibi arusi. (bis)

Wimbo 26 — kipande 4

Tunasherekea kwa meza hii

Pendo la Kondoo uliyechinjwa

Kwako roho zetu zinalindwa

Zikionja salama na uheri

Na kwa bei ulivinunua : ulivinunua. (bis)

27.                  Wimbo 27

Wimbo 27 — kipande 1

Mbele ya kiti cha neema

Twakuabudu Mungu wetu

Tukiingia patakatifu

Kwa njia ya Yesu Kristo.

Wimbo 27 — kipande 2

Mkate wa juu ushibishao

Ni chakula chetu kweli

Ndani ya Yesu tumepewa

Uzima unaodumu.

Wimbo 27 — kipande 3

Pa’li pa kikombe  kikali

Ulichomunywesha, Mungu

Mwokozi mwema na mupole

Ametupa cha wokovu.

Wimbo 27 — kipande 4

Kwa sauti ya malaika

Tukinyakuliwa juu

Tutamuimbia sifa zake

Tutamuona… siku nzuri !

28.                  Wimbo 28

Wimbo 28 — kipande 1

Ukitutazama Mungu,

Tunazunguka meza hii,

Twafurahi kuwa kando,

Kutukuza neema yako.

Pendo lako ni uheri ;

Linafukuza woga kwetu

Na chini ya ukingo huu,

Mwokozi, hazina yetu.

Wimbo 28 — kipande 2

Tumesafishwa kwa damu

Yesu, hatuna tena taka ;

Tulikuwa wapotevu,

Twafichama kifuani mwako

Hatutanyanganywa kwako

Hatutatikisika kamwe

Kwani tuna tumaini kuu

Pendo lako ni imara.

Wimbo 28 — kipande 3

Kwa wakombolewa wako,

Ni kutamu kukukumbuka !

Tunakumbusha pamoja

Mateso na ushindi wako

Mukombozi, pendo lako,

Ambalo tuna uarabuni,

Linadumu mioyoni mwetu,

Hadi utakaporudi !

29.                  Wimbo 29

Wimbo 29 — kipande 1

Neema ya mbingu ! hazina ishangazayo !

Tunajua Yesu na mkono wa mapendo.

Alitukamata kutoka zambini

Aleteye Mungu – waabudu wa kweli. (bis)

Wimbo 29 — kipande 2

Mungu Mtakatifu aliona haki

Ndani ya Adamu wa pili akimtukuza :

Ni mupendwa wake, anayemutaka,

Kwa sheria yake – alimupendeza. (bis)

Wimbo 29 — kipande 3

Mungu ulimtoa katika mapendo yako

Aliitimiza yote kwa kutukomboa :

Yesu, haki yetu, utakatifu wetu,

Tumepata kuishi – milele kwa yeye. (bis)

Wimbo 29 — kipande 4

Fumbo ya milele isiyoeleweka !

Ulituchagua katika neema yako ;

Na sasa ; ee Mungu, Roho wako daima,

Atufunulia – Mwana wa mapendo. (bis)

30.                  Wimbo 30

Wimbo 30 — kipande 1

Yesu sadaka ya Mungu

Ulishuka duniani

Ukafunga ile shimo

Itutengayo naye.

Wimbo 30 — kipande 2

Ukavaa mwili wa mutu

Ukateswa kabisa ;

Kwa Kuokoa kiumbe

Ukapata uchungu.

Wimbo 30 — kipande 3

Ni wewe hekima yetu

Uhai na salama

Kimbilio kwa mateso

Wokovu wa milele.

Wimbo 30 — kipande 4

Ee Mwokozi mwaminifu

Twabaki ndani yako

Hadi uzima milele

Waishi tutaishi.

31.                  Wimbo 31

Wimbo 31 — kipande 1

Kwa kutuokoa, Bwana wa uzima

Alisumbuliwa na kuaibiwa

Sifa kwake  Mwana

Sifa kwako Kondoo

Pokea mioyo yetu, mshahara wako

Ulioupewa, kwa mlima kalvari.

Wimbo 31 — kipande 2

Kifo chako Yesu, kikaosha zambi

Ukafunga shimo kwa miguu yetu

Sifa kwake Mwana

Sifa kwako Kondoo

Twakusifu Bwana, ulitupa amani

Heri, ukombozi kwa mateso yako.

Wimbo 31 — kipande 3

Kututajirisha, mwenyewe mbinguni

Ukawa  maskini, wewe Mungu  mkubwa

Sfa kwake Mwana

Sifa kwako Kondoo

Pokea mapendo na heshima zetu

Viwe kwako Mungu pasipo mwengine.

Wimbo 31 — kipande 4

Mema ya pendo lako Mchungaji wetu

Unatuandalia meza kila siku

Sifa kwake Mwana

Sifa kwako Kondoo

Wapendwa wako Bwana wanafurahi

Wakionja pendo na matunzo yako.

Wimbo 31 — kipande 5

Kwa amani twafwata uriti wetu

Wewe ni sehemu yetu kwa milele

Sifa kwake Mwana

Sifa kwako Kondoo

Mukombozi Mungu, unayetupenda

Upewe nguvu, ufalme na heshima.

Wimbo 31 — kipande 6

Milele na milele tutakusifu

Pendo lako kubwa na ushindi wako

Sifa kwake Mwana

Sifa kwako Kondoo

Pokea mioyo yetu, mshahara wako

Ulioupewa, kwa mlima kalvari.

32.                  Wimbo 32

Wimbo 32 — kipande 1

Nani atatukuza, nani atatambua,

Pendo lililokushusha toka mbinguni

Kwenda Getsemane,...Golgota ya damu

Pale ulipochomwa mkuki na Mungu.

Wimbo 32 — kipande 2

Siyo wale, Bwana, majeshi wa mbinguni,

Ama vile vyote ambavyo uliumba

Ama urefu wa bahari na mbingu,

Vitakavyotukuza upendo wako.

Wimbo 32 — kipande 3

Yesu ! Pendo lako na neema yako nzuri,

Nani atavikuza ? ni sisi waovu tu

Uliofanya wafalme, makuhani,

Kwa ajili yao ulionja kifo.

Wimbo 32 — kipande 4

Wakombolewa tu, kwa raha takatifu,

Wataimba wema wako na kubariki.

Uliwanunua, Ee Yesu, kwa damu

Watakuwa nawe milele mbinguni.

33.                  Wimbo 33

Wimbo 33 — kipande 1

Twakuona ukiangaika

Ukinywa kikombe kile

Tunakuona ukijitoa

Mtakatifu kwetu waovu.

Wimbo 33 — kipande 2

Kifo chako sadaka safi

Tukitazame daima

Damu yako ilituosha,

Ikatufungulia mbingu.

Wimbo 33 — kipande 3

Pendo lako ni kubwa Kristo

Linagusa mioyo  zetu

Ulifilia ulimwengu

Wewe ndiye Mwokozi wetu.

34.                  Wimbo 34

Wimbo 34 — kipande 1

Wewe uliyetuandalia nafasi

Tukiwa na wewe, tutaishi hapo,

Twataka tukuza haki na neema yako,

Pendo la Mwokozi, pendo lako nzuri. (bis)

Wimbo 34 — kipande 2

Ee Bwana ! twakuja mbele yako kabisa

Kuonja utamu, ushirika wako ;

Hata hapa chini, wewe huonekane…

Tunangojea siku ya mukutano. (bis)

Wimbo 34 — kipande 3

Ni wakati halisi kwa kanisa lako,

Utaliingiza juu mbinguni kwako !

Kwa salama yako, litaijaa sifa

Kwa karamu hiyo, pahali pa mbingu. (bis)

Wimbo 34 — kipande 4

Tungojapo, Bwana, twatumia duniani

Chakula hiki, cha mapendo unayo,

Twatangaza humo neema iokoayo,

Mateso na kifo pia kurudi kwako. (bis)

35.                  Wimbo 35

Wimbo 35 — kipande 1

Kama Kondoo ulikufa, Yesu

Kwa zambi zetu, Mukombozi wetu

Pendo gani ? ni pendo la ajabu

Kwa kutuokoa, Yesu ukafa.

Wimbo 35 — kipande 2

Kwa ule wakati zambi zetu

Zilikuletea azabu kali

Kwa kufa ukavunja minyororo

Ukatuletea neema, raha.

Wimbo 35 — kipande 3

Amen ! Bwana ! Uwezo na sifa

Kwako heshima, hekima, ufalme

Tangu sasa tunasema na wewe :

Ubarikiwe Ee Mukombozi.

36.                  Wimbo 36

Mwana Kondoo uliteswa

Ukachukua taabu yetu

Na ukatufanya kwa Baba

Wafalme na makuhani

Pamoja tunakuheshimu

Twakusifu na kukuinua

Nguvu, ufalme pia kutii

Mioyoni tunakuabudu

Amen ! Amen ! Bwana ! Amen.

37.                  Wimbo 37

Ewe Kondoo takatifu

Uliacha sifa za mbingu

Kapokea taji ya miiba

Ukatukomboa sisi

Tunaimba wakati huu

Wimbo huu bora wa ushindi

Ee mbele ya kiti cha sifa

Tutaimba pendo lako

Kuja, Bwana, Amen ! Amen.

38.                  Wimbo 38

Wimbo 38 — kipande 1

Upendo wa ajabu (bis)

Kunyenyekea sana

Mwana akachukua mwili

Kakubali laana (bis)

Na akasulubiwa

Kuokoa kiumbe chake.

Wimbo 38 — kipande 2

Kristo Mwana wa Mungu (bis)

Aliyetufilia

Kafufuka kwa uwezo

Tutukuze ushindi (bis)

Ushindi wake Yesu :

Ni sifa na tumaini.

Wimbo 38 — kipande 3

Yesu ametukomboa (bis)

Ndani yake tu hai

Tumuimbie kwa furaha

Bwana katika mbingu (bis)

Unaketi mushindi :

Sifa kwako kwa milele !

39.                  Wimbo 39

Wimbo 39 — kipande 1

Twakuona utukufuni

Ee Mwokozi !

Tukionja ushindi wako

Mwenye nguvu

Milele pamoja na Mungu

Kwa kuume kwa Baba Mungu

Uliyeshuka duniani

Na upole.

Wimbo 39 — kipande 2

Kwa sisi ukawa laana

Ee Mwokozi !

Ukateswa zaidi sana

Ee Mwokozi !

Damu ’katoka mbavu zako

Ukatuondolea zambi

Kwa kufa kwako tunaishi

Ee Mwokozi.

Wimbo 39 — kipande 3

Tunakungoja toka mbingu

Ee Mwokozi !

Ulisema waja kututwaa

Yesu mweza !

Furaha isiyo na mwisho

Yakutazama sura yako

Na vile yakukufanana

Ee Mwokozi.

40.                  Wimbo 40

Yesu, neema, damu yako

Na musalaba wako

Kungaa kwa uso wako

Vyatupatia haki

Nafsi yetu yapumzika

Ndani yako Mwokozi

Wewe mwanzo na chemchemu

Ya uheri milele.

41.                  Wimbo 41

Wimbo 41 — kipande 1

Mwokozi Mupendwa, ni wewe tumaini !

Ulitukomboa kutoka mauti :

Aleluya ! Aleluya ! (bis)

Kati pendo lako (ter)

tumefurahi kweli.

Wimbo 41 — kipande 2

Umetusafisha toka zambi kwa damu,

Sifa ya mbinguni itatupokea

Aleluya !Aleluya ! (bis)

Tuna tumaini (ter)

kutoka kwa imani

42.                  Wimbo 42

Wimbo 42 — kipande 1

Katupenda mpaka kufa

Mwokozi wa mapendo

‘Katushindia shetani

Hadi kwa ngome yake. (bis)

Wimbo 42 — kipande 2

Namna vilikulemea

Pekee kwa saa ya giza

Kuachwa pia na hofu

Ya zambi zetu nyingi. (bis)

Wimbo 42 — kipande 3

Sasa fujo ya mawimbi

Yaliyokufikia

‘katuletea pumziko

Ya kazi yako nzuri. (bis)

Wimbo 42 — kipande 4

Kando yako wateule

Wako hapa duniani

Sasa wanaonja raha

Ya nyumba yake Baba. (bis)

43.                  Wimbo 43

Wimbo 43 — kipande 1

Kondoo wa Mungu Kristo akafa

Mutini (bis)

Pazia pale ’kapasuka

Kwa muti (bis)

Kwa patakatifu sana,

Mbele ya Mungu twafika

Kwako Yesu uliyejitoa

Mutini (bis)

Wimbo 43 — kipande 2

Uliinuliwa toka chini

Mutini (bis)

Ulikunywa kikombe chetu

Mutini (bis)

Kwa pendo ‘kakimaliza

Damu yako ilituosha

Tumeokoka kwa milele

Kwa muti (bis)

Wimbo 43 — kipande 3

Hayani sifa zako ‘kangaa

Mutini (bis)

Yesu uliupata ushindi

Mutini (bis)

Milele upewe  nguvu,

Heshima na sifa nyingi

Kwa sababu ulishinda

Mutini (bis)

44.                  Wimbo 44

Wimbo 44 — kipande 1

Nyimbo za mbinguni

Ni nzuri sana

Vinanda na nyimbo

Jaeni mbingu

Kwa nafasi kubwa,

ule wimbo mpya

Daima waanza

Kando ya Kondoo.

Wimbo 44 — kipande 2

Kwa kiti cha enzi

Tutakuona

Ukivikwa taji

Za kila aina

Na mikono yako

Inaonyesha

Ginsi uliteswa

Kwa musalaba

Wimbo 44 — kipande 3

Neema ya milele !

Uliye chinjwa

Ukajitolea,

‘Kamwanga damu

Kwa patakatifu,

Uheshimiwe

Mungu Baba yako

Aabudiwe.

Wimbo 44 — kipande 4

Nyimbo za mbinguni

Ni nzuri sana

Vinanda na nyimbo,

Vyajaa mbingu

Heshima na nguvu,

Kuzo milele

Kwa Mungu mushindi,

Na Kondoo wake.

45.                  Wimbo 45

Wimbo 45 — kipande 1

Mwana wa Mungu, wa ajabu

Waonekana usoni

Upendo muzuri wa Baba

Hata sifa zake nyingi

Washika dunia mkononi

Uliitosha utupuni

Vyote vinaimba Hekima,

Na kuzo lako Muweza.

Wimbo 45 — kipande 2

Mbele ya Baba kifuani

Wamupendeza daima

Mupo mumoja uwezoni

Mupo mumoja pendoni

Ulipenda, siri ya ajabu

Kutoka patakatifu

Kuja dunia yenye zambi

Ili ufe Mwana Kondoo.

Wimbo 45 — kipande 3

Upendo, neema ya ajabu

Twakuona Mutu, Mungu

Kwa sanduku hadi kalvari

Ukifwata njia chungu

Mugeni, ulikataliwa

Hata na walio wako

Ukanywa kikombe kichungu

Shambani mwa Getsemane.

Wimbo 45 — kipande 4

Ukabeba, Mwana Kondoo

Kwa saa za giza mutini

Hukumu ya makosa yetu

Pia gazabu ya Mungu

Ee Bwana tutakutukuza

Milele kule mbinguni,

Na roho zetu zitaimba

Pendo lishindalo kifo.

46.                  Wimbo 46

Wimbo 46 — kipande 1

Pendo safi, kubwa, lake Mungu mukuu,

Kwakujifunua katoa Mwana wake

Duniani humu, gizani mwa zambi

Sisi tulikuona na tukakugusa.

Wimbo 46 — kipande 2

Ulingaa kwa muti kwa saa tatu za giza

Zilizo funika dunia ya upofu

Mtu Mukamilifu Mwana Mtakatifu

Kaona kuachwa, hasira, mauti.

Wimbo 46 — kipande 3

Ukateswa Yesu, Mwokozi na sadaka

Jicho lako kaona ile shimo ndefu

Wewe wa milele ukabeba mzigo

Uliokuwa juu yetu milele.

Wimbo 46 — kipande 4

Kasema « imekwisha » na akatoa roho

Na pazia ya hekalu ikapasuka

Safi twaingia mbele yake Baba

Katika mwangaza wa uso wa Mungu.

Wimbo 46 — kipande 5

Kwa pendo la juu ushindi wa kifalme

Musalaba wako wamutukuza Baba

Na watuokoa, wajaza vinywani

Mwetu na wimbo wa waabudu wa kweli.

47.                  Wimbo 47

Wimbo 47 — kipande 1

Mwana wa milele, wa pekee wa Baba

Unamufurahisha Baba pale juu

Mbele ya nyakati ulipenda dunia

Ulimokuja na kujishusha vile.

Wimbo 47 — kipande 2

Ulifurahiya kukaa na wanadamu

Mungu akakuumbia mwili ukakuja

Munyenyekevu ukazaliwa chini

Siri ishangiliwayo na malaika.

Wimbo 47 — kipande 3

Uliye tazama kwa ndani taabu yetu

Tulipokuwa kati ile shimo kubwa

Ukatuponyesha Mwokozi wa ajabu

Damu yako kamwangwa na kutuosha.

Wimbo 47 — kipande 4

Kristo uliye hai tunaimba ushindi

Mungu alikuvika nguvu na heshima

Ukaja kututafuta tuone sifa

Tuwe nawe milele katika heri.

Wimbo 47 — kipande 5

Kondoo mutukufu, Mwokozi wa mapendo

Uliyetupenda na pendo la milele

Tunakuzunguka tukijaa furaha

Tunakuabudu, barikiwa milele !

48.                  Wimbo 48

Wimbo 48 — kipande 1

Wewe unayetupenda,

Mungu wa pendo, neema !

Twaingia hata mbingu

Kukuabudu siku hii.

Jamaa yako yakutana,

Ee Baba mbele yako ;

Ndani ya Yesu kanisa

Uliliweka kando kwako.

Wimbo 48 — kipande 2

Sifa gani kwa watoto

Kukutazama Mungu,

Na kuuimba ushindi

Wa Yesu aliyekufa !

Jamaa yako yakutana,

Ee Baba mbele yako ;

Ndani ya Yesu kanisa

Uliliweka kando kwako.

Wimbo 48 — kipande 3

Neema gani Baba Mpendwa,

Kujua pendo lako,

Tukingoja duniani

Kurudi kwa mwanawe !

Anakuja : heri gani !

Kanisa lake imba

Punde utamufanana

Mukombozi na Muweza.

49.                  Wimbo 49

Wimbo 49 — kipande 1

Kukupenda, kukujua

Na kupumzishwa nawe

Wewe rafiki na Bwana

Na kinywaji na mkate

Kuonja neema yako

Ya kifo chako Bwana

Twaonja utakatifu

Utamu gani kwetu.

Wimbo 49 — kipande 2

Heri itushangazayo:

Wewe kuwa mchungaji

Msaada wetu kila siku

Na haubadiliki

Katika upendo wako

Ukashuka duniani

Kutafuta kondoo zako

Na kuzikumbatia.

Wimbo 49 — kipande 3

Watujaza neema yako

Watujua kwa jina

Watuongoza njiani mwako

Tukienda  mbinguni

Kwa unyonge na makosa

Wewe ni msaada wetu

Unataka kwa upendo

Kutusamehe sisi.

50.                  Wimbo 50

Wimbo 50 — kipande 1

Yesu rafiki yetu mkubwa

Pendo gani !

Atupenda kushinda ndugu

Pendo gani !

Jamaa, rafiki, wanapita

Heri yaja na kutoweka

Moyo wake tu hauchoke

Pendo gani

Wimbo 50 — kipande 2

Yu uzima wetu milele

Pendo gani!

Na kwa milele tutukuze

Kazi yake !

Kwa damu yake tumeoshwa

Alipotukuta jangwani

Kwa neema akatuokoa

Pendo gani !

Wimbo 50 — kipande 3

Alijitoa kama zabihu

Pendo gani!

Anapenda kutubariki

Pendo gani!

Nafsi yetu imusikie

Kwa amani, kamwe, isiogope

Iishi karibu na Yeye

Kwa upendo.

 

51.                  Wimbo 51

Wimbo 51 — kipande 1

 

52.                  Wimbo 52

Wimbo 52 — kipande 1

 

53.                  Wimbo 53

Wimbo 53 — kipande 1

 

54.                  Wimbo 54

Wimbo 54 — kipande 1

 

55.                  Wimbo 55

Wimbo 55 — kipande 1

 

56.                  Wimbo 56

Wimbo 56 — kipande 1

Tayari kwetu pambazuko

Ya uheri usiokoma

Bwana kwa wakati kidogo

Tutakumbatiwa nawe. (bis)

Wimbo 56 — kipande 2

Wakati utukimbizapo,

Tunakutumainia,

Punde taabu itakwisha,

Wewe ni pumziko letu. (bis)

Wimbo 56 — kipande 3

Sifa nzuri kuzoni mwako

Utaonekana kwetu’,

Na Kwa kelele ya ushindi,

Yesu utatutwaa kwako. (bis)

 

57.                  Wimbo 57

Wimbo 57 — kipande 1

Bwana Yesu, mwenye mapendo kubwa

Wewe, kungaa kwa sifa za Mungu

Uje Bwana! Tuone uzuri wako

Twakungoja, tukitazama juu.

Wimbo 57 — kipande 2

Katuokoa, sisi ni kazi yako

Mbinguni tutakutumikia

Tutakuona, na kufanana nawe

Na milele tutakuabudu.

Wimbo 57 — kipande 3

Aleluya, ni raha takatifu!

Arusi ya Mwana kondoo yaja

Kando yako tutaimba milele,

Ee mupendwa, ule wimbo mupya.

 

58.                  Wimbo 58

Wimbo 58 — kipande 1

 

59.                  Wimbo 59

Wimbo 59 — kipande 1

 

60.                  Wimbo 60

Wimbo 60 — kipande 1

Yesu ! jina lako kwa nafsi aminifu,

Ni kubwa na nzuri !

Linatukumbusha pendo na neema yako,

Wokovu muzuri ! (bis)

Wimbo 60 — kipande 2

Mwana wa aliye juu, wewe mpendwa wa Baba,

Sifa ya mbinguni !

Ulituletea, katika nuru yako,

Zawadi za Bwana. (bis)

Wimbo 60 — kipande 3

Kwa wenye zambi, watoto wenye hatia

Wastahilio kufa,

Ulileta mema yapitayo fahamu

Na amani ya Mungu. (bis)

Wimbo 60 — kipande 4

Nafsi zetu zimekuwa zako Mkombozi :

Tupo mali yako

Zaa ndani yetu moto wa pendo lako,

Tuishi kwa imani. (bis)

61.                  Wimbo 61

Wimbo 61 — kipande 1

Utukumbatie, ee Mwokozi wa nafsi !

Utupe salama

Tuongezeye moto wa uhodari wema

Tuongoze milele. (bis)

Wimbo 61 — kipande 2

Pendekezo letu ni kukukaribia,

Wewe Emanueli !

Pendo lako kwetu, chemchemu ya uzima,

Kweli ni daima. (bis)

Wimbo 61 — kipande 3

Tukuzwa, Mwokozi ! pendo lako aminifu

Halibadiliki ;

Ulitupumzisha chini ya bawa lako,

Kwa milele yote. (bis)

62.                  Wimbo 62

Wimbo 62 — kipande 1

Mbinguni tuna Baba mwema na mupendwa,

Aliyetoa agizo zamani :

Mungu mwenye nguvu ni tumaini letu,

Akiwa juu akinga watoto. (bis)

Wimbo 62 — kipande 2

Alitupatia uzima wa mwanae

Akituokoa kwa damu yake

Alitutayarishia sifa milele,

Yesu pekee ni njia ya mbingu. (bis)

Wimbo 62 — kipande 3

Hekima, neema na ufalme vyaambatana

Kutuongoza pahali pa heri

Matunzo yako kwetu Mungu yanadumu;

Usiku, mchana watutazama. (bis)

Wimbo 62 — kipande 4

Musaada, nguvu kwa siku ya jaribu

Neema, msamaha, tegemeo,

Vyatoka kati roho yako kama muto

Usiyokoma na kukauka. (bis)

Wimbo 62 — kipande 5

Kwa pendo kubwa hii, tukupe nini Baba ?

Utupe mioyo ya utiifu

Nyuso zetu ziangaze tabia yako

Roho wako apambayo wako. (bis)

63.                  Wimbo 63

Wimbo 63 — kipande 1

Zizini mwa Yesu tule kwa uhakika

Tuonje neema kubwa ya mchungaji mukubwa

Tunywe maji yale yatiririkayo

Kutoka kiti kile cha pendo lake.

Wimbo 63 — kipande 2

Tupumzike katika zizi yake nono;

Hatutaogopa hata zoruba kubwa;

Yesu ni kwa upande wetu daima :

Tubaki daima kando ya mchungaji.

Wimbo 63 — kipande 3

kwa ajili yetu roho yake yawaka ;

Katika unyonge aonyesha fazili,

Unyonge wetu njoo uhodari wetu ;

Amtegemeaye anaweza yote.

64.                  Wimbo 64

Wimbo 64 — kipande 1

Kazi ya milele, tutakapo pumzika

Bila mwishowako watakuabudu

Wakitupa taji juu ya miguu yako

Wakistaajabu na watainama. (bis)

Wimbo 64 — kipande 2

Tutautazama uso wa Muabudiwa,

Uzuri wa Mwokozi, Bwana Arusi

Na tutavumbua fumbo isiyopimwa

Ya neema na mapendo bila mpaka. (bis)

Wimbo 64 — kipande 3

Kwako pekee Yesu, kwa nuru yako nzuri

Wewe jua la haki liangazalo

Kanisa litavaakatika utukufu

Nuru safi ya ukamlifu wako. (bis)

Wimbo 64 — kipande 4

Utaona pekee lile unalotaka !

Tunda kamili la kazi ya msalaba

Utafurahia kazi ya nafsi yako

Mapendo yako Mungu yatatosheka. (bis)

65.                  Wimbo 65

Wimbo 65 — kipande 1

Ndiyo, raha kubwa sana,

Uheri hapa chini,

Ni kufuata Bwana Yesu,

Hatua kwa hatua

Wimbo 65 — kipande 2

kwa pendo atupendalo,

Hakuna kizuio ;

Alitununua kwake,

Ni wetu kwa milele

Wimbo 65 — kipande 3

Pendo lake aminifu

Halitatukosea :

Ni kisima cha milele

Ambacho kitadumu.

Wimbo 65 — kipande 4

Ikiwa anapendezwa

Tumupende kabisa,

Ni sababu yeye pekee

Hatabadili pendo.

66.                  Wimbo 66

Wimbo 66 — kipande 1

 

67.                  Wimbo 67

Wimbo 67 — kipande 1

Uliyevunja vifungo

Yesu Kristo Mwokozi !

Katika haya na taabu,

Watufariji sisi

Wimbo 67 — kipande 2

Kazi ya neema yako

Imetukamilisha;

Na tupo mshahara wako,

Yesu, Bwana arusi

Wimbo 67 — kipande 3

Ulituponyesha sisi ;

Nafsi yetu, daima,

Ikutumikie wewe,

Ikikufurahia.

 

68.                  Wimbo 68

Wimbo 68 — kipande 1

 

69.                  Wimbo 69

Wimbo 69 — kipande 1

 

70.                  Wimbo 70

Wimbo 70 — kipande 1

Twaishi kwako, chemchemu njema

Tufurahie nuru yako

Kukuona mbele ya Baba

Yesu, pumziko ya roho yetu.

Wimbo 70 — kipande 2

Mungu alitutolea Yesu

Na kwake akaleta amani

Akapendezwa na uhaki

Deni yetu kweli imelipwa.

Wimbo 70 — kipande 3

Tuna heri, Bwana wema wako

Umetufungulia mbingu

Na mukristo kwa utulivu

Aingia kwani ameokoka.

Wimbo 70 — kipande 4

Kwa nini tusikupende Yesu ?

Uliyejitolea kwetu

Wewe ambaye pendo lako

Laja kila siku mbele yetu.

71.                  Wimbo 71

Wimbo 71 — kipande 1

 

72.                  Wimbo 72

Wimbo 72 — kipande 1

Watufunza, watufariji

Yesu ukiwa mbinguni

Kwani Roho na neno Lako

Vyabaki na wateule.

Wimbo 72 — kipande 2

Twasikia sauti yako

Kupitia neno Lako

Roho wako hufahamisha

Agusa moyo na macho.

Wimbo 72 — kipande 3

Kumbukumbu La pendo Lako

Lafikiawalio wako

Katika Jangwa watukuzwa

Twaonja mema ya mbingu.

Wimbo 72 — kipande 4

Hilini Neno La uzima,

Kama tunda La Eskoli

Linalotupatia nguvu

Jangwani tulikulapo.

Wimbo 72 — kipande 5

Muda kitambo kazi yake

Itakwisha kwa kundi hii

Tutakapo kuona nuruni

Tutazungumuza nawe.

 

73.                  Wimbo 73

Wimbo 73 — kipande 1

 

74.                  Wimbo 74

Wimbo 74 — kipande 1

 

75.                  Wimbo 75

Wimbo 75 — kipande 1

Tuimbe, wandugu, wema wa Baba wetu

Wema wa ajabu !

Jina lake nzuri liinuliwe popote

Na watakatifu ! (bis)

Wimbo 75 — kipande 2

Nani kuliko jamaa aliyochagua,

Atamutukuza ?

Malaika gani atasema vizuri

Mbele yake Mungu. (bis)

Wimbo 75 — kipande 3

Tutukuze yule anayetutakia

Kuzo ya juu sana

Utukuzwe Baba, heshima iwe kwako

Kwa mapendo yako ! (bis)

 

76.                  Wimbo 76

Wimbo 76 — kipande 1

Kwetu, wakristo, ni heri

Tutakapouona

Uso wa Yesu Mwokozi

Mbinguni juu ya vyote ! (bis)

Wimbo 76 — kipande 2

Kuwa nawe juu mbinguni,

Tukifanana nawe,

Tukitamka na waheri

Sifa zako milele. (bis)

Wimbo 76 — kipande 3

Kuwa nawe na kuonja

Uzuri, wema wako,

Wema wako raha yetu,

Furaha kubwa gani. (bis)

Wimbo 76 — kipande 4

Kwani kwako ni pumziko

Tunalotumaini,

Ni mwisho wa kazi zetu

Nyumbani mwake Baba. (bis)

Wimbo 76 — kipande 5

Tusikie Bwana arusi

Anayetuambia

“Ninaja!  Mufarijike,

Hakuna fazaiko” (bis)

Wimbo 76 — kipande 6

Bidii kwenu wasafiri!

Tunyanyuwe vichwa juu;

Haraka! Viuno vifungwe:

Wokovu ni karibu. (bis)

 

77.                  Wimbo 77

Wimbo 77 — kipande 1

 

78.                  Wimbo 78

Wimbo 78 — kipande 1

Yesu, Nguvu, Mwamba wangu

Mwokozi wangu mkuu

Adui hawataweza

Nikilindwa nawe.

Wimbo 78 — kipande 2

Kwa Neema ulinisamehe

Umenipa mbingu

Ninazungukwa na nguvu

Imani yatosha.

Wimbo 78 — kipande 3

Wewe ndiye Mukombozi

Na mwenye upendo

Wewe ni uheri, sifa

Na Mwokozi wangu.

79.                  Wimbo 79

Wimbo 79 — kipande 1

 

80.                  Wimbo 80

Wimbo 80 — kipande 1

Ndani yako, Yesu nakuja,

Kwake Mungu bila woga,

Mbele yake, bila taka yote

Nina kubaliwa kwake.

Wimbo 80 — kipande 2

Ndani yako, ninapumzika;

Ninajua uwema wako,

Moyo wako ni kimbilio

Damu yako ilininunua.

Wimbo 80 — kipande 3

Ndani yako, hakuna shaka

Jangwani nisijali,

Ulinipasulia njia,

Nalindwa na pendo lako.

Wimbo 80 — kipande 4

Niko nawe kifo kikija,

Ninangoja bila woga :

Ninaishi uzima wako,

Nitaishi sawa na wewe.

 

81.                  Wimbo 81

Wimbo 81 — kipande 1

Ni kwa Baba mwenye nuru

Kutokapo zawadi

Jibu maombi yangu,

Apenda kubariki.

Wimbo 81 — kipande 2

Baba mwenye kurehemu,

Msaada wangu saa zote ;

Neema yako inanipa

Kujua pendo lako.

Wimbo 81 — kipande 3

Pendo gani la ajabu

Nilipatalo kwako

Pendo lako kubwa sana,

Hazina ya mkosaji.

Wimbo 81 — kipande 4

Nyumbani patakatifu

Ninakukaribia

Niishi wala nikufe

Mbingu ni wazi kwangu.

Wimbo 81 — kipande 5

Sifa kwako, Baba Mungu

Kanipenda wa kwanza

Niko na samani kwako

Mimi ni mali yako.

82.                  Wimbo 82

Wimbo 82 — kipande 1

 

83.                  Wimbo 83

Wimbo 83 — kipande 1

Neno lako ni aminifu

Bwana halipite kamwe

Nafsi yangu iliaminiyo

Haitaogopa tena.

Wimbo 83 — kipande 2

Ninajuwaee wazo nzuri

Miongoni mwa kondoo zako

Hakutapotea yoyote

Mchungaji uliahidi.

Wimbo 83 — kipande 3

Wana wa pendo lako kubwa

Tupokifuani mwako

Hata dunia na kuzimu

Havitatutosha kwako.

 

84.                  Wimbo 84

Wimbo 84 — kipande 1

 

85.                  Wimbo 85

Wimbo 85 — kipande 1

Bwana wangu mwema

Uliniponya

Nipo mushahara

Kwa kazi yako

Nilikuwa mnyonge

Sasa ni wako

Neema yako nzuri

Kaniokowa.

Wimbo 85 — kipande 2

Chunga kwa rehema

Nafsi milele

Katika furaha

Na usalama

Unishike mkono,

Nisilegeye

Nichunge daima

Karibu nawe.

 

86.                  Wimbo 86

Wimbo 86 — kipande 1

 

87.                  Wimbo 87

Wimbo 87 — kipande 1

 

88.                  Wimbo 88

Wimbo 88 — kipande 1

 

89.                  Wimbo 89

Wimbo 89 — kipande 1

Ee Mwokozi, mapendo ya ajabu,

Ee Mchungaji, nijuaye sauti !

Kwa Kondoo, katika pendo lako,

Ulikubali kufungwa mtini.

Wimbo 89 — kipande 2

Nimechoka na kukosa bidii ?

Unionapo waniponya yote

Wanilisha na majani mabichi,

Wanitajirisha na zawadi.

Wimbo 89 — kipande 3

Nina kiu ? Kandokando ya maji,

Waniongoza kwa uaminifu ;

Ninapata ndani yako kisima,

Cha kuninywesha hadi milele.

Wimbo 89 — kipande 4

Wewe Yesu, nguvu ya nafsi yangu :

Kila saa naona pendo lako

Ulinitosha motoni milele,

Kunipeleka pahali pa juu.

Wimbo 89 — kipande 5

Msalaba, mauti na neema yako,

Ni uheri wa kondoo zako ;

Ee Mwokozi ! Timiza na tukuza

Nguvu zako 'zaifuni mwangu.

Wimbo 89 — kipande 6

Nitaimba sifa na mema yote

Ya wokovu na upendo wako

Ee Mwokozi ! U tumaini langu

Katika imani waniongoza.

 

90.                  Wimbo 90

Wimbo 90 — kipande 1

 

91.                  Wimbo 91

Wimbo 91 — kipande 1

Wakristo, tusifu na tukuze pamoja

Jina la Mkombozi !

Anatukusanya sisi wapendwa wake

Tutukuze Bwana. (bis)

Wimbo 91 — kipande 2

Malaika wa Bwana anatuzunguka

Watoto wa Mungu,

Anawakomboa na kuwachunga pia

Katika hatari. (bis)

Wimbo 91 — kipande 3

Tunaonja, Bwana, mbele ya uso wako,

Pendo lako la juu

Mutu wa uheri ni yule tu ambaye

Anakuamini ! (bis)

 

92.                  Wimbo 92

Wimbo 92 — kipande 1

Ni ndani ya Mungu

Kwa tumaini lote

Mioyo yapumzika

Uvumilivu wako,

Rehema yako kubwa

Vinanionyesha

Matunzo ya pendo.

Wimbo 92 — kipande 2

Ni kutamu kwangu !

Kuwa wewe ni Baba

Yu nami popote

Waniangazia neema

Wapokea maombi

Unanitazama,

Wanipa imani.

Wimbo 92 — kipande 3

Salama na pendo

Furaha kamilifu

Ni vyangu milele

Naona mbele yangu

Njia nzuri ya raha

Ni ya utukufu

Yaenda mbinguni.

Wimbo 92 — kipande 4

Bwana niongoze

Ukinishika mkono

Linda nyayo zangu

Mungu kwa pendo lako

Nguvu, hekima yako

Vinatuzunguka

Ni msaada wa nguvu.

 

93.                  Wimbo 93

Wimbo 93 — kipande 1

 

94.                  Wimbo 94

Wimbo 94 — kipande 1

Pendo kubwa na la milele

Lake Kristo

Damu yake ilimwangika

Kwami, muovu

Yaniokoa toka shida

Na kunipokonya mauti

Na kuchapa sura ya Yesu

Juu yangu.

Wimbo 94 — kipande 2

Anisimamishaye mimi ?

Yesu kristo

Ahimizaye nafsi yangu

Yesu kristo

Yesu alisema : ninaamini

Nipige vita kumtukuza,

Ngao na ushindi wangu ndiye :

Yesu kristo.

Wimbo 94 — kipande 3

Ninaenda kwa Baba yangu

Njia ni Yesu ;

Nina heri na raha tele

Kwake Kristo ;

Hata kama ndani ya ziki,

Moyo wangu una tumaini,

Ni kwa sababu niliamini

Yesu kristo.

Wimbo 94 — kipande 4

Ninafurahi ndani yake

Yesu Kristo ;

Duniani, mbinguni naishi

Kwake Yesu

Punde, kwaheri vya dunia !

Mbali na ninyi nina bawa,

Kwenda makao ya milele

Kwake Yesu.

 

95.                  Wimbo 95

Wimbo 95 — kipande 1

 

96.                  Wimbo 96

Wimbo 96 — kipande 1

Nikufikilipo Bwana

Pia neema yako

Moyo wangu wafurahi

Kwani utakuona. (bis)

Wimbo 96 — kipande 2

Hata kama ninachoka

Ninasonga mbele tu

Kama mahali pakavu

Kunakoota miiba. (bis)

Wimbo 96 — kipande 3

Hata adui ni wengi

Kwa kunishambulia

Kwa mitego ya hatari

Wanizunguka sana. (bis)

Wimbo 96 — kipande 4

Ninaweza kila siku

Kufuata njia yako

Na kwa pendo lako kubwa

Kuonja lifaalo. (bis)

Wimbo 96 — kipande 5

Bwana, pumziko na Mwamba

Wokovu, haki yangu

Wanikaribia mimi

Wanipendeza mimi. (bis)

Wimbo 96 — kipande 6

Yesu, Mukombozi wangu

Nijaze uhodari

Wezesha mtumishi wako

Akuwe mwaminifu. (bis)

Wimbo 96 — kipande 7

Hadi siku wateule

Washindi ndani yako

Wakivaa kanzu nyeupe

Watakuona kuzoni. (bis)

97.                  Wimbo 97

Wimbo 97 — kipande 1

Katika uzaifu

Tunaona juu

Na Mungu wa mapendo

Atulinda sisi

Hadi patakatifu

Njia iko wazi

Kwetu sisi ni Baba

Mungu wa salama.

Wimbo 97 — kipande 2

Na katika mateso

Tunaona juu

Ambapo Yesu Kristo

Atashuka punde,

Mwokozi mwaminifu

Atatunyakua

Kanisa lakuita

Bwana Yesu kuja.

Wimbo 97 — kipande 3

Tukuzwa Baba wetu !

Tukuzwa Kondoo !

Hakuna tena taabu

Tukitazama juu

Tupatie bidii,

Imani na pendo ;

Nafsi yetu ingoje

Kurudia kwako.

98.                  Wimbo 98

Wimbo 98 — kipande 1

Mungu twakuabudu, uliye mukarimu,

Tukiwa gizani ulituangazia

Pendo lako kwetu,

Lilijaa mioyoni

Usalama wako, zawadi ya neema.

Wimbo 98 — kipande 2

Radi za torati zilizima kabisa,

Mwana wako alipobeba upotevu

Na watoto wako,

Ni wenye ushindi,

Kwa mabaya mengi neema imelipa.

Wimbo 98 — kipande 3

Pendo lako Bwana, linatufungulia,

Msaada wa Roho, hazina ya salama ;

Na kwa mema yako

Tumeshirikishwa

Kwa uvuli wako unatuficha sisi.

Wimbo 98 — kipande 4

Tukifwata njia, utuongoze ee Yesu,

Na tupewe kungoja kurudi kwako

Tu wapendwa wako,

Twaenda mbinguni

Ambako jina zetu zimeandikiwa.

99.                  Wimbo 99

Wimbo 99 — kipande 1

Sifa kwake Bwana, Mungu na Baba wetu

Anayetujaza mema kila siku

Atupenda sana kuliko mama mpenzi :

Pendo lake halilinganishwe kamwe.

Wimbo 99 — kipande 2

Uliutangaza huu upendo bora

Ee Mungu wa pendo ! kwa zawadi nzuri

Ya Mwokozi wetu, Yesu, mwana wa pekee

Aliyesulubiwa tuhurumiwe.

Wimbo 99 — kipande 3

Watujaza pendo, Mungu mwema, mhekima,

Mioyoni kwa Roho wako tulipewa ;

Yeye ni ndani yetu akishuhudia

Neema kwa Yesu iliyoturehemu.

Wimbo 99 — kipande 4

Katika pendo hii, Mwokozi mwaminifu,

Utuchunge hadi utakaporudi

Utupe uhodari tuombe na tungoje

Wewe na tubaki katika pendo lako.

100.             Wimbo 100

Tumutazamie Yesu,

Bado kitambo Mwokozi

Atarudi toka mbingu,

Katika kungoja kwa heri

Nafsi zetu ziwe tayari

Tuwe macho, tusilale

Wakristo, Mwokozi aja.

101.             Wimbo 101

Wimbo 101 — kipande 1

Mungu anatupenda

Na tufurahi !

Tunakumbatiwa

Na pendo lake !

 

Refrain :Tumusifu Yeye,

Tuonje mema

Tuimbe ushindi

Wa Mukombozi.

Wimbo 101 — kipande 2

Ee Mungu  Muweza !

Ona hitaji,

Wewe ndiwe Baba,

Unatujali.

Wimbo 101 — kipande 3

Katika safari

Watufuata ;

Unatupa moyo !

Tunapochoka.

Wimbo 101 — kipande 4

Roho wa neema

Atuhimiza,

Atuonyesha wewe,

Mwokozi wetu !

Wimbo 101 — kipande 5

Tumaini letu,

Mungu wa pendo !

Tumaini letu

Ni wema wako

Tumusifu yeye, etc.

102.             Wimbo 102

Wimbo 102 — kipande 1

Tuende mbele kwa furaha tele,

Katika nyumba ya wenye heri,

Ambapo Yesu anatuombea,

Tuende mbele ndiyo inchi yetu

Tuende mbele tukifurahi

Katika nyumba ya wenye heri.

Wimbo 102 — kipande 2

Nyimbo za pendo zitaimbwa juu ;

Nyimbo tamu za walio na heri !

Na tutashiriki kwa nyimbo hizo

Tutakapofika nyumbani mwetu

Tuende mbele kwa furaha tele

Katika nyumba ya wenye heri.

Wimbo 102 — kipande 3

Toka mbingu twakungoja, Bwana,

Kwani sisi tupo mali yako.

“Kuja, Yesu” kanisa linaita ;

“Tupokee utukufuni mwako”

Pale tutafurahi daima :

Ndani ya nyumba ya wenye heri.

Wimbo 102 — kipande 4

Heri, punde katika inchi mpya,

Tutaimba sifa zake Kondoo ;

Hakutakua msiba na kulia,

Wala zambi kwa fasi nzuri hiyo ;

Raha tele pamoja na Yesu,

Pendoni mwake tutafurahi !

103.             Wimbo 103

Wimbo 103 — kipande 1

Kamwe Mungu haache

Amtumainiye ;

Dunia ikinitesa,

Nina tegemeo.

Na huyu Mungu Mwema

Anachunga wake

Anawapa uzima,

Anawapa mema.

Wimbo 103 — kipande 2

Najua ananipenda,

Nataka anitunze :

Vema kuliko mimi,

Ajua hitaji

Huyu Mungu wa pendo

Hataniachilia

Sivyo, kama mabaya,

Yakija yu nami.

Wimbo 103 — kipande 3

Ee Mungu uso wako

Waangaza juu yangu,

Unipe neema yako

Niishi yote kwako.

Hadi siku yakuitwa

Kuingia kwako,

Unipe uaminifu

Wakukufuata.

104.             Wimbo 104

Wimbo 104 — kipande 1

Heri aliye na nia

Ya kumufwata Bwana !

Yesu anavuta

Kwa upole,

Yote yafwata Heri yake. (bis)

Wimbo 104 — kipande 2

Muchungaji amwitaye

Anamuweka huru.

Ni mwaminifu

Ampa nguvu,

Na bidii mupya Ampatia. (bis)

Wimbo 104 — kipande 3

Mkono wako wamukinga :

Anakutegemea.

Muovu akimtisha

Ila mbele

Mtego waanguka Mbele yako. (bis)

105.             Wimbo 105

Wimbo 105 — kipande 1

Heri aliye na nia

Ya kumufwata Bwana !

Yesu anavuta

Kwa upole,

Yote yafwata Heri yake. (bis)

Wimbo 105 — kipande 2

Muchungaji amwitaye

Anamuweka huru.

Ni mwaminifu

Ampa nguvu,

Na bidii mupya Ampatia. (bis)

Wimbo 105 — kipande 3

Mkono wako wamukinga :

Anakutegemea.

Muovu akimtisha

Ila mbele

Mtego waanguka Mbele yako. (bis)

106.             Wimbo 106

Wimbo 106 — kipande 1

Kamwe sitapungukiwa

Kwani Bwana ni Mchungaji

Ninaishi chini ya gongo

La asiyebadilika

Kweli Yesu ulinitia

Miongoni mwa kondoo zako.

Wimbo 106 — kipande 2

Ulinipa salama yako

Najua ulinipenda

Nikipita katika moto

Najua sitaungua

Macho yako ni juu yangu

Ongoza yangu juu yako.

Wimbo 106 — kipande 3

Bwana nikukaribiapo

Sioni woga yeyote

Neema yako ni mwamba mkubwa

Kimbilio haki kwangu

Ulinishika mkononi

Shetani hata nitosha.

107.             Wimbo 107

Wimbo 107 — kipande 1

Watoto wa Mungu tuishi

Tukiungwa katika pendo ;

Ni utayari wa milele

Wa wanao barikiwa.

Wimbo 107 — kipande 2

Tukiwa tumenyweshwa pale,

Tuwe na nia moja tu ;

Tuendelee safarini,

Tukitazama Mwokozi.

Wimbo 107 — kipande 3

Bwana uwashe moto wako

Utuongezee imani ;

Na kutokea mioyo yetu

Wimbo upande kwako juu !

108.             Wimbo 108

Tufurahi wakristo ; (bis)

Bado kitambo Yesu,

Ndani mwetu atatukuzwa

Bwana utarudia, (bis)

Tutakutana nawe

Na tutaishi ushindi.

109.             Wimbo 109

Wimbo 109 — kipande 1

Kanisa ni ligeni

Sasa hapa chini :

Ni fasi ya unyonge,

vita, machafuko.

Ila kwa mkono wake,

Yesu atalitwaa

Mbinguni kwa ushindi,

Daima atakaa. (bis)

 

Pumziko ni karibu ;

Vita vitakwisha

Tuinue vichwa juu ,

Kwani Yesu aja.

Yeye Mwana wa Mungu,

Mwokozi milele,

Tukivuka dunia

Twatazamia juu,

Twatazamia juu.

 

Giza linatoweka;

Ee ndugu tuamke:

Muda kitambo sasa

Tutaona Bwana.

Na kwa furaha nafsi

Imufurahie

Kwa Roho wa uzima

Tuite “njoo Bwana”. (bis)

110.             Wimbo 110

Wimbo 110 — kipande 1

Siku gani tutaona

Kanana ya mbinguni ?

Juu ya mbingu mwasikia ?

kristo anatuita.

Na tutaishi naye,

zoruba itakoma

Tutaimba kwa milele

wimbo wa salama.

 

Refrain : Heri kamilifu, Uheri, uheri

Heri kamilifu, Pumziko ni Bwana

Kanisa litakapokusanyika mbinguni

Litaimba bila mwisho :

Sifa kwake Kondoo.

Wimbo 110 — kipande 2

Wateule wataona,

utukufu wa Kristo

Wakiwa wamefufuka,

watamshuhudia

Wakisifu ushindi,

kazi ya musalaba

Pamoja kando ya kiti,

tutampa naziri.

Wimbo 110 — kipande 3

Kama kule juu mbinguni,

mwenye zambi akitubu,

Malaika kwa umoja,

wabariki Bwana

Itakuwa furaha,

wakati kundi lake

Litakapo kombolewa,

nakushinda vyote.

Wimbo 110 — kipande 4

Kanana ni fasi nzuri,

Ni inchi ya ahadi

Tukikusanywa na Mungu,

kwa upendo wake

Tutaimba milele

wimbo wa kufurahi

Utasikika mbinguni,

Milele daima.

Wimbo 110 — kipande 5

Siku hiyo ya milele,

itaangaa asubui

Sote katika umoja

Na mapendo pia

Na tutasema tena

Na yule Muabudiwa :

Mwana Kondoo astahili

nguvu na mamlaka

Heri kamilifu, uheri, uheri, etc.

 

111.             Wimbo 111

Wimbo 111 — kipande 1

Neema yako kubwa,

Mungu wa pendo,

Yapita maisha

Kwa waaminio.

 

Refrain : Watoto wa nuru,

Tusifu Baba

Anayetupenda

Yeye ni pendo.

Wimbo 111 — kipande 2

Neema yako Baba,

Kwa wateule,

Mbele yako wewe,

Na ndani ya Yesu

Wimbo 111 — kipande 3

Neema yako ya juu

Kwa wasafiri

Ni tamu kabisa,

Mioyoni mwetu.

Wimbo 111 — kipande 4

Duniani humu,

Mungu wa pendo,

Neema yafurika

Hadi kwa milele !

Watoto wa nuru, etc.

112.             Wimbo 112

Wimbo 112 — kipande 1

Kati wanyanganyi

Katika mateso

Alikufa

Mtakatifu pekee

Pale msalabani,

Alivunja nguvu

Ya muovu.

Wimbo 112 — kipande 2

Yesu alifufuka

Alipanda juu :

Tulimuona.

Yesu ni Kiongozi,

Anatuongoza

Ana nguvu kweli

Tunajua.

Wimbo 112 — kipande 3

Atatoka mbingu :

Na kutupeleka ;

Tuishi naye

Asema : « nakuja »

Tuchunge hazina

Tukeshe usiku

Tujiandae.

Wimbo 112 — kipande 4

Yesu hadi leo,

Mbingu, kao lako

Tufundishe

Tukinge vitani ;

Tuongoze kwa lengo

Rahani, kilioni

Utuongoze.

Wimbo 112 — kipande 5

Mungu, chunga wako ;

Wamimiye mema ;

Wahimize

Kukutumikia,

Na kukushukuru,

Wajingojee kwako,

Ni sheria.

Wimbo 112 — kipande 6

Kupenda, kuabudu,

Kutangaza pote

Mbele yake ;

Kumupenda Yesu,

Kutangaza mema,

Kufwata bendera,

Ni mapashwa.

 

113.             Wimbo 113

Wimbo 113 — kipande 1

Niwapo na fasi mbinguni

Hapa chini nina amani ya roho

Mbali ya mawimbi na zoruba

Niwezapo pumzisha kichwa

Kifuani mwa Mwokozi

Wimbo 113 — kipande 2

Juu nyumbani mwa Baba yangu

Ndani yako Yesu nina vyote

Vyote vya pa’li patakatifu

Bwana, uso wako, nuru yangu

Wanipa sifa na pendo.

 

114.             Wimbo 114

Wimbo 114 — kipande 1

Tunaweza kukufuata

Njiani mwako Yesu

Ulimopenda kuishi

Ukiwa mgeni kwetu

Ulikuwa pekee yako

Ukitenda mema tu

Katika njia hii nzuri

Yako mtu mkamilifu.

Wimbo 114 — kipande 2

Hiyo njia yafungua

Mema, mali ya pendo

Mungu mwenyewe atambua

Humo utakatifu

Hivi kwa neema yako

Twaweza kukufuata

Kwani ulituokoa.

Wabarikiwa wako.

Wimbo 114 — kipande 3

Mwili wetu ukiteswa

Sikitiko na taabu

Tunapoonja uchungu

Tukufuatapo, Yesu

Juu yako twatazamia

Katika uzaifu

Ili utuonyeshe

Utakatifu wako.

Wimbo 114 — kipande 4

Njia hii yaishia

Inchini penye sifa

Palipo uso wa Mungu

Na wa Mutu mushindi

Tukiwa wakamilifu

Kuzoni tutaabudu

Yesu tutakufanana

Tutashibishwa nawe.

 

115.             Wimbo 115

Wimbo 115 — kipande 1

Jangwani nifuatamo njia yangu

Kuelekea inchi ya kuishi,

Kusiwe kizuizo hata kazi

Kwani mbingu ni uriti wangu.

Wimbo 115 — kipande 2

Mwokozi ni Kiongozi, tumaini

Nichunge na hatari ya siku.

Uniangazie kwa usiku

Unichunge pendoni mwako.

Wimbo 115 — kipande 3

Kila asubui mapendo yako

Yanitumia kila siku mukate.

Jioni ninapolala salama

Wewe unahusika na kesho.

Wimbo 115 — kipande 4

Mwamba wangu ! Maji safi ya neema

Yatiririka kuniondolea kiu

Kwa Roho wako unichunge

Moyo wangu usinungunike.

Wimbo 115 — kipande 5

Hivi sasa mwisho wa njia yangu

Utaniletea pumuziko ;

ushuhuda hakika wa Bwana

Unanikinga na mawimbi.

Wimbo 115 — kipande 6

Inchi yangu, ee inchi ya ahadi

Moyo wangu sasa wakusalimu

Katika raha tele takatifu

Jina lako Mungu lisifiwe.

 

116.             Wimbo 116

Wimbo 116 — kipande 1

Bwana pekee, nguvu, uzima wangu :

Hakuna awezaye kunitisha

Uwezo wake mkubwa :ngao yangu

Mutu hawezi kunishitua.

Wimbo 116 — kipande 2

Hata kama kambi nzima ikuje,

Wajali na hiyo moyo wangu ?

Hata kama msaada ukikosa,

Nina Mwokozi mwenye uwezo.

Wimbo 116 — kipande 3

Kama mama mpenzi akiniacha,

Sitapata msaada kwa mutu,

Muweza, Baba na muaminifu,

Ataniokoa akishika mkono.

Wimbo 116 — kipande 4

Nafsi yangu, ukiwa matesoni

Ngoja kwa Mungu neema, msaada ;

Umutumainie pekee yake :

Mkono wake utakupa nguvu.

Wimbo 116 — kipande 5

Kristo ndiye salama na wokovu ;

Nguvu yangu Kiongozi wangu ;

Pendo lake litanipa ushindi :

Siogopi, Yesu yupo nami.

 

117.             Wimbo 117

Wimbo 117 — kipande 1

Ee Bwana pendo lako,

Ee Mchungaji Mwema,

Wanizunguka mimi,

Nakingwa zikini.

Wanibeba moyoni,

Nichokapo mimi ;

Mkono wako wa nguvu

Wanishika mimi.

Wimbo 117 — kipande 2

Mikono yako Bwana,

Ilitobolewa,

Iliumizwa na watu

Ulipotufia,

Na kwa mateso yale

Uyakumbukayo ;

Mikono ni tayari

Ili ibariki.

Wimbo 117 — kipande 3

Mufano wa kufwata,

Moyo wa Mwokozi,

Mwaminifu msaidia,

Mkamilifu kweli,

Mpole wa kufuata

Bila hata woga

Nataka kuishi nawe,

Uliyenifia.

 

118.             Wimbo 118

Wimbo 118 — kipande 1

Nani atatuhukumu

Sisi wachaguliwa ?

Nani atatushitaki,

Tuliopata haki ?

Mwana wa Baba,

Alifufuliwa,

Avikwa nuru,

Alipanda juu.

Tukiwa tunasumbuka

Anatusaidia,

Na tunashinda zaidi

Ndani ya atupendaye.

Wimbo 118 — kipande 2

Yesu alitukomboa

Toka kifo milele ;

Yeye ametufufua,

Anatuita mbinguni

Hakika tamu

Kuishi mbinguni !

Ni tumaini

Kwetu tuliopendwa !

Kwa mufalme wa milele,

Mkubwa, mwenye hekima,

Iwe heshima milele

Pendo, uwezo na sifa.

Wimbo 118 — kipande 3

Tutaona siku gani

Siku yakuonekana

Kwa atokaye mbinguni,

Yesu Kiongozi wetu ?

Na siku nzuri,

Ya mwisho wa kazi !

Imani nzuri,

Na pumziko tamu !

Wakristo kwa muda mfupi,

Bwana wa utukufu

Atakuja kuwalipa

Wapiganaji ushindi.

 

119.             Wimbo 119

Wimbo 119 — kipande 1

Kuokolewa kutoka inchi

Ya utumwa, zambi, giza

Tunatarajia uriti

Tukiongozwa na Roho.

Wimbo 119 — kipande 2

Huko hatutalia tena

Kazi, kiu vile njaa

Hakuna hatari, kilio

Ni amani, uheri tu.

Wimbo 119 — kipande 3

Milele pamoja na Kundi

Upendoni kwa furaha

Tutakusifu kwa milele

Kondoo uliyetufia.

 

120.             Wimbo 120

Wimbo 120 — kipande 1

Kujeni wapendwa, tuchote kwa furaha

Amani na neema kwa chemchemu

Tutangaze mema, tuinue upendo

Wa Mwokozi anayetuponya. (bis)

Wimbo 120 — kipande 2

Tutakutukuza, Bwana nyimboni mwetu

Tunaojua mapendo yako

Ulitutendea mambo mazuri sana

Tutakubariki siku zote. (bis)

Wimbo 120 — kipande 3

Twakuabudu Yesu, Mwokozi wa mapendo

Uliyetuokoa kwa damu

Twaimba upendo wako hapa duniani

Mbinguni tutauimba daima. (bis)

 

121.             Wimbo 121

Wimbo 121 — kipande 1

Furaha gani, tunyakuliwapo

Yesu akirudi

Na milele Kanisa litakwenda

Mbali ya dunia. (bis)

Wimbo 121 — kipande 2

Wakati mzuri, Kristo atatuleta

Karibu ya Baba

Tutakapotukuzwa mbele yake

Kristo atatuingiza. (bis)

Wimbo 121 — kipande 3

Kutasikika kule juu mbinguni

Nyimbo za heri tu

Wote watatangaza neema yake

Pendo la Mwokozi. (bis)

Wimbo 121 — kipande 4

Shuka mbinguni, tunakuhitaji

Twakupenda, kuja

Tangu zamani tunakungojea

Bwana arusi njoo. (bis)

 

122.             Wimbo 122

Wimbo 122 — kipande 1

Wateulewako

Katikavita,

Wakutapohapa

Unyongemwingi,

Mbinguniwabebwa

Moyonimwako

Eekuhaniwetu

Mukubwasana.

Wimbo 122 — kipande 2

Ukijaanawema

Napendopia

Hautamsahau

Mukombolewa

Niwewemsaada

Katikavita

Unatutetea

Mungu Mtetezi.

Wimbo 122 — kipande 3

Kwakilauchafu

Niwewepekee

Utusafishaye

Miguukwamaji

Wasema : mwamini

« Niigemimi

Mufanokamili

Mtumishimwema. »

Wimbo 122 — kipande 4

Tundalaushindi,

Wakombolewa,

Watakuwanawe

Kuzonimwako

Nyumbanimwa Baba

Usonimwake

Tumepewakazi :

Nipendolako.

 

123.             Wimbo 123

Wimbo 123 — kipande 1

Neema gani Bwana, kuitwa ndugu zako

Na kuwa na amani, tukikungojea

Ulitufungua kutoka shida zetu

Haki yetu, pendo lako. (bis)

Wimbo 123 — kipande 2

Ni wewe uliyetusafisha kwa damu

Na moiyoni mwetu, ukaleta amani,

Yesu, mkate wa juu, chakula cha mbinguni,

Kwako tupo wa milele. (bis)

 

124.             Wimbo 124

Wimbo 124 — kipande 1

Mshindi wa shetani na dunia

Bwana Yesu amefufuka

Na Kwa woga wa giza kubwa

Siku nzuri inafwata

Hakuna woga, ziki tena

Enyi taifa teule,

Pamoja na furaha tele

Tuimbe Yesu amefufuka.

Wimbo 124 — kipande 2

Siku yaja ya raha kubwa

Mwili huu utainuka

Umepandwa muharibifu

Utafufuka kuzoni

Miili yetu ya uzaifu

Itakapobadilishwa

Yesu utaifananisha

Na mwili wako wa kuzo.

Wimbo 54 — kipande 3

Tayari kwa uhai wako

Yesu tumefufuliwa

Ndani yako, kwa neema yako

Tumepanda juu mbinguni

Kwa kungojea siku yako

Itakayoonekana

Tukikutegemea wewe

Tunapiga vita nzuri.

 

125.             Wimbo 125

Wimbo 125 — kipande 1

Usiku kati kasikika

Sauti : « Bwana anakuja »

Mumuone Yesu akishuka :

Na tujiunge na yeye

 

Refrain : Kanisa lijitayarishe

Kwa saa hii ya kukutana ;

Ninakaribia siku kuu :

“Mutazame Bwana arusi!”

Wimbo 125 — kipande 2

Tumaini la utukufu

Linatupatia bidii

Tarajio la heri kubwa

La kuonekana na Yesu !

Kanisa lijitayarishe etc.

Wimbo 125 — kipande 3

Wanaolala mavumbini

Kama sisi watamsikia ;

Na huko, mbali ya dunia,

Watamukutana Bwana.

Kanisa lijitayarishe etc.

 

126.             Wimbo 126

Wimbo 126 — kipande 1

Ni kutamu kupenda Mungu Baba

Kumwendea sawa, bila woga

Kufanya kazi hapa duniani

Tukiongozwa na Roho wa Bwana.

Wimbo 126 — kipande 2

Ni kutamu kupata kwa saa zote

Rafiki mpendwa na msaidizi

Kuwa huru kuingia mbele yako

Kupata msaada hatarini !

Wimbo 126 — kipande 3

Ni kutamu kuwaza neema yako,

Kwa Uzaifu na ulegevu

Na kusema : Alitwaa fasi yetu

Akateswa kama Mwana Kondoo

Wimbo 126 — kipande 3

Ni kutamu kuona sifa zako,

Bwana Yesu, na watakatifu,

Kungoja kwa salama siku yako

Ya ushindi bei ya imani !

Wimbo 126 — kipande 4

Siku gani mbele ya kiti chako,

Watakatifu wametukuzwa,

Kila moja akivaa taji yake

Wataziweka kwa miguu yako !

 

127.             Wimbo 127

Wimbo 127 — kipande 1

Haki yako kamili, safi,

Ee Mwokozi ni uzuri

Na kuonekana kwa heshima

Kwa aliye kombolewa.

Wimbo 127 — kipande 2

Uliturehemu kabisa

Na tumepewa zawadi

Pia uhakika imara

Twangojea siku kubwa.

Wimbo 127 — kipande 3

Kwetu taifa kamilifu,

Hakuna tena hukumu

Hakuna pia woga kwetu !

Mungu alitusamehe.

Wimbo 127 — kipande 4

Yesu wewe ni haki yetu,

Wasema : “naja upesi”

Kanisa lote lifurahi,

Kukuona Mukombozi !

 

128.             Wimbo 128

Wimbo 128 — kipande 1

Tuimbe bila mwisho

Uwema wa Bwana :

Furaha takatifu

Ijae moyoni!

Wokovu milele

Ulitoka mbingu :

Tuna Mukombozi. (bis)

Wimbo 128 — kipande 2

Uheri wa damani !

Upendo mukubwa !

Mungu asamehe muovu

Aliyemukataa

Kwa kutupumzisha,

Kwa kutupa amani,

Yesu alijitoa. (bis)

Wimbo 128 — kipande 3

Kwa kiti cha neema

Tukiinua macho

Tutauona uso

Wa Mwokozi mwema.

Kwetu hadi mwisho

Anatuombea,

Yesu ni mushindi. (bis)

Wimbo 128 — kipande 4

Kuiongoza njia

Ya wakombolewa,

Mioyoni mwao atuma

Mwanga wake wa juu

Roho atuongoza,

Neema yatufunza

Kweli takatifu. (bis)

129.             Wimbo 129

Wimbo 129 — kipande 1

Ndugu sote tusimame

Tuna Mwalimu hapa

Bwana arusi yu aja

Kristo ataonekana. (bis)

Wimbo 129 — kipande 2

Karibu atatawala

Pamoja na kanisa

Punde atalivika taji

La sifa ya ahadi. (bis)

Wimbo 129 — kipande 3

Usiogope kundi ndogo

Wewe mpendwa wa Baba

Msalaba wa Mwana Kondoo

Uwe bendera yako. (bis)

Wimbo 129 — kipande 4

Dunia ikikuchukia

Chuki yake ni kuzo,

Pendo, tumaini, imani

Vitakupa ushindi. (bis)

Wimbo 129 — kipande 5

Sifa kwa Yesu Mwokozi

Tunamutumainia

Heri anayemuabudu

Ndani ya moyo wake. (bis)

130.             Wimbo 130

Wimbo 130 — kipande 1

Tunainua, ee Baba mpenzi

Kwako mioyo yetu na mikono

Na maombi twakutolea

Pendoni safi na ukweli

Kama waabudu wa kweli.

Wimbo 130 — kipande 2

Mbele yako twajisikia

Kama tumepewa Mwana wako

Wana wa neema yako ya mbingu

Tuna fasi rohoni mwako

Kama Yesu na rafiki.

Wimbo 130 — kipande 3

Tumependwa jinsi tulivyo

Unyonge watusumbuwa sisi,

Na kuita mapendo yako.

kwa Roho tuliyeahidiwa,

Uzaifuni twabariki.

Wimbo 130 — kipande 4

Tukipiga hivi mwendo huu,

Twaelekea kwako, Ee Yesu,

Ndani yako hazina yetu,

Maji ya chem.chemu ya mbinguni

Na mkate wa wateule.

131.             Wimbo 131

Wimbo 131 — kipande 1

Tangu asubui, mioyo yakubariki.

Mchana na usiku, tu mkononi mwako

kwa wana wako, wema wako haukomi

Tena watupenda bila hata kuchoka.

Wimbo 131 — kipande 2

Tunaomba kwako neema ya ajabu:

Utulishe leo na mkate wa mbingu;

Tunajingojea kwa musaada wako;

Daima watufunika na mkono wako.

Wimbo 131 — kipande 3

Roho wako Mungu atufundishe njia,

Kwa neno lako takatifu mioyoni!

Tukitiwa nguvu naye hakuna woga,

Na tupo washindi pamoja na Kristo.

Wimbo 131 — kipande 4

Tupo wasafiri, wageni duniani,

Moyo wetu unahaja ya mbinguni.

Ni mbinguni mwako, Mungu na baba wetu

Tutakapoingia kwa pendo lako.

Wimbo 131 — kipande 5

Utuchunge katika safari salama,

Hadi siku ya heri bila magumu,

Tutaonja pamoja uheri muzuri,

Wakati Yesu atakapo tupumuzisha.

132.             Wimbo 132

Wimbo 132 — kipande 1

Sifaidiki wala kupoteza

Jangwani humu sina chaguo :

Hakuna pori hata jani bichi,

Hakuna maji yakuninywesha.

Wimbo 132 — kipande 2

Jangwani hakuna kimbilio,

Wala pumziko hata kidogo,

Kwa nini mimi nisimame bure

Ninapokaribia kufika?

Wimbo 132 — kipande 3

Jangwani mimi ninajua njia :

Njia ya pendo, neema na imani,

Nitakayoifwata bila shaka,

Kwani Mwokozi aliipasua.

Wimbo 132 — kipande 3

Njia ya nguvu ijaayo heri,

Ambamo yote ni salama tu ;

Iniongozayo toka duniani,

Ilinifike kwa Baba Mungu.

Wimbo 132 — kipande 4

Bila tamaa, bila kazi na woga,

Umenifundisha kukaa pale,

Nitaonja, pale patakatifu

Pumziko karibu nawedaima.

133.             Wimbo 133

Wimbo 133 — kipande 1

Muchungaji, kwa gongo lako

Pendoni mwako twakaa ;

Unatutunza tuna vyote,

Watuita kondoo zako.

Wimbo 133 — kipande 2

Bwana wangu, kama dunia

Inatawanya wapendwa…

Mkono wako muaminifu

Ulituumba mumoja.

Wimbo 133 — kipande 3

Tupendane kwa pendo kweli ;

Kando yake tuwe mmoja

Roho, Mwana na Baba pia,

Kwa imani ni ushirika.

134.             Wimbo 134

Wimbo 134 — kipande 1

Kwa miguu kama Maria,

Kuacha saa zipite

Kwa kimya tukijisahau,

Yesu tukuache useme.

Wimbo 134 — kipande 2

Kwa miguu katika taabu,

Ninapata, kwa mateso,

Pendo na musaada wako,

Unanifuta machozi.

Wimbo 134 — kipande 3

Kwa miguu, kwa sifa zako,

Tumwange,  Mwokozi Yesu,

Manukato yasiyo changwa

Ya chupa iliyovunjika.

Wimbo 134 — kipande 4

Ibada ya wakupendao,

Marashi ya juu mbinguni,

Yaliyochungwa kwa saa kubwa

Ya toleo lililotosha.

Wimbo 134 — kipande 5

Nibaki kwa miguu yako,

Hapa chini sauti yangu

Iiname kwa wimbo mbinguni,

Mwana wa Mungu aliyekufa !

135.             Wimbo 135

Wimbo 135 — kipande 1

Tuimbe, tuimbe katika wimbo safi

Pendo la Mwokozi

Neema yake amini

Siku zote ni mpya

Inaangaa sana

{Yeye mkubwa na muzuri

Tumsifu Bwana. (bis)}

Wimbo 135 — kipande 2

Tuimbe, tuimbe katika wimbo safi

Pendo la Mwokozi

Kiti cha neema

Fasi ya hakika

Kwa mioyo yetu

{Yeye mkubwa na muzuri} etc.

Wimbo 135 — kipande 3

Tuimbe, tuimbe katika wimbo safi

Pendo la Mwokozi

Yesu utukufuni

Ni ushindi wetu

Na heri yetu

{Yeye mkubwa na muzuri} etc.

136.             Wimbo 136

Wimbo 136 — kipande 1

Sifa, uwezo na nguvu

Heshima kwake Mungu

Upendo na shukurani

Kwake Yesu Mwokozi.

Wimbo 136 — kipande 2

Mwokozi ulivikwa miiba

Damu yako’kamwangwa

Hata gazabu ya Mungu

Na Ikakulemea.

Wimbo 136 — kipande 3

Kwako ee Yesu mateso

Kilio, kifo, kuachwa

Na kwa sisi ukombozi

Wokovu, usamehe.

Wimbo 136 — kipande 4

Sifa, uwezo na nguvu

Heshima kwake Mungu

Upendo na shukurani

Kwake Yesu Mwokozi.

137.             Wimbo 137

Wimbo 137 — kipande 1

Wakristo tulichaguliwa

Kuishi huko mbinguni

Mbele ya muumbaji wetu

Tuimbe nyimbo za furaha

Wimbo 137 — kipande 2

Tulisitahili gazabu

Na tulikufa zambini

Katika hali yetu mbaya

Yesu alituokowa.

Wimbo 137 — kipande 3

Tumeokolewa na Yesu

Kwa kufa na kufufuka

Tukapate Roho wake

Zawadi ya pendo lake.

Wimbo 137 — kipande 4

Ndani ya Yesu tuna Baba

Nasi tu watoto wake

Kwa neema yake kila siku

Twapata matunzo mema.

Wimbo 137 — kipande 5

Pendo lake halina mwisho

Hakuna cha kututenga

Hata mbinguni na duniani

Anatupenda daima.

Wimbo 137 — kipande 6

Kristo ametupa uriti

Wa mbingu kwa damu yake

Ni fungo nzuri ya furaha

Karibu naye  milele.

Wimbo 137 — kipande 7

Twakusifu kwa  tumaini

Baba harikisha siku

Mwana mupendwa kwa uwezo

Atakapo tutwaa kwake.

138.             Wimbo 138

Wimbo 138 — kipande 1

Kazi imekwisha kwa Mwamba wa Yakobo

Alilolisema, atalitimiza.

Bwana atatushika mkono ! (bis)

Kwa kuwa ni Mungu, (bis)

Kwa kuwa ni Mungu makimbilio yetu.

Wimbo 138 — kipande 2

Bwana anatupenda milele na milele :

Neema yake kwetu haina mupaka ;

Kwa lengo atatufikisha, (bis)

Ndiye tumaini, (bis)

Ndiye tumaini ndiye uheri wetu.

Wimbo 138 — kipande 3

Maadui wetu anawajua wote

Atupigania na atatufungua ;

Atashindana kwa nguvu (bis)

Na waovu wote, (bis)

Na waovu wote watamukimbia Bwana.

Wimbo 138 — kipande 4

Miili ya kufa itapata ushindi

Twajua karibu ataigeuza

Baragumu iliapo (bis)

Kwetu waamini, (bis)

Kwetu waamini tutaona sifa tu.

Wimbo 138 — kipande 5

Tutukuze Mungu, aliye Baba wetu!

Bwana akiwa kwetu: tutashinda yote.

Hatutatengwa na yeye (bis)

Tushinde kwa Yesu, (bis)

Tushinde kwa Yesu tuishi kumupendeza.

139.             Wimbo 139

Wimbo 139 — kipande 1

Sikugani tutapata uheri

Wakukusanyika nawe daima

Na kukuona Mwokozi muabudiwa

Pahali pa amani milele.

Wimbo 139 — kipande 2

Muda mfupi ututengao nawe

Watuongezeya tumaini

Saa zapita na asubui yaja

Karibu Bwana utatoka juu.

Wimbo 139 — kipande 3

Miaka elfu kwako ni kama wazo

Kwetu sisi usikuwapita

Bwanani siku gani utakwisha ?

Siku gani nyota itaangaza.

Wimbo 139 — kipande 4

Kwa kukesha, vita, mchoko, uzaifu

Tunangoja kuinuliwa naye

Sababu mioyonimwetu nyota hii

Yatuangazia nuru njema.

Wimbo 139 — kipande 5

kungojea kutukuzwa milele

Kwatupa hamu yakukuona

Moyo wetu wakutaka ee Yesu

Leta jibu la tumaini hii.

 

140.             Wimbo 140

Wimbo 140 — kipande 1

Ee Bwana uliyejitoa msalabani,

Utujaze bidii tukutumikie

Kwa mali, mwili na roho

Tupe kutembea hata tupo wanyonge,

Tukikutazama, na kwa wewe mwenyewe,

Tuwe sote na ushindi.

Wimbo 140 — kipande 2

Utupe kuonja namuna ni kutamu,

Kwa kila mutoto wa Mungu apumzikaye,

Kupenda na kutumika !

“Kwangu kuishi ni Kristo” : Huu uwe musimamo

Wa wakristo wote, kila moja aseme,

Na wote wafanye hivyo.

141.             Wimbo 141

Wimbo 141 — kipande 1

Kwa furaha na tumaini,

Nakuona Mwokozi wangu.

Najua pendo lako kubwa,

Laokoa mwenye zambi ;

Nakutumainia eeBwana

Wewe ndiwe heri yangu.

Wimbo 141 — kipande 2

Ni mbinguni, kwa mwendo wangu,

Nitarajiapo mimi

Chemchemu hai yake Roho

Yaninywesha nichokapo

Hatarini, hazina yangu

Ni nguvu ya mkono wako.

Wimbo 141 — kipande 3

Mchana, chini ya nuru yako ;

Usiku kifuani mwako,

Asubui waniangazia

Nakuniongoza njiani

Na kila mangaribi Baba,

Waandaa kesho yangu.

Wimbo 141 — kipande 4

Mwisho wa safari yangu hii

Nauona ni karibu

Ninangoja kwa uhakika,

Uriti ulio mbinguni :

Hata nikiwa kaburini,

Nitafufuka kwa shangwe.

142.             Wimbo 142

Wimbo 142 — kipande 1

Juu ya kanisa lako lote,

Ulipendalo saa zote

Bwana katika neema yako,

Unalimimia zawadi

Waamini, kwa tumaini,

Wapiga magoti pote ;

Utatujaza tumaini :

Bwana utakuwa nasi.

Wimbo 142 — kipande 2

Ee Bwana Yesu wakumbuka

Ahadi za Neno lako ;

Roho wako anafariji,

Na kuongoza wana wako,

Tutembeze nuruni mwako

Chunga moyo wetu kwako

Kanisa lako likiomba

Lifurahi ndani yako.

143.             Wimbo 143

Wimbo 143 — kipande 1

Mungu Baba, wewe ulinipenda

Wewe Bwana Yesu

Ulinipenda kuzidia mama

Apendavyo mtoto. (bis)

Wimbo 143 — kipande 2

Nikupende, ee Mungu wa mapendo,

Ndiwe ulianza

Nikupende, unipatiaye nguvu,

Nguvu, mwamba wangu. (bis)

Wimbo 143 — kipande 3

Chemchemu ya neema, ulinipenda,

Mwanzo wa wokovu

Ulinigeukia ! Kanipenda

Utanifikisha. (bis)

Wimbo 143 — kipande 4

Nikupende : kamwe akupendaye

Hatabaki pekee

Ni kwa pendo lako ulinipenda

Langu litaishi. (bis)

 

144.             Wimbo 144

Wimbo 144 — kipande 1

Kwako uliye tufundisha

Neno lililo la kweli

Wewe ulitufahamisha

Pendo lako lidumulo,

Wimbo 144 — kipande 2

kwako uwezeshaye mutu

Kuwa mtakatifu kweli

Katika nuru kubwa sana

Upendapo wako wawe,

Wimbo 144 — kipande 3

Kwako wewe, kwa neema yako

Ulitutosha kwa muovu,

Ulituokoa na uwezo

Wa giza pia mauti,

Wimbo 144 — kipande 4

Kwako Mungu na Baba wetu,

Uliyetubeba vema

Kati ufalme, hekaluni

Mwa Yesu, Mwana wa pendo,

Wimbo 144 — kipande 5

Kwako utukufu, hekima,

Mungu wa pendo na kweli,

Kwako nguvu na utajiri

Katika milele yote !

Wimbo 144 — kipande 6

Kwako, Bwana, mwenye ushindi

Uliotupa uheri,

Kwako, Yesu, tunakusifu ;

Tunakuabudu, Mwokozi.

145.             Wimbo 145

Wimbo 145 — kipande 1

Kondoo za Yesu, ziko pendoni mwako,

Zinamutambua na kufwata sauti ;

Aziongozaye azipa mazuri ;

Aliweka pendo lake ndani mwao.

Wimbo 145 — kipande 2

Hawapungukiwi kitu zizini mwake ;

Kando ya mchungaji, hawaogopi kitu.

Alinda kondoo, kifuani mwake ;

Jicho lake nzuri lawafurahisha.

 

146.             Wimbo 146

Wimbo 146 — kipande 1

Duniani tufani

Ikiunguruma

Inanishituwa :

Nakuogopesha

Mimi sitaogopa :

Yesu yuko nami,

Hata uwepo wake

Wafukuza woga.

Wimbo 146 — kipande 2

Na nikiona giza

Maishani mwangu

Unaitawanya,

Ee Mwokozi mwema !

Juu ya wingu lote

Hakika nakuona :

Unanitia moyo,

Wanijaza heri.

Wimbo 146 — kipande 3

Na nishindwapo mimi

Katika hatari,

Nipo mkononi mwako

Muchungaji mwema

Kwa pendo lako njema

Mimi sitatengwa

Nafichama bawani,

Sitashituliwa.

Wimbo 146 — kipande 4

Kikombe kinajaa :

Najua pendo lako,

Na neema yako nzuri

Itanifuata

Kati safari yangu,

Mimi mgeni hapa,

Wewe, uriti wangu

Haubadiliki.

 

147.             Wimbo 147

Wimbo 147 — kipande 1

Chemchemu nzima,

Wokovu wetu,

Damu ya Kristo ilimwangwa.

Kuteswa kwake,

Kujitolea,

Ndiyo wokovu wa muovu.

Wimbo 147 — kipande 2

Furaha kubwa !

Kristo ni njia

Ifikishayo kwa lengo.

Yesu asamehe ;

Hakuna mutu

Asiyemupa wokovu.

 

148.             Wimbo 148

Wimbo 148 — kipande 1

Uheri ni kwako, Mwokozi wa mapendo.

Ulitufundisha wimbo wakufurahi ;

Na kwa wema wako, tunaishi sisi,

Na wataka milele kutubariki.

Wimbo 148 — kipande 2

Tumepata sisi muchoko duniani,

Tulipokuwa watoto wa kasirani ;

Tulipokimbia neema yako Yesu.

Tulipotea zaidi duniani.

Wimbo 148 — kipande 3

Ukaonekana, kavunja minyororo ;

Pendo lako kubwa likatosha hukumu.

Kwa imani neema ikatufunza

Yakwamba tuna salama naye Roho.

Wimbo 148 — kipande 4

Mapendo makubwa yatuambia kwamba,

Sisi tuna deni yakukusifu wewe,

Ongoza mioyo ili itazame

Mbinguni utuwekeapo hazina.

 

149.             Wimbo 149

Wimbo 149 — kipande 1

Bwana anatuita :

Tumuendee !

Ni mwema, mwaminifu,

Tegemeo ;

Wokovu atoao,

Hautanyanganywa.

Pamoja na huruma,

Abariki.

Wimbo 149 — kipande 2

Pendo lake ni kubwa :

Mukombozi

Kajitoa mwenyewe

Kwa muovu.

Pale musalabani

Alipenda kufa ;

Mutegemee nafsi,

Abariki.

 

150.             Wimbo 150

Wimbo 150 — kipande 1

Wokovu, salama !

Habari ya furaha

Kwa watu waovu !

Yatuponya mioyo

Na kidonda kichungu,

Yatuliza woga. (bis)

Wimbo 150 — kipande 2

Wokovu, msamaha !

Tuimbe maneno haya

Popote duniani !

Tuungane pote

Na waamini wote

Kukuimbia Bwana ! (bis)

Wimbo 150 — kipande 3

Wokovu, salama

Yesu, mateso yako

Yalileta heri ;

Tunakushukuru

Ewe mwenye huruma

Ee Mungu Mwokozi. (bis)

Wimbo 150 — kipande 4

Sifa kwa Kondoo !

Heshima na uwezo

Kwa mwenye mateso

Aliyetufia

Juu ya musalaba !

Twakuabudu, Bwana ! (bis)

151.             Wimbo 151

Wimbo 151 — kipande 1

Bwana Ulinipenda, mbele nuru iwe

Juu ya dunia uliyoiumba

Vile nyota ya mwanga kutembea muchana

Na kutoa uzima juu ya dunia yote

Mungu ulinipenda. (bis)

Wimbo 151 — kipande 2

Mungu ulinipenda, wakati msalabani

Yesu ‘kaonekana akijiachilia

Kwa kuniokoa toka moto wa milele

Mwana wako alichukua zambi zangu zote

Mungu alinipenda. (bis)

Wimbo 151 — kipande 3

Tanipenda milele!Shetani na dunia

Hawatazuia Kamwe hili pendo.

Kwa uwingi wa zambi, neema ikawa nyingi

Pendo langu lijibu kwa pendo lako Mungu.

Wewe wanipenda. (bis)

 

152.             Wimbo 152

Wimbo 152 — kipande 1

Sifa yako Mungu, yaangaa katika Neno

Kwa watoto wako, hazina damani ;

Ni sauti ya rafiki, na tegemeo ;

Ni barua ya pendo kutoka mbingu.

Wimbo 152 — kipande 2

Tunaposoma, nafsi yashibishwa daima

Mioyo imepumzishwa na mizigo

Ndiyo chemchemu inayotoa uzima,

Muto wa neema kwa maji ya wokovu.

Wimbo 152 — kipande 3

Ninyi musumbukao duniani humu,

Ninyi ambao mioyo yachoka kweli,

Muje wote na mupate hapa salama

Kutoka katika injili na pendo.

 

153.             Wimbo 153

Wimbo 153 — kipande 1

Sikieni wote habari njema ;

Yesu akafa kwa kutuokoa !

Anaemwamini ana uzima :

Wokovu ni zawadi ya Mungu. (bis)

Wimbo 153 — kipande 2

Wenye zambi, katika taabu yenu,

Mukishindwa kutazama Mungu,

Njooni kwa Kristo anaonyesha Baba,

Kwa upendo a katoka mbinguni. (bis)

Wimbo 153 — kipande 3

Ee, pokeeni neno hili nzuri

Roho anaambiya moyo wako.

Ni Yesu peke mponya na mfariji :

Njooni wote kwa mwokozi wetu. (bis)

 

154.             Wimbo 154

Wimbo 154 — kipande 1

Kwa nia moja, wapendwa wako

Waimba sifa, pendo lako kubwa

Mashauri yako yote ni nguvu imara

Na nia zako hazitageuka.

Wimbo 154 — kipande 2

Siku yaja, Ee Mungu wa kweli

Dunia, mbingu zitakapokimbia

Ila watakatifu wako wa neema

Watasimama imaramilele.

Wimbo 154 — kipande 3

Siku yaja ! Kuja Bwana Yesu

Kuja kuishi wokovu kuzoni

Namauti yamezwe na ushindi

Kusanya wateule juu mbinguni.

 

155.             Wimbo 155

Wimbo 155 — kipande 1

Mwana mpendwa ufurahishaye

Upendotele wa Baba yako

Ukawa mtu na kwa kujitoa

Tumejua upendo wa Mungu.

Wimbo 155 — kipande 2

Chanzo cha mwangaza wa milele

Jua la Mungu liangazalo

Kwa mwangaza wako tunazaliwa

Giza ya mioyo yetu yatoka.

Wimbo 155 — kipande 3

Ukusanyaye waovu wote

Mwana wa watu ukatundikwa

Damu yakoni kisima daima

Chaosha milele aaminiye.

Wimbo 155 — kipande 4

Chanzo cha sifa na utukufu

Mwana Kondoo unayeangaa

Dunia yote yakuhimidi

Taifa lako lakuabudu.

 

156.             Wimbo 156

Wimbo 156 — kipande 1

Kukuona uso kwa uso,

Na Kusikia pia

Sauti iliyotutunza,

Na inayotuongoza ;

Wimbo 156 — kipande 2

Kukufuata pamoja,

Tukivaa nguo safi,

Iliyo kama teluji

Ingaayo kwa jua ;

Wimbo 156 — kipande 3

karibu, hakuna giza !

Karibu nawe, Bibi

Ataonyesha uwezo,

Neema pia uzuri.

Wimbo 156 — kipande 4

Ni tunda la pendo lako !

Watu watamuona,

Amezungukwa mwenyewe

Na pendo la milele.

Wimbo 156 — kipande 5

Bila kuelewa pendo,

Tunapiga magoti,

Kwani musalaba wako

Ulilishusha kwetu.

Wimbo 156 — kipande 6

Utimilifu wa Bwana

Kwa muhuri wa Roho,

Kwa raha na uhakika

Watunywesha, twashiba,

Wimbo 156 — kipande 7

Siku isiyo na wingu,

Tuitarajiayo,

Wakati tutakutana

Kukupenda ee Yesu !

 

157.             Wimbo 157

Wimbo 157 — kipande 1

Utakapokuja, Yesu, kwa nguvu

Walalao watafufuliwa,

Kwa muda mchache watanyakuliwa,

Mbele ya Baba watafikishwa.

Wimbo 157 — kipande 2

Sisi tulio hai duniani,

Hazina ifichwayo uliyopenda,

Usiku tukikesha na kuomba,

Tunakungoja kama mwokozi.

Wimbo 157 — kipande 3

Kujuta, kulia na kuteseka,

Havipo pale juu mbinguni :

Panajaa uepo wako, Yesu ;

Vyote ni salama na pumziko.

Wimbo 157 — kipande 4

Pale ndani ya nyumba yake Baba

Kuna taifa la waabudu,

Kando yako kuliko duniani

Tukiwa wafalme, makuhani.

Wimbo 157 — kipande 5

Ukuu wa upendo wa ajabu,

Uangazao neema na kweli !

Ulitembelea mutu mutumwa,

Duniani alikataliwa.

Wimbo 157 — kipande 6

Ukaacha kuangaa kwa milele,

Ukashuka tumboni mwa kifo,

Msalabani, ee Bwana wa uzima,

Ukapigwa juu ya zambi zetu.

Wimbo 157 — kipande 7

Tujipe moyo, tuinue vichwa ;

Ndugu, Bwana, Arusi atakuja !

Atualika kwa karamu milele :

Na tutapumzika pendoni !

 

158.             Wimbo 158

Wimbo 158 — kipande 1

Jina nzuri liangazalo,

Duniani mujaamo giza,

Katika kuangaza kwake,

Mungu asiyeonekana !

Wimbo 158 — kipande 2

Jina la Mtu munyenyekevu

Na mwenye huruma kwetu,

Achukuaye, mtumwa mtashi,

Mzigo wa mateso yetu ;

Wimbo 158 — kipande 3

Jina kubwa lenye uwezo

Jibu la imani yetu ;

Likusanyalo wateule,

Kando yako duniani ;

Wimbo 158 — kipande 4

Jina ambalo, Mungu Baba

Ataweka juu ya vyote ;

Mbele yake, mbingu, kuzimu,

Dunia vitainama.

Wimbo 158 — kipande 5

Jina mupya, sehemu kubwa

Ya wateule washindi,

Jina kanisa litabeba,

Milele mbinguni mupya ;

Wimbo 158 — kipande 6

Jina la Yesu bila mpaka,

La Mungu mwenye uwezo,

Na la Mwana, Kondoo mwokozi,

Na mtu aliyefufuka ;

Wimbo 158 — kipande 7

Jina la nyota ya asubui,

Jina la nyota ya mchana,

Sifa kwako, Jina la nuru,

Na pendo, libarikiwe !

 

159.             Wimbo 159

Wimbo 159 — kipande 1

Uliyetufundisha wimbo wa furaha

Mioyo yetu yajibu kwa wito wako

Tusisahau kamwe unyonge wetu sisi

Ili tutangaze vema upendo wako

Na kusifu wema wako udumuo

Wimbo 159 — kipande 2

Tulikuwa mbali nawe, tukiteseka,

Tulikuwa gizani, bila msaada,

Punde kwa macho yetu tuliiona nuru ;

Yesu akatufunulia Jina la Baba

Na wema wako unaodumu daima ;

Wimbo 159 — kipande 3

Ee Mungu Mwokozi, ambaye neema yako

Haikujizuiza kutusaidia,

Shauri zako nzuri, kwa njia nzuri pia,

Tutakutukuza kwa wimbo wa milele,

Na tutausifu wema wako daima !

 

160.             Wimbo 160

Wimbo 160 — kipande 1

Kwenye kiti cha enzi cha Mungu Mkuu,

Roho zangoja utukufu,

Wakifurahia pia,

Ushindi wa Mwokozi wao.

Kutoka kwa kundi lake,

Alilopendelea sana,

Wimbo waanza hapa chini :

Usifiwe, usifiwe.

Wimbo 160 — kipande 2

Tukiwa mwili mumoja,

Tusifu mfalme wa uzima

Aliyefufuka mbele;

Ile wakati wa taabu

Mzigo wa mabaya yetu

Ukalemewa Mtakatifu

Wakati uliachwa na Mungu :

Usifiwe, usifiwe.

Wimbo 160 — kipande 3

Yeye ni Kuhani Mkuu

Akaaya katika nuru,

Na Mwokozi wetu pia,

Anatutetea kwa Baba.

Ametuweka muhuri,

Tunaye Roho wa uzima

Kwa yeye Kanisa lasema :

Usifiwe, usifiwe.

Wimbo 160 — kipande 4

Upesi kwa Bwana Arusi

Kwa ahadi ya kuaminiwa,

Aja na kutupeleka.

Tutakuwa naye milele,

Tukiimba wimbo mpya

Katika urizi mbinguni.

Ndipo tutasema daima :

Usifiwe, usifiwe.

 

161.             Wimbo 161

Wimbo 161 — kipande 1

Pendo lako latukusanya

Sisi ni wapendwa wako

Kwa Roho twakuja pamoja

Kukuabudu Mwokozi !

Wimbo 161 — kipande 2

Uepo wako ni mema kuu

Pendo lako linadumu,

Unawapa uwapendao

Pumziko, heri, salama.

Wimbo 161 — kipande 3

Moyo wetu wakutukuza

Sauti zetu, siku hii,

Zinatangaza kazi yako,

Sifa na kurudi kwako.

 

162.             Wimbo 162

Wimbo 162 — kipande 1

Ua za utukufu zimefunguliwa

Kwenye wateule, wakiinuwa ushindi,

Pamoja na Yesu Bwana na Mfalme !

Wimbo 162 — kipande 2

Mbingu yapaza sauti ya furaha

Usiku umekwisha ; kilio na huzuni

Imetoweka, hapatakuwa kifo !

Wimbo 162 — kipande 3

Sauti itawaita kutoka mbinguni,

Kwa furaha kubwa, mabikira wapita,

Na taa mkononi pamoja na Bwana wao ;

Wimbo 162 — kipande 4

Na sababu walikuwa waaminifu,

Awafungulie makao ya milele,

Na kuingizwa karamuni daima.

 

163.             Wimbo 163

Wimbo 163 — kipande 1

Anakuja toka utukufuni,

Kristo, aliyekufa mutini :

Na watakatifu wamshangilia,

Waliosikia sauti yake, –

Aleluya ! Aleluya ! –

Wataandamania Mfalme.

Wimbo 163 — kipande 2

Mubarikiwa wa tumaini,

Akingaa anatoka mbingu.

Wapendwa wake waliosumbuka,

Watafurahi pamoja naye.

Aleluya ! Aleluya !

Mwana wa Mungu aonekana.

Wimbo 163 — kipande 3

Mumuone kuzoni ana alama

Za mateso aliyopata.

Akizungukwa milele na sifa,

Wakombolewa watamuabudu.

Aleluya ! Aleluya !

Aja, Bwana, Arusi, Kondoo !

Wimbo 163 — kipande 4

Bibi arusi anakuita, Bwana ;

Yeye na Roho wasema : Kuja !

Kuja tukuone utukufuni,

Na uangae, ndani ya wako !

Aleluya ! Aleluya !

Ndiyo, Bwana ! – Watujibu : « Naja ».

164.             Wimbo 164

Wimbo 164 — kipande 1

Yesu, Mwana mpendwa wa Baba,

Ulishuka hadi kwetu,

Kwa watoto wote wa nuru

Jina lako nilikubwa !

Wimbo 164 — kipande 2

Hakuna aliye kama, Yesu,

Wewe pekee ndiwe kweli ;

Yote ndani yako ni pendo,

Ukubwa, uzuri pia,

Wimbo 164 — kipande 3

Tangu hapa chini kwa moyo,

Mwaminifu tuishi kwako,

Kwa bidii twakutolea,

Kuzo ya imani yetu !

 

165.             Wimbo 165

Wimbo 165 — kipande 1

Watumwa wa zambi, tuliishi duniani

Tulipotea bila tumaini

Ukatutazama katika giza kubwa

Kwa kutusaidia ukatoka juu.

Wimbo 165 — kipande 2

Ukashuka hadi kwa msalaba wa haya.

Ulipopatwa na gazabu ya Mungu

Kuachwa na kifo vikapita juu yako

Na ukapigwa na hukumu ya Mungu.

Wimbo 165 — kipande 3

Tumeokolewa kwa neema ya ajabu

Tukipendwa nawe twaenda mbinguni

Tuna usalama na kazi yako pia

Ilituletea njia ya pumziko.

Wimbo 165 — kipande 4

Kwa wimbo wa pendo na wa shukrani pia

Nafsi zetuzainuka kwako Bwana

Tunangoja siku ya kuokolewa kwetu

Inayoangaa kwa macho ya imani.

 

166.             Wimbo 166

Wimbo 166 — kipande 1

Yesu akatoka mbinguni,

Akaja, Akaja,

Na akajitoa mwenyewe,

Kwa kifo, Kwa kifo,

Kwa sifa akapanda mbinguni

Kwa Baba, Kwa Baba.

Wimbo 166 — kipande 2

Ukaapo kwa kiti cha enzi

Nakuona, (bis)

Mwana uliyelaumiwa

Kwa muti, (bis)

Baba akakufanya kuwa

Mufalme. (bis)

Wimbo 166 — kipande 3

Kwa sasa tutakuona

Kwa macho, (bis)

Twataka, ee Mwokozi wetu

Mtukufu, (bis)

Tukutumikiye kwa pendo

Zaidi, (bis)

Wimbo 166 — kipande 4

Nyayo zetu zionekane

Duniani (bis)

Tukikufuata kwa amani

Duniani, (bis)

Majaribuni na furaha,

Na vita. (bis)

Wimbo 166 — kipande 5

Mapambazuko ni karibu

Hakika, (bis)

Hewa yalilia mlimani

Na mbali, (bis)

Juu ya milima asubui ni

Karibu ! (bis)

 

167.             Wimbo 167

Wimbo 167 — kipande 1

E nuru kamilifu

Isiyo haribika

Watakatifu watakapofurahi

Uheri wa ajabu,

Uso  muabudiwa

Utawaangazia  kati salama ! (bis)

Wimbo 167 — kipande 2

Kwa milele nuruni

Nyumbani mwake Baba!

Giza itatoweka mbele ya mchana

Mbali ya dunia

Nafsi yetu yote

Itaonja pumziko karibu naye. (bis)

 

168.             Wimbo 168

Wimbo 168 — kipande 1

Sifa kwako Mwokozi

Yesu na kwa kazi yako

Wachaguliwa wako

Kwa juhudi na salama

Wakusanyika hapa kutangaza upendo.

Wimbo 168 — kipande 2

Kwa furaha ya roho

E sadaka ya kuchinjwa

Mwana Kondoo mshindi

Twakumbuka kifo chako

Pamoja tunaimba kazi ya ukombozi.

 

169.             Wimbo 169

Wimbo 169 — kipande 1

Kukuinua Mwana wa Baba

Wimbo wa mbingu na dunia

Utapanda patakatifu

Milele, Milele.

Wimbo 169 — kipande 2

Uso wako ‘tatuangazia

Rohoni mwetu kwa neema

Wewe pekee utatawala

Milele, Milele.

Wimbo 169 — kipande 3

Wako watapasha habari

Za kifo chako cha toleo

Za ushindi ulio hai

Milele, Milele.

Wimbo 169 — kipande 4

Kanisa mshuhuda wa sifa

Litaimba neema yako

Kwako wewe mufalme wake

Milele, Milele.

 

170.             Wimbo 170

Wimbo 170 — kipande 1

Ee Yesu ! (bis)

Mungu mkuu wa mbinguni,

Wewe mwenye sifa tele,

Shina la utukufu,

Kanisa linakuabudu

Ulilojipatia

Kwa damu ! (bis)

Wimbo 170 — kipande 2

Ee Yesu ! (bis)

Utuongoze Bwana.

Unavyotaka ni vyema

Na si muzigo kwetu ;

Upendo washinda woga

Milele. (bis)

 

171.             Wimbo 171

Wimbo 171 — kipande 1

 

172.             Wimbo 172

Wimbo 172 — kipande 1

Bwana, yawezekana mtu wa mavumbi,

Mwenye zambi kama mimi,

Awe mwana wako na kukuita Baba,

Atiwe karibu yako ?

Wimbo 172 — kipande 2

Ndiyo, kwa mipango ya pendo lako kubwa,

Ulipenda kutuokoa

Ukamwacha Mwana hukumuni

Akipigwa hata kifo.

Wimbo 172 — kipande 3

Mpendwa wako Yesu akufurahishaye,

Ajuaye mambo yako,

Akajitoa mwenyewe kuwa sadaka

Atuokoe wenye zambi.

Wimbo 172 — kipande 3

Kizuri gani cha kuona kwa milele

Isipokuwa msalaba

Wa Mfalme wa uzima wakati wa giza

Mungu akihukumu zambi.

Wimbo 172 — kipande 4

Malaika wanashangaa wakitazama

Na kusema kwa magoti

Kwa hofu takatifu fumbo la ajabu

La kujishusha kabisa.

Wimbo 172 — kipande 5

Nasi tuliyookoka, jamaa teule

Ulitakalo karibu,

Hatutaweza kabisa kusifu pendo

Matunda ya kazi yako !

 

173.             Wimbo 173

Wimbo 173 — kipande 1

Bwana ukagunja kichwa

Ukabeba mzigo

Kwa kunilipia deni

Ukajitolea

Mimi si lemewe tena, Sina mzigo tena ! (bis)

Wimbo 173 — kipande 2

Na kikombe cha hasira

Kilikufurikia

Ulikinywa hadi mwisho

Kipo wazi kwangu

Teso lako, lalamiko ni wokovu wangu ! (bis)

Wimbo 173 — kipande 3

Kwa kufa, ukaniponya

Nilikufa nawe

Mshindi, ukanifungua

Ninaishi kwako

Kuja kwako mawinguni ni sifa na wewe ! (bis)

 

174.             Wimbo 174

Wimbo 174 — kipande 1

Nyota iangazayo

Gizani mwangu

Fimbo kiongozi

Mkate chakula

Kisima cha maji

Taa nionayo

Pale ngambo nzuri

Yote ni wewe.

Wimbo 174 — kipande 2

Hakuna mwengine

Kama wee Yesu

Nionapo shida

Wanifariji

Tumaini njema

Msaada wangu

Salama, uhakika

Vyatoka kwako.

Wimbo 174 — kipande 3

Utakapokuja

Nitasikia

Mwito wa sauti

Iniitayo juu

Ninaleta nini ?

Hakuna adui

Wafungua mlango

Wanipa vyote.

 

175.             Wimbo 175

Wimbo 175 — kipande 1

Mbingu ilitembelea dunia

Emanueli amekuja

Mungu alijifanya mutu

Kanisa limuabudu.

Wimbo 175 — kipande 2

Pendo lipitalo fahamu

Mwana wa Mungu, muumba

Alitujia, wenye zambi

Kama vile mtumishi.

Wimbo 175 — kipande 3

Pendo kubwa, linyenyekevu

Lilishuka chini sana

Mwana wa mutu kajitoa

Kufilia dunia hii.

Wimbo 175 — kipande 4

Manukato isiyochangwa

Wako watakutolea

Marasi ya kusifu kwetu

Ni Yesu pendo lako.

Wimbo 175 — kipande 5

Mbingu ilitembelea dunia

Emanueli amekuja

Mungu : mutu, fumbo ya ajabu

Kanisa limuabudu.

 

176.             Wimbo 176

Wimbo 176 — kipande 1

Kwa unyenyekevu mkubwa

Twakufwata zikini

Yesu ulizarauliwa

Ukiwa msaidizi

Pendo lako ni msaada

Na huruma, kamili

Juu ya watu wabaya

Likamwanga mema tu.

Wimbo 176 — kipande 2

Roho yako ya mapendo

Yafungua hazina

Mungu mwenyewe atambua

Humo utakatifu

Nasi tukijazwa neema

Tu watoto wa Mungu

Tunaweza kukufuata

Njiani kwa upendo

Wimbo 176 — kipande 3

Hayani na uchunguni

Sikitikoni pia

Mwili wetu uuguwapo

Mfano wako Mwokozi

Utatupatia moyo

Hata tu wazaifu

Kukufuata kikamili

Katika uutu wako.

Wimbo 176 — kipande 4

Muda kitambo tutakaa

Karamuni  mbinguni

Wako watakapo kuona

Mwana Kondoo wa Mungu

Tukivaa utukufu

Tukiwa kuume kwako

Yesu tukikufanana

Kweli tutashibishwa.

 

177.             Wimbo 177

Wimbo 177 — kipande 1

Ee Mwokozi mwema.

Kanisa leo

Linakutamani.

Uje upesi !

Nyota ya mbinguni,

Moyoni mwetu,

Utukufu wako,

Usifiwe !

Wimbo 177 — kipande 2

Tukiwa mbinguni,

Tutapendezwa

Na zawabu yetu !

Njoo Bwana Yesu !

Na kanisa lako

Kwa siku ile

Litapokelewa

Huko mbinguni !

 

178.             Wimbo 178

Wimbo 178 — kipande 1

Twaimba mapendo mazuri yake Yesu

Inatosha kwetu, hii hazina nzuri,

Tuu ya ulimwengu unaojaa nuru,

Yanaonekana, mapya kila siku.

Pendo hili nzuri, linapita kuzimu,

Na linapanda juu kuliko mbingu.

Tangu umilele, mbele dunia kuumbwa,

Bwana, ka Tupenda ! Tunakubariki !

Wimbo 178 — kipande 2

Mahali pa heri, ukijaa na sifa,

Wewe wa milele umevikwa kungaa,

Muumba muweza, upewaye ibada,

Pekee ulishuka kati ya waovu,

Ili u Tulete nyumbani mwake Baba,

Ukiacha haki zako na kuonewa.

Muchungaji mwema, kaona taabu yetu,

Uka Tutafuta ! Tunakubariki.

Wimbo 178 — kipande 3

Ulifwata njia yako pekee yako,

Ukitoa hazina za wema wako,

Ukitoa neema : Hiyo ni siri kubwa !

Kwa upofu wake, mutu alikukataa :

Kazarauliwa bila kuficha uso

Kwa lengo hilo kuu la mapendo yako,

Hakuna chakuzuia kazi ya neema yako ;

Bwana, ka Tupata ! Tunakubariki.

Wimbo 178 — kipande 4

Saa ilifika ! Siku hiyo ya giza

Katika njia ngumu, kabeba msalaba,

Kichwa chako, Yesu, kilivalishwa miiba,

Na uka Tukanwa pia kulaumiwa !

Uliachwa kwetu kwa muti wa Kalvari,

Kapata uchungu, azabu juu yetu.

Uliazibiwa sana juu ya zambi ;

Uka Tuokoa ! Tunakubariki !

Wimbo 178 — kipande 5

Twataka tuimbe maishani mwetu mwote

Pendo hili nzuri, lipitalo vyote !

Na tukigeuzwa kwa nguvu ya milele,

Tutaifikia siku ya uamsho,

Macho yetu sisi yatakuona kuzoni,

Ee Yesu, Mwokozi, uu Rafiki wetu,

Wako kwa miguu, wata Tupia taji,

Wakikuabudu ! Tunakubariki.

 

179.             Wimbo 179

Wimbo 179 — kipande 1

Yesu anapenda,

Yeye mwenyewe

Kutubeba.

Yesu aja,

{Matumaini

Ya waamini !} (bis)

Wimbo 179 — kipande 2

Huko nyumbani

Mwa Baba yetu,

Tuingie

Na furaha

{Katika nuru

Ya mbinguni !} (bis)

Wimbo 179 — kipande 3

Kazi imekwisha ;

Makao yapo.

Kifuani

Bwana arusi

{Tulaze sote

Vichwa vyetu !} (bis)

Wimbo 179 — kipande 4

Na itulie,

Bila mwengine

Ila wewe,

Na kuweza,

{Nyuma ya vita

Kukuona !} (bis)

Wimbo 179 — kipande 5

Wewe uliye,

Ee Bwana mtukufu,

Kwa hakika

U milele

{Ni kuelewa

Pendo lako !} (bis)

 

180.             Wimbo 180

Wimbo 180 — kipande 1

Usikie kanisa pendwa

Bwana aja

Taa zetu ziwe tayari

Bwana aja

Saa sita za usiku hizi

Hatujaona hata mutu

Aangazia mioyo yetu

Bwana aja.

Wimbo 180 — kipande 2

Tunaisikia sauti

Ona Bwana

Hakuna  giza na kukesha

Ona Bwana

Na sasa hivi baragumu

Yatualika kwa karamu

Asema : « kanisa tayari ? »

Ona Bwana.

 

181.             Wimbo 181

Wimbo 181 — kipande 1

Furaha ikasikika mbinguni

Wakati sauti ya muweza

Ilipo towa nuru.

Alipoumba mbingu kwa mkono

Akionyesha uwezo wake

Akaumba ulimwengu.

Wimbo 181 — kipande 2

Furaha ikasikika mbinguni

Hapa chini, Yesu, Emanueli

Akazaliwa mnyonge!

Malaika waliimba sifa,

Salama duniani, sifa juu

Walijaa raha tele.

Wimbo 181 — kipande 3

Furaha ikasikika mbinguni

Mwenye zambi asikiapo sauti

Ya Mwokozi akiita

Zambi zake zimeondolewa

Yesu amupa uzima, salama

 Anamulinda kifuani.

Wimbo 181 — kipande 4

Furaha gani na shangwe juu

Wakati waamini wa milele

Watakuja kuketi

Karibu na Yesu kwa furaha

Wataimba pendo lake njema

Na neema yake nzuri.

 

182.             Wimbo 182

Wimbo 182 — kipande 1

Chemchemu ya nuru, uzima

Ya neema kwa imani

Pumziko, uheri, salama

Tulipata ndani yako.

Wimbo 182 — kipande 2

Chemchemu ya pendo iliyo mpya

Kutoka patakatifu

Watujaza chemchemu nzuri

Na uwepo wa milele.

Wimbo 182 — kipande 3

Heri aliye karibu na mto

Amepandwa muti hai

Wanywa maji na unaota

Wakomaa kwa milele.

Wimbo 182 — kipande 4

Wazaa matunda, wasitawi

Wapata nguvu kabisa

Heri yule, hapa duniani

Anywaye kwa chemchemu hii.

 

183.             Wimbo 183

Wimbo 183 — kipande 1

Chemchemu ya neema hai

Mwaminifu, muchungaji

Pendo lako halina mwisho

Wewe haubadiliki

Hata kama twajaribiwa

Na kushambuliwa pia

Unapatia nafsi zetu

Tumaini, imani, pendo.

Wimbo 183 — kipande 2

Mwisho wa vyote ni karibu

Vizuri havisitawi

Umilele wakaribia

Majaribu ya dunia

Yatageuka kuwa mema

Ya pumziko ile kubwa

Imani pia tumaini

Vitakwisha, upendo la !

 

184.             Wimbo 184

Wimbo 184 — kipande 1

Ninaleta sifa nikitazama

Mbingu, hii kazi yako ya ajabu,

Mawingu, mwezi na nyota zote

Ulizoziweka kwa mustari.

Wimbo 184 — kipande 2

Nasema mwenyewe nikishangaa :

Mtu ni kitu gani, ee Mfalme mkuu

Ili uweze kumukumbuka

Na neema yako kumuarifu ?

Wimbo 184 — kipande 3

Akafanywa chini ya malaika

Wanaozitangaza sifa zako

Ukamvika utukufu pia

Hata kuzungukwa na heshima.

Wimbo 184 — kipande 4

Umemupa kutawala viumbe

vilivyoumbwa kwa mkono wako.

Katika mipango yako, Bwana,

Vyote vitakuwa chini yake.

 

185.             Wimbo 185

Wimbo 185 — kipande 1

Eh kuja Bwana

Kwani dunia hii

Ijaamo zambi

Kwa roho yangu

Haitaleta

Pumziko, amani

Asubui yaja

Kuja kunitwaa

Ninakuhitaji

Pumziko langu.

Wimbo 185 — kipande 2

Kondoo mwema

Nitakutazama

Ukingaa neema

Na usalama

Upendo wako

Paradizoni

Nyumba yake Baba

Atanimwangia

Nuru yake pole

Pumziko langu.

Wimbo 185 — kipande 3

Pumziko njema

Kutoka pendoni

Utafurahisha

Hata milele

Heri ijayo

Kukubariki

Na kukufanana

Utanipa vyote

Mwokozi mupendwa

Pumziko langu.

 

186.             Wimbo 186

Wimbo 186 — kipande 1

Pendo la Mwokozi, kisima kishukacho

Kinanituliza, (bis)

Hakuna kiwezacho kufunga maji

Nitaonja daima uzuri wako Bwana

Pendo la Mwokozi. (bis)

Wimbo 186 — kipande 2

Pendo la Mwokozi, watosha nafsi yangu

Pumziko, uheri, (bis)

Nina vyote kwako, naota moto wako

Nitavumilia jaribu na kemeo

Pendo la Mwokozi. (bis)

Wimbo 186 — kipande 3

Pendo la Mwokozi, nitatazama wazi

Utukufu wako, (bis)

Nyumbani mwa Baba, kwa mwisho wa safari

Nitakutazama na kukuza milele

Pendo la Mwokozi. (bis)

 

187.             Wimbo 187

Wimbo 187 — kipande 1

Nyumbani mwa Baba, tutakuwa pamoja

Ee Yesu Mwokozi uliye jitoa

Niwe nawe Mungu wa upendo na nuru

Milele na wewe ! (bis)

Wimbo 187 — kipande 2

Mjini mtakatifu sifa yako yaangaza

Wako wanakutazama kwa imani

Nitaonja tunda ya neema yako kubwa

Milele na wewe. (bis)

 

188.             Wimbo 188

Wimbo 188 — kipande 1

Ee Mwokozi, wewe uzima,

Na nilipokukimbia,

Sauti yako ikaniita

Kwa karamu ya Mufalme.

Na tangu sasa, mbele yako,

Umeniosha kwa damu,

Ninaonja neema nzuri

Ya Mungu Mwokozi wangu.

Wimbo 188 — kipande 2

Kwa wakati huu wa magumu,

Kwa kunipatia nguvu

Na kuniongoza kwa ukingo,

Muchungaji wanitunza.

Mabaya yasongapo mbele,

Tukungojapo urudi,

Ninakubariki kwa pendo,

Matunzo ya pendo lako.

Wimbo 188 — kipande 3

Punde, nyumbani mwake Baba,

Utatupokea sisi,

Ili tuone siri kubwa

Ya neema na pendo lako.

Na sasa malangoni mwako,

Pamoja na kundi lako,

Nitasifu katika nyimbo

Sifa zote za Kondoo !

 

189.             Wimbo 189

Wimbo 189 — kipande 1

Heri gani kukujua

Usiye badilika

Mwokozi, mwalimu wangu

Musaidia, mchungaji.

Wimbo 189 — kipande 2

Sitapungukiwa kamwe

Wajibu mahitaji

Nalindwa na gongo lako

Ninajiacha kwako.

Wimbo 189 — kipande 3

Katika bonde la giza

Unanikaribia

Nina farijika mimi

Kuwa karibu nawe !

Wimbo 189 — kipande 4

Kwa pahali pa mbinguni

Nitaingia  hapo

Ili nikuone nuruni

Mchungaji wa uwezo !

Wimbo 189 — kipande 5

Heri gani kukujua

Usiyebadilika

Mwokozi, mwalimu wangu

Mchungaji wangu mwema !

 

190.             Wimbo 190

Wimbo 190 — kipande 1

Katika jangwa kubwa

Bila njia kamwe,

Anayeniongoza,

Naye alipita

Kwa Baba ananileta

Ni furaha yangu

Hakuna kitu hapa

Cha kunishawishi.

Wimbo 190 — kipande 2

Ninamutegemea

Namfuata kwa bure,

Wala kwa kupoteza,

Akinifaidia ?

Vitu vya ulimwengu

Vyataka nifunga

Uwezo wake mkubwa

Wanitoa hapo.

Wimbo 190 — kipande 3

Heri aliye huru,

Njiani mwa mbingu

Ninaungana sasa

Kwa wimbo milele

Uchungu na tatizo,

Havitetemeshi.

Jaribio linajaa

Matokeo mema.

Wimbo 190 — kipande 4

Kwa njia ya saa moja

Ninapotembea,

Kama nanungunika

Nitakata tamaa ?

Sivyo, neema yake

Ndiyo kimbilio,

Gongo na fimbo yake

Vitanifariji.

Wimbo 190 — kipande 5

Yesu chakula changu

Nilacho duniani,

Nikipiga hatua

Unanipa nguvu.

Kwakufanana nawe,

Nitakutazama

Katika utukufu

Na nitakusifu.

 

191.             Wimbo 191

Wimbo 191 — kipande 1

 

192.             Wimbo 192

Wimbo 192 — kipande 1

 

193.             Wimbo 193

Wimbo 193 — kipande 1

 

194.             Wimbo 194

Wimbo 194 — kipande 1

« Nakuja upesi : ngojeni kuja kwangu »

Asema Mkombozi aliyetupenda.

Aleluya ! Aleluya ! (bis)

Kuja, Bwana Yesu, (ter)

Juu ya wingu nyeupe.

Wimbo 194 — kipande 2

Dunia na mwili, mpinzani wetu mkubwa,

Maadui wote, umetushindia ;

Aleluya ! Aleluya ! (bis)

Kuja, Bwana Yesu, (bis)

Tunayetumaini.

Wimbo 194 — kipande 3

Hapa duniani tupo majaribuni,

Ila juu mbinguni hakuna tatizo

Aleluya ! Aleluya ! (bis)

Kuja, Bwana Yesu, (bis)

Kutwaa Kanisa lako.

 

195.             Wimbo 195

Wimbo 195 — kipande 1

Tumwendee nani ? dunia hii ni mbovu

Kao la shetani, jangwa danganyifu

Twataka kujenga nyumba zetu mchangani ?

Hapana, si hivyo uheri ujavyo.

Wimbo 195 — kipande 2

Tumwendee nani kwa kupata ujuzi

Wa Mungu wa kweli, wa nuru na pendo ?

Nani atatoa salama, uhakika,

Tunapotembea na tukilemewa ?

Wimbo 195 — kipande 3

Tumwendee nani ? chemchemu mpya daima

Inayotuliza kiu ya mioyo,

Neno lako, Bwana, uzima wa milele :

Tunalinywa tukikuabudu wewe.

Wimbo 195 — kipande 4

Tumwendee nani ? Sauti yako tamu

inatuambia : Musiwe na hofu :

unatufariji, waondosha machozi

Tumwendee nani ?, wewe pekee tu.

 

196.             Wimbo 196

Wimbo 196 — kipande 1

 

197.             Wimbo 197

Wimbo 197 — kipande 1

 

198.             Wimbo 198

Wimbo 198 — kipande 1

Twavuka bahari mbio,

Tu wenyeji wa mbingu.

Mapambazuko yakuja

Mchana waonekana.

Wimbo 198 — kipande 2

Mutazame : bado ngambo

Yaonekana mbali ;

Rafiki tujipe moyo

Pumziko ni hakika.

Wimbo 198 — kipande 3

Tufani ikitutisha

Tusiogope hatari ;

Safarini tupo naye

Abiriya wa juu ;

Wimbo 198 — kipande 4

Shimo saliti la wimbi,

Fasi ya kuzamisha,

Bwana anaikomesha ;

Na sasa tunavuka.

Wimbo 198 — kipande 5

Ni furaha kubwa gani !

Tutakapomuona,

Na wakati pendo lake

litatuvika sisi !

Wimbo 198 — kipande 6

Mutazame bado ngambo

Yaangaza asubui ;

Rafiki tujipe moyo,

Tumepata pumziko !

 

199.             Wimbo 199

Wimbo 199 — kipande 1

 

200.             Wimbo 200

Wimbo 200 — kipande 1

Moyo wangu watamani kuwa nawe daima

Nikipupa natamani wakati utarudi

Ninaimba na wako:

”Amina ! Bwana kuja !”

Wewe ni hazina yangu,

Ni wewe nihitajiye.

Wimbo 200 — kipande 2

Ayala atakavyo kunywa

Sana maji ya mito,

Hivyo katika jangwa hii

Nakutamani wewe,

Ninaimba na wako:

« Amina ! Bwana kuja ! »

Itakuwa siku gani

Nitakapo kuona wewe ?

Wimbo 200 — kipande 3

Kufurahia neema,

Kutukuza mapendo,

Kukuona uso kwa uso,

Kuwa nawe milele

Yanituma kusema:

« Amina, Bwana kuja ! »

Ujibu kwa ombi langu,

Kwani ninakuhitaji.

 

201.             Wimbo 201

Wimbo 201 — kipande 1

Ndugu, tujipe moyo !

Punde tutaona

asubui ingaayo :

Kwa pwani ya milele

Sisi tutafika. (bis)

Wimbo 201 — kipande 2

Hapa chini zoruba,

Hapa chini ziki,

Hatuna pumuziko :

Fasi yakujikinga

Kwa mioyo yetu. (bis)

Wimbo 201 — kipande 3

Kwa moyo mutiifu

Ni bandari nzuri ;

Ni pumuziko kimya,

Na Kimbilio kimya

Kwa nguvu ya Mungu. (bis)

Wimbo 201 — kipande 4

Ndugu, tujipe moyo !

Punde tutaona

Asubui ingaayo :

Kwa pwani ya milele

Sisi tutafika. (bis)

 

202.             Wimbo 202

Wimbo 202 — kipande 1

Kwa moyo mkunjufu, kwa nafsi ichokayo

Yesu, kwa mapendo ni pumziko tamu,

Pumziko idumuyo neemani mwake

Iliyotutafuta na kutupumzisha.

Wimbo 202 — kipande 2

Twapata pumziko tunapogunja vichwa,

Muabudiwa wetu, kwa nira ya pendo,

Twafundishwa nawe pia na neema yako,

Kubeba muzigo tukiuvumilia

Wimbo 202 — kipande 3

Pumziko ya mbingu ! Tumeipata hapa

Tukifuata njia, inayoangaza,

Ituongozayo kwako katika nuru,

Kwenye pumuziko letu wakombolewa.

 

203.             Wimbo 203

Wimbo 203 — kipande 1

Nafsi usiogope wakati wa mateso

Bwana ni mwamba na nguvu yako pia

Inua macho juu : ni ukombozi wako

Hatakuacha kamwe : ee nafsi  tulia.

Wimbo 203 — kipande 2

Yanipasa vita, kujaribiwa pia

Kusafishwa kama zahabu chomboni,

Kupitia moto ama kuvuka mito,

Yu Mwokozi wangu, kiongozi, hazina.

Wimbo 203 — kipande 3

Na sitaogopa shetani na dunia

Hawataninyanganya mchungaji wangu.

Hapo kwa amani naonja pendo kubwa ;

Ninalindwa toka hatari daima.

 

204.             Wimbo 204

Wimbo 204 — kipande 1

Inchini mwangu, kule kwako

Roho ananiongoza

Bila woga ninakufwata

Kila siku hadi mwisho

Wimbo 204 — kipande 2

Anipa nguvu pia moyo

Kati njia ya mbinguni,

Punde kwa mwisho wa safari,

Nitakuona Emanueli.

Wimbo 204 — kipande 3

Ila katika njia hii,

Fujo haitanizuru,

Kwa kimya nafsi yasikia

Sauti ya Roho wako.

 

205.             Wimbo 205

Wimbo 205 — kipande 1

 

206.             Wimbo 206

Wimbo 206 — kipande 1

Bwana utuongoze, fungua njia zetu,

Mungu wa salama,

Tuna karibu nawe chemchemu ya furaha,

Wakati wowote. (bis)

Wimbo 206 — kipande 2

Tunapojikuta, tukikosa msaada,

Hatari ikija,

Tunakukimbilia pale ulipo wewe,

Bwana utuongoze. (bis)

Wimbo 206 — kipande 3

Bwana utuongoze, tukiwa na ushindi

Tupumzike kwako,

Tuongozwe na wewe katika utukufu,

Kwa imani yetu. (bis)

 

207.             Wimbo 207

Wimbo 207 — kipande 1

 

208.             Wimbo 208

Wimbo 208 — kipande 1

Bwana ninapotazama

Kazi ulizofanya,

Mbingu ni hekalu lako

Lifunikalo watu.

Wimbo 208 — kipande 2

Nionapo jeshi kubwa

Nyota za juu mbinguni,

Ushikazo kwa uwezo

Katika njia zao.

Wimbo 208 — kipande 3

Mimi kweli ni mudogo

Si kitu mbele yako,

Najisikia munyonge,

Ee muumbaji muweza.

 

209.             Wimbo 209

Wimbo 209 — kipande 1

 

210.             Wimbo 210

Wimbo 210 — kipande 1

 

211.             Wimbo 211

Wimbo 211 — kipande 1

« Imekwisha. » ni kazi ya neema

Ushindi wapandisha sauti

Mwenye kufa akainamisha kichwa

Alishinda. Imekwisha.

Wimbo 211 — kipande 2

Aliteswa. Yeye akajitoa

Mungu akamufurahia sana

Akakuzwa naye akamupa sifa

Mkamilifu. Imekwisha.

Wimbo 211 — kipande 3

Mupotevu katika umaskini

Kaondoshwa zambini na Yesu.

Malipo makali akayatoa

Aliteswa. Imekwisha.

Wimbo 211 — kipande 4

Kutoka juu Mungu akapasuwa

Ile pazia njia ikawekwa,

Mpya mupaka kwa makao mbinguni

Kwa milele. Imekwisha.

Wimbo 211 — kipande 5

Mbingu mupya hata dunia mupya

Vyote vitaimba sasa kwa upendo.

Sifa kwa Mungu, na Mwana, na Baba !

Kwa milele. Imekwisha.

 

212.             Wimbo 212

Wimbo 212 — kipande 1

Sasa, sifa zako zafwata,

Uchungu uliyopata

Mbinguni kwa wakombolewa,

Waonekana Mtukufu. (bis)

Wimbo 212 — kipande 2

Mwili wetu, hema legevu,

Twateseka, twalemewa

Twatarajia jengo letu

Tutakalo vaa kuzoni. (bis)

Wimbo 212 — kipande 3

Kupitia chozi na teso

Twakusikia toka juu,

Julisho la heri ijayo,

Lisemalo : « Ninakuja ». (bis)

Wimbo 212 — kipande 4

Kwa upendo na tumaini

Jibu la wachaguliwa

Lapanda kupitia Roho :

« Amen, kuja, Bwana Yesu ! » (bis)

 

213.             Wimbo 213

Wimbo 213 — kipande 1

Ulipohukumiwa,

Kati ya waovu,

Fimbo za haki yake

Zilikulemea.

Kosa lako ni gani ?

Kwa nini kupigwa ?

Kondoo takatifu,

Hukuwa na kosa.

Wimbo 213 — kipande 2

Ulikuja kuokoa;

Watu wakakataa,

Na yote tumekuwa

Ilionekana.

Dunia ilikutesa,

Ikakuzarau,

Katika ziki kubwa,

Moyo kavunjika

Wimbo 213 — kipande 3

Saa ilipofika

Ukaachwa pekee,

Mungu Mutakatifu

Akakuacha wewe.

Siri ishangazayo,

Wewe mpenzi wake,

Ukapata gazabu

Yake kali sana.

Wimbo 213 — kipande 4

Mwokozi Muabudiwa,

Kafungwa mutini,

Ukafia waovu,

Kaondosha zambi,

Kavumilia teso

La makosa yetu ;

Katufungua sisi,

Katupa salama.

Wimbo 213 — kipande 5

umemaliza kazi

Mungu ametosheka,

Umeivikwa taji,

Ushindi kamili.

Kwako sifa uwezo,

Heshima ukuu,

Hata mashukurani

Kwa milele yote.

 

214.             Wimbo 214

Wimbo 214 — kipande 1

Mwana wako, ee Baba wetu,

Juu mbinguni na duniani,

Yeye ni furaha yako,

Yesu akajitoa kwetu

Mupendwa wako kila siku,

Amepewa heshima kuu ;

Tunaona kwa uso wake

Kukingaa utukufu,

Uonyeshao neema yako,

Ufunuo wako wote.

Wimbo 214 — kipande 2

Mbele ya dunia kuumbwa,

Uliweka kando, kwa neema,

Mwana Kondoo bila taka.

Alipata hukumu yetu,

Na hapo manukato bora

Yalipanda mbele yako !

Mupendwa wako, kajitoa,

Katimiza mpango wako ;

Msalabani, akamaliza

Kazi, akakutukuza.

Wimbo 214 — kipande 3

Ametukuzwa hekaluni,

Kuume kwako, Baba wetu,

Ameketi na ushindi.

Punde 'tanyakua Kanisa

Alilinunua kwa bei

Talipeleka mbinguni.

Kando yake, kwa utukufu

Litangaa sifa zake

Na litaimba kwa ushindi

Katika milele yote.

 

215.             Wimbo 215

Wimbo 215 — kipande 1

Mungu, tunatangaza sifa,

Za aliye shuka hapa

Kuanza historia yetu,

Akikutii kwa yote. (bis)

Wimbo 215 — kipande 2

Ni jambo lakukupendeza,

Mwana wako muabudiwa !

Ndani yake tunatazama

Sifa zako bila mwisho. (bis)

Wimbo 215 — kipande 3

Alikuwa mwenye huruma,

Mnyenyekevu, msaidia ;

Alipokuwa akitembea

Alikuwa mkubwa sana. (bis)

Wimbo 215 — kipande 4

Katika kufa na kuishi,

Alikupendeza wewe,

Alipokuja, neema tele,

Kutumika na kukufa. (bis)

Wimbo 215 — kipande 5

Alikataliwa duniani

Mutu alimsulubisha

Ingawa alikutukuza

Ulimutukuza vile. (bis)

Wimbo 215 — kipande 6

Punde katika neema yako

Tutapata pumuziko,

Tutauona uso wake,

Nakumuabudu milele. (bis)

 

216.             Wimbo 216

Wimbo 216 — kipande 1

Kunakuja, Bwana, siku katika kuzo

Tutakapoonyeshwa mbele ya Baba ;

Na utafurahia tunda la ushindi,

Tutakapo kuzunguka. (bis)

Wimbo 216 — kipande 2

Tukiwa kuzoni – Bibi arusi amevikwa –

Kwa karamu yako, utatuingiza,

Utatuketisha ulipotayarisha,

Utakuja kutulisha. (bis)

Wimbo 216 — kipande 3

Malangoni pa juu, mwisho tungojeao,

Ambapo milele ulitaka watu,

Tutautazama uso wako muzuri,

Machapa mkononi mwako. (bis)

Wimbo 216 — kipande 4

Tutakapoona utajiri wa neema,

Hazina ambayo isiyo na mwisho,

Sifa na muhuri wa ahadi za Mungu,

Yesu, utazifunua. (bis)

Wimbo 216 — kipande 5

Asifiwe Mungu ! Na wewe Mwana wake,

Usifiwe Mwana wa watu, Kondoo !

Bwana, tupatie kuangaza duniani

Picha za patakatifu. (bis)

 

217.             Wimbo 217

Wimbo 217 — kipande 1

Siku ya huzuni, Mungu akakuacha !

Siku ya haya na mchanganyiko,

Ukalipa pahali petu, Bwana,

Bei ya ukombozi wetu.

Wimbo 217 — kipande 2

Ulitafuta pendo, mapatano,

Ila wako hawakukujali

Walikuzihaki na kukukana

Haukupata hata mfariji.

Wimbo 217 — kipande 3

Ulinyamanza katika mateso,

Wakati mbele yako maadui

Walipokuwa wakikutukana

Lawama ikakuchana moyo.

Wimbo 217 — kipande 4

Ulipo kunywa kikombe kikali

Ulisema : « Yote imekwisha ».

Mushindaji ! Mikononi mwa Baba,

Kwa salama, ukatoa roho.

Wimbo 217 — kipande 5

Mwokozi mwema, juu ya malaika,

Mungu, akitosheka, alikuinua,

Toka duniani, twaimba sifa,

Na kwa magoti tunakuabudu.

 

218.             Wimbo 218

Wimbo 218 — kipande 1

Twakuabudu, Bwana wa sifa,

Uliye tukuzwa juu ya mbingu.

Tunatangaza, Mungu mshindi

Jina tukufu daima,

Tunakutukuza, wewe pekee yako,

Sifa kwako juu mbinguni.

Wimbo 218 — kipande 2

Mfalme, uvikwaye uwezo,

Utarudi ukiangaa,

Ulikuwa hapa, matesoni,

Ulikataliwa na watu !

Utukufu kwako

Kwa Wewe mwenyewe,

Sifa kwako kwa milele.

Wimbo 218 — kipande 3

Ee Yesu, Bwana wa uzima,

Ulipigiliwa mtini,

Katika mateso makubwa,

Ulikufa musalabani !

Utukufu kwako

Milele yote,

Nyimbo na mioyo vipande.

Wimbo 218 — kipande 4

Ukiangaa kwa nuru kubwa,

Utaonekana wazi,

Mbinguni hata duniani,

U Mufalme, Kristo Bwana.

Hivi nafsi zetu,

Zinakutangaza

Mwana wa Mungu, Mkombozi.

 

219.             Wimbo 219

Wimbo 219 — kipande 1

Barikiwa, Mwokozi mwema

Uliye tutembelea

Ukifunika utukufu

Hata kufanana mutu.

Wimbo 219 — kipande 2

Wewe mubebaji wa mbegu

Ulizipanda kwa chozi,

Ukapata mateso, Yesu

Katika kujitolea.

Wimbo 219 — kipande 3

Mbegu ya ngano udongoni,

Ikifa, iandikwavyo,

Haitabaki pekee yake

Ila itazaa matunda.

Wimbo 219 — kipande 4

Mavuno sasa ni tayari

Mbele yako, mupandaji ;

Utarudi, ukiimba raha,

Ukiyashika masuke.

Wimbo 219 — kipande 5

Utaonekana kwa sifa

Sisi Tukikuzunguka,

Sisi matunda ya ushindi,

Tukikusanywa milele.

 

220.             Wimbo 220

Wimbo 220 — kipande 1

Wana wa neema ya Mungu

Twaweza kuja kwa Baba,

Tukifurahi mbele yako,

Tukikutukuza wewe.

Kwa Yesu Kristo, tumaini

Ni vema tukuletee

Ushuru wa mashukurani

Tukuinuwe pamoja.

Wimbo 220 — kipande 2

Giza ya taabu na woga

Ilitumeza milele,

ukatuangazia pia

Na tukapewa amani

Kazi ya neema imetimia,

Tunaona Mukombozi

Akivaa utukufu tele

Alipotutangulia.

Wimbo 220 — kipande 3

Tunda la ushindi milele

Yesu ametuokoa

Twamuona utukufuni

Ambapo umempokea

Tukuabudupo hekaluni

Tuingiapo kwa imani,

Mungu Mweza, Baba wetu 

Twainama mbele yako.

Wimbo 220 — kipande 4

Punde, mbinguni, kwa vizazi,

Tukiimba wimbo mupya,

Wakombolewa wataabudu

Mbele ya Mwana Kondoo.

Wakifurahi mbele yake,

Na kushangalia Yesu,

Na Watatangaza uwezo

Nakusifu wema wake.

 

221.             Wimbo 221

Wimbo 221 — kipande 1

Twastaajabia ufunuo wa Baba,

Kwa Mipango ya Mungu Mwokozi,

Aliyefanya uumbaji mupya

Mpango wa moyoni

Wimbo 221 — kipande 2

Mbele zambi iingiye duniani,

Kondoo alikuwa mbele yako,

Baba milele, hekima ya ajabu

Shauri la fumbo !

Wimbo 221 — kipande 2

Yesu kajitolea kwa zabihu

Akaleta salama kwa damu ;

Apitiaye Kwake aona Mungu,

Kwake wampokea

Wimbo 221 — kipande 3

Utukufu kwa Yesu malimbuko,

Aliyefufuka na ushindi !

Ameketi juu, ni furaha yako

Adamu wa mwisho.

Wimbo 221 — kipande 4

Ulimwengu wote unateseka

Siku moja utakuwa huru ;

Kristo ndiye chanzo cha ukombozi

Toka ubatili.

Wimbo 221 — kipande 5

Mungu ndani ya yote, tumaini !

Salama ya muji mtakatifu !

Utajaza wako na uepo wako,

Siku ya milele.

Wimbo 221 — kipande 6

Tukikuabudu sasa duniani,

Mwana Kondoo mushindi atukuzwa,

Twakusifu, Mungu na Baba wetu,

Kwa zawadi yako.

 

222.             Wimbo 222

Wimbo 222 — kipande 1

Huru kwa furaha, watoto kwa Babao,

Kwa ushirika wako, wapendwa wako,

Waweza kuonja, katika nuru yako,

Utamu wa upatanishi wa neema.

Wimbo 222 — kipande 2

Twafika mbinguni, umetukubaliya,

Pamoja sote twaja kukuabudu,

Tukikutolea shukurani kwa Yesu,

Sifa ambayo pendo lilitupatia.

Wimbo 222 — kipande 3

Ulitaka wana pamoja naye Yesu:

Baba, ulituleta kwako milele

Na uzima wetu ni ndani ya mupendwa,

Yesu mbinguni, Mutu aliyefufuka.

Wimbo 222 — kipande 4

Sote ndani yake, tunakuabudu wewe,

Tukitangulia siku ya milele,

Tutamufanana Kristo aliyetukuzwa,

Milele mbele yako katika heri.

 

223.             Wimbo 223

Wimbo 223 — kipande 1

Nani aweza kueleza,

Mateso ulivumilia

Kwa pendo vile utiifu,

Ukuongozao Golgota,

Na huzuni yako ya ajabu,

Ulipokuwa ukiomba,

Mwokozi kwa mateso yako,

vitani mwa Getsemane !

Wimbo 223 — kipande 2

Kutangulia saa ile,

ulipata woga, taabu,

Ukiomba, ikiwezekana,

Kikombe kikupitiye.

« Ila mapenzi yako yawe ! »

Kukubali kwa ajabu

Kwa Mwokozi asiye zuizwa,

Yote kwake ni kamili !

Wimbo 223 — kipande 3

Ulija kutukuza Baba,

Hadi kifo ukafika ;

Ndani yako alifurahi,

Mpendwa wake mnyenyekevu.

Twakutolea sifa, Bwana ;

Tukiona bidii yako ;

Tutakutukuza milele

Nakujitolea kwako.

 

224.             Wimbo 224

Wimbo 224 — kipande 1

Twainua, Mungu, Mwana wa pendo lako,

Ulimupenda milele na milele ;

Kwa kukutukuza, alijitoa yeye :

Ili ayatimize mapenzi yako.

Wimbo 224 — kipande 2

Mwana wa milele, ni mukubwa zaidi,

Kama vile Mungu, alipewa vyote,

Ila akajishusha, na akanyenyekea,

Alikutukuza, hadi msalabani.

Wimbo 224 — kipande 3

Mwana wa watu alihangikwa mutini,

Sadaka iliyopita katika moto,

Mupendwa wako akajitoa mwenyewe

Zabihu kamili, kwake Baba Mungu.

Wimbo 224 — kipande 4

Ulitosheka na hii sadaka nzuri

Ya Mwana Kondoo, bila hata taka :

Kujitoa kwake, na utiifu wake,

Ni manukato ipandayo juu kwako.

Wimbo 224 — kipande 5

Alipojitoa, sadaka takatifu,

Kristo alikuonyesha wewe vema,

Kwa Mungu wa haki anayeomba sifa,

Alilitukuza pendo lako nzuri.

Wimbo 224 — kipande 6

Tumefufuliwa, tu wapendwa kwa yeye,

Baba, twazitukuza shauri zako.

Twafungwa na mpendwa kwa neema yako nzuri

Twakuabudu sasa pahali pa juu.

 

225.             Wimbo 225

Kwa anayetupenda, na aliyeosha zambi zetu kwa damu, kwa damu tu ;

– na akatufanya tuwe ufalme, wa makuhani wa Mungu Baba ; –

Tumupe heshima, kwake pia nguvu, katika milele.

Amen ! Amen !

 

226.             Wimbo 226

Wimbo 226 — kipande 1

Tupatie Bwana

Utakatifu

Tuwashie moto,

Ututulize ;

Leta tumaini

Tuwe imara

Tukivumilia

Kila jaribu.

Wimbo 226 — kipande 2

Tupe kutazama

Mwana Kondoo,

Mfano na msalaba,

Kaburi lake,

Neema aminifu,

Mapendo yake,

Utukufu wake,

Kurudi kwake.

Wimbo 226 — kipande 3

Kwa machozi yetu

Watusaidia,

Watuvika sisi

Silaha zote.

Na katika nuru

Tutembee nawe,

Hata tukiomba,

Twaishi sisi.

Wimbo 226 — kipande 4

Tufundishe sisi

Kwa kazi yako,

Na tuwe tayari

Usoni mwako

Tuimbe na kushuka,

Kwa bidii kuu ;

Mioyo ifanane

Wako, Mwokozi.

 

227.             Wimbo 227

Wimbo 227 — kipande 1

Yesu atuletea

Wokovu waamini ;

Asema : « mimi mlango,

Muingiye kwangu ».

Kutuongoza kwa Baba,

Alifa mutini,

Na sasa duniani

Twamjua sauti.

Wimbo 227 — kipande 2

Kwa kondoo apendazo

Yeye ni Mchungaji :

Azilinda mwenyewe

Hata kuzikinga.

Azipapo uzima

Ni milele yote ;

Uwezo wake mkubwa

Ni ukingo wao.

Wimbo 227 — kipande 3

Hakuna atakaye

Nitosha mkononi ;

Mwokozi atuongoza

Katika njia nzuri.

Aonapo unyonge,

Atuhakikisha,

Na matunzo ya pendo

Anatuzungusha.

Wimbo 227 — kipande 4

Tuonje kwa uepo wake

Muchungaji mkubwa,

Uwingi wa uzima

Atupatiao ;

Tukimutegemea,

Twatembea huru,

Na tuufurahie

Uepo wake nasi.

 

228.             Wimbo 228

Wimbo 228 — kipande 1

Hakuna duniani, muji unaodumu,

Ambamo twaweza kaa, (bis)

Makao duniani ni hema bila nguvu

Iangushwayo na upepo.

Wimbo 228 — kipande 2

Hakuna duniani, muji unaodumu,

Muji wetu ni mbinguni, (bis)

Punde tutasikia sauti ya nguvu,

Sauti yakuondoka.

Wimbo 228 — kipande 3

Hakuna duniani, muji unaodumu,

Tutaupata baadaye, (bis)

Tuungojeapo, imani yauleta

Mioyo yaufurahia.

Wimbo 228 — kipande 4

Punde muda mdogo, wa kazi na kungoja…

Milango itafunguka, (bis)

Muji wa Mungu hai, wa juu, udumuo,

Makao ya wateule.

 

229.             Wimbo 229

Wimbo 229 — kipande 1

Neno lako ni utajiri,

Ni kweli iliyo hakika,

Tayari kwa unyonge wetu

Katika ukubwa wake.

Wimbo 229 — kipande 2

Mungu, Neno lako laficha

Hazina damani sana,

Kwani Roho afunua humo

Yesu, njia moja ya juu.

Wimbo 229 — kipande 3

Neno lako, ujumbe hai,

Unaoleta uheri,

Salama, raha na bidii

Tumufwatapo Mwokozi.

Wimbo 229 — kipande 4

Neno lako ni nuru safi,

Ituongozayo sisi

Ili tuweze, Baba Mpendwa,

Kukutukuza duniani.

Wimbo 229 — kipande 5

Neno, kwa Mwanako mwenyewe

Linataka kutufunga,

Lionyeshapo sifa zote

Za Mwokozi, Bwana wetu.

 

230.             Wimbo 230

Wimbo 230 — kipande 1

Atakuwaje unyongeni

Mtoto wako,

Asipoweza, zikini,

Kujikinga

Kwa pendo lako aminifu,

Mungu mwema,

Anaweza ishi bawani,

Akilindwa.

Wimbo 230 — kipande 2

Ni mgeni hapa duniani

Haogopi.

Mungu wa pendo na nuru

Amuongoza

Na uepo wako muzuri,

Ee Mwokozi !

Ni msaada wake kwa mateso

Yamujiapo.

Wimbo 230 — kipande 3

Avukapo maji marefu,

Yuko nawe;

Salama tamu umupayo

Yampa nguvu.

Ni uheri kando ya Baba,

Atakuona,

Na uso kwa uso nuruni,

Ataabudu.

 

231.             Wimbo 231

Wimbo 231 — kipande 1

« Neema yakutosha ». Neno lilo tamu !

Latosha kwa yote kuenda hadi mwisho,

Tangulio nzuri ya heri ya ajabu

Tutakayoonja kando yako, Yesu.

Wimbo 231 — kipande 2

« Neema yakutosha ». Kati unyonge wetu,

Twawezeshwa, Bwana, Twapata msaada ;

Unatupa nguvu hata katika taabu,

Unapotutunza na mapendo yako.

Wimbo 231 — kipande 3

Kwa neema yako, nyumbani mwake Baba,

Tutaweza kuonja baraka zako,

Tukikumbuka, juu, siku, hapa duniani,

Ulimotujibu : « Neema yakutosha ».

 

232.             Wimbo 232

Wimbo 232 — kipande 1

Kwa siku za jaribu,

Vita, na mateso,

Mkononi mwake Baba,

Tumwange machozi,

Hivi tusife moyo,

Tumutegemeye.

Tufunzwe kwa magoti

Na Mungu Mukubwa.

Wimbo 232 — kipande 2

Aruhusu mateso

Ili atubariki ;

Kamwe mukono wake

Hautatuvunja.

Tawi asafishalo

Ni lile apendalo,

Ili duniani humu

Lizae matuda.

Wimbo 232 — kipande 3

Adibisho aminifu

Lake Mtakatifu,

Ambamo neema ya juu

Yazaa matunda !

Wafundisha duniani

Watoto wapendwa

Tukuzwa, Baba mpenzi,

Kwa matunzo yako !

 

233.             Wimbo 233

Wimbo 233 — kipande 1

Ee Bwana, gizani kubwa,

Twakuhitaji wewe ;

Tunaonja mema mengi

Kupitia imani.

Huruma yako penzi

Yatuzunguka kila saa,

Moyo wetu wafurika…

Ila hatukuone.

Wimbo 233 — kipande 2

Twakujua bila shaka,

Yesu, kuliko mbele

Ulipofwata safari,

Yakwenda msalabani.

Kanisa lakuhesabu,

Siyo hapa, duniani,

Ila mbinguni, kwa Baba,

Ambapo utatokea.

Wimbo 233 — kipande 3

Imani, jicho la nafsi,

Yapanda juu ya mbingu,

Bibi arusi atazama

Mwokozi mutukufu.

Akishangaa anaabudu,

Akutamani urudi :

Kwa heri yake akosa

Kuwa nawe milele.

Wimbo 233 — kipande 4

Hivi twaweza kungoja

Siku hiyo na nzuri,

Ambapo sauti yako,

Itafufua wafu,

Nakukusanya wahai,

Itatimiza yote

Na tutakwenda pamoja ;

Bwana, tutakuona.

 

234.             Wimbo 234

Wimbo 234 — kipande 1

Kwa ahadi zako, Mungu,

Wako wanapumuzika.

Msaada wao, nguvu yako,

Neema yako, mwamba wao.

Wimbo 234 — kipande 2

Ulitupa yote, Mungu,

Katika Yesu, zawadi.

Kwake twafika mbinguni,

Kwake tunakubariki.

Wimbo 234 — kipande 3

Utuwezeshe kupima

Ukubwa wa pendo lako,

Na sasa, bila kuchoka,

Tunaimba wema wako.

 

235.             Wimbo 235

Wimbo 235 — kipande 1

Unifunze, Bwana,

Kila siku ;

Linda moyo wangu

Kando yako.

Kati njia nzuri

Nitembee mimi,

Nikikutazama,

Ee Mwokozi !

Wimbo 235 — kipande 2

Bwana, matesoni,

Unifunze ;

Juu ya bahari,

Niongoze.

Katika giza kuu,

Unanitazama,

Unaniongoza :

Siogope.

Wimbo 235 — kipande 3

Roho wako, Bwana,

Anifunze

Niweze kuishi,

Kwako Bwana.

Pote hadi mwisho,

Kwa uwezo wako,

Nibaki mkononi,

Mwako Bwana.

 

236.             Wimbo 236

Wimbo 236 — kipande 1

Nani akujuaye,

Mungu milele,

Bwana na Mwalimu,

Mutakatifu ?

Wewe ni mukubwa,

Kuliko mbingu,

Na hakuna kitu

Kikupitacho.

Wimbo 236 — kipande 2

Mbali yako Bwana

Mutu ametengwa ?

Hapana, neema

Ilimtafuta.

Mungu bila mpaka,

Asiyeguswa,

Unatualika

Kukukaribia.

Wimbo 236 — kipande 3

Moyo wako, Baba,

‘Katoa Yesu,

Yesu ndiye nuru,

Pia wokovu.

Kwa damu atakasa

Uovu wetu;

Twapata kuishi

Hadi milele.

Wimbo 236 — kipande 4

Zawadi hii kuu

Ni kwa waamini ;

Ni sehemu gani

Kuwa watoto !

Tunaimba hadi

Kule mbinguni,

Tukikushukuru,

Mungu wa pendo.

 

237.             Wimbo 237

Wimbo 237 — kipande 1

Kwa Mungu, tulia nafsi yangu ;

Yesu yupo, daima na wewe.

Matesoni, majini hata moto,

Pendo lake lataka kukubeba.

Mungu akikufunza na kukupima,

Anakuongoza kwenye heri.

Wimbo 237 — kipande 2

Pumuzika, ukimutumaini,

Muachie Yesu matunzo yako.

Zamani yeye alikusaidia,

Atabaki Kiongozi, Mwokozi.

Kama zamani sauti yake nzuri

Itatuliza mawimbi yote.

Wimbo 237 — kipande 3

Pumuzika, Mungu hakusahau,

Saa yaja Yesu akujapo.

Utafahamu mateso ya maisha,

Utaona kwamba ni baraka.

Hivi Imani yako imuheshimu

Mungu aliyekupenda wewe.

 

238.             Wimbo 238

Wimbo 238 — kipande 1

Sifa kwako Mungu, ulitaka duniani

Waabudu wa kweli wamzunguke Baba !

Kwa kundi lako zamani ulifichama,

kwa damu ya Yesu twakaribia.

Wimbo 238 — kipande 2

Yesu ndiye musingi wa kanisa lake,

Jiwe kuu na hai, alikataliwa,

La samani kwako, la mshangao kwetu.

utukufu, kwake nyumbani mwa Baba !

Wimbo 238 — kipande 3

Tunakusanyika, sisi kwa jina lake,

Wote kwa nia moja, wakuimbia wewe.

Ni hekaluni humu kao la Roho,

Sifa, Ee Mungu, yapanda na kuJaa.

 

239.             Wimbo 239

Wimbo 239 — kipande 1

Baba, tutajua, tukiwa mbele yako

Ulivyomupenda kila muteule,

Tutashukuru neema yako milele

Tulioipokea katika Yesu.

Wimbo 239 — kipande 2

Bila mipango yako hatungeliishi

Kwa imani tunapokea wokovu ;

Tunasifu neema yako bila mwisho

Iliyotuchagua kuwa mbinguni.

Wimbo 239 — kipande 3

Mpango ajabu wa Mungu mwenye hekima :

Kuwa na Yesu katika utukufu !

Tumetayarishwa kufanana na yeye

Katika pendo lako toka milele ;

Wimbo 239 — kipande 4

Hazina kubwa katika fumbo la Mungu

Tutakaloweza kujua daima,

Tukifurahi katika nyumba ya Baba :

Ee Baba, jina lako liinuliwe !

 

240.             Wimbo 240

Wimbo 240 — kipande 1

Sifa ni kwako, Ulifufuka !

Kwako ni ushindi

Milele yote !

Ukingaa nuru,

Na malaika

Alitosha jiwe

La kaburini

Refrain : Bwana mtukufu,

Walio wako

Waimba ushindi

Milele yote.

Wimbo 240 — kipande 2

Salama kubwa,

Yesu yu hai !

Furaha yajaa

Mioyo yetu !

Tukijaa furaha

Twaweza, Bwana,

Tangaza daima

Kwamba yu hai !

Bwana mtukufu, etc.

Wimbo 240 — kipande 3

Tumeketishwa

Kando ya Mungu,

Punde, neema gani !

Utatoka juu.

Wavikwa zahabu,

Mwokozi Mkubwa,

Kitini mwa enzi,

Waheshimiwa,

Bwana Mtukufu, etc.

 

241.             Wimbo 241

Wimbo 241 — kipande 1

Yesu amefufuka, utukufu kwake !

Alitokea wake, nao hawakuamini.

Kuona mikono, mbavu ; kugusa machapa,

Ndipo walisikia sauti hakika.

Wimbo 241 — kipande 2

Kasema : « Amani kwenu » ! na kwa uepo wake,

Wakajaa kushangaa, na furaha kubwa.

Kati wawili, watatu wanaomuabudu,

Yupo kama zamani kwa wamukuzao.

Wimbo 241 — kipande 3

Kristo alishinda kifo : nguvu za milele !

Tunatukuza, Bwana, kazi yako nzuri.

Sadaka ilitosha kwa Mungu mwenye nuru ;

Ushindini twaona sifa yake Baba.

Wimbo 241 — kipande 4

Baragumu italia utakapokuja

Kanisa litajibu kwa sauti yako.

Tukiwa na mwili mpya, tutakufanana,

Tutakuona, Kondoo, Mukombozi wetu.

Wimbo 241 — kipande 5

Yesu, Mukombozi wetu, Bwana wa uzima,

Toka kifo na woga, wewe wafungua.

Kifo, ushindi wako, nguvu yako vipi ?

Pamoja twakuabudu, Bwana mutukufu.

 

242.             Wimbo 242

Wimbo 242 — kipande 1

Kwa imani, twaweza yote

Kwa Mungu wetu Mukubwa ;

Ni jicho lionalo mbali,

Mkono ushikao vipawa,

Na ni utamu uonjao,

Matunda mbele ya siku ;

Inapoivuka jangwa kuu,

Imestarehe nyumbani.

Wimbo 242 — kipande 2

Yapigana bila silaha,

Kupoteza ili ipate,

Kuimba ikimwanga machozi,

Ikiteswa, yatawala ;

Kupanda, ikiona bondeni

Kwa mbali, shamba lakomaa ;

Inatii na kuweza pia,

Imani hii ina haki.

Wimbo 242 — kipande 3

Tangu mababu wa zamani,

Bendera ilipepea ;

Mtazame jeshi kubwa lile

Ambalo lina Kichwa juu ;

Lina historia ndefu sana,

Na hiki kizazi chetu,

Labda, kitaiona sifa,

Nakuvikwa taji lake.

Wimbo 242 — kipande 4

Imani kubwa ya hakika :

Dunia, mauti vyashindwa ;

Sababu ya msimamo wake,

Ni msalaba wake Yesu.

Bado kidogo, mawinguni,

Wakristo, tutasafiri ;

Imani itabadilishwa,

Na tutamuona Yesu.

 

243.             Wimbo 243

Wimbo 243 — kipande 1

Kuna njia ya amani na

Nuru, usalama pia

Tunayopitia duniani

Tukiwa na moyo huru.

Wimbo 243 — kipande 2

Ni nyembamba na takatifu

Huko mbali ya dunia !

Upendo wafukuza woga

Hapo Yesu alipopita.

Wimbo 243 — kipande 3

Ni njia ambayo, duniani

Yatufungulia pendo,

Na uso wake unaangaza

Nuru yazidi daima.

Wimbo 243 — kipande 4

Mpaka wakati tutafika

Mbele ya kiti cha enzi,

Nyumbani munamojaa nuru

Ya Mwana wa Mungu wetu.

 

244.             Wimbo 244

Wimbo 244 — kipande 1

Kama bikira katika mufano,

Bwana Yesu, sisi tunalala !

Wengi wako, wasahau mufano,

Wamekuwa rafiki za dunia

Lakini wote wanahamakiwa,

Twakuita tukipiga magoti !

Ufukuze kutokujali kwetu,

Tuamshe, Bwana, tuamshe !

Wimbo 244 — kipande 2

Tukitafuta mambo ya dunia,

Tumesahau mara na mara

Neno lile, ee kristo, lililo muhimu,

La kuketi na kukusikiliza !

Ila Roho wako asema nasi

Kwamba unakuja, Bwana arusi !

Kwa ujasiri, twatamani uje :

Tuamshe, Bwana, tuamshe !

Wimbo 244 — kipande 3

Ikifichwa katika udongo mbaya,

Bwana, talanta haikutoa !

Kando yetu, nuru yetu zaifu

Haikuangazia usiku.

Tunaweza kwa saa ile ya mwisho,

Kuzaa matunda na kutumika

Hadi siku ya kuingia kwako.

Tuamshe, Bwana, tuamshe !

 

245.             Wimbo 245

Wimbo 245 — kipande 1

Yesu Mwana wa pendo lako,

Ana bei gani Baba !

Analisha imani yetu,

Na utawa, siri kubwa.

Wimbo 245 — kipande 2

Njiani mwa dunia hii,

Yeye alikutumikia.

Toka sanduku kwa Kalvari,

Alikupendeza wewe.

Wimbo 245 — kipande 3

Mwana wako alifunua

Neema, kweli, yako Mungu ;

Alikutambulisha wewe,

Hivi ukaonekana.

Wimbo 245 — kipande 4

Uzima wake ni sadaka,

Kifo, manukato bora

Ya Mtu mtakatifu kwa asili,

Mutiifu mkamilifu.

Wimbo 245 — kipande 5

Amevikwa na utukufu,

Furaha yako, pumziko,

Alituandalia  mwenyewe

Fasi pamoja naye juu.

 

246.             Wimbo 246

Wimbo 246 — kipande 1

Nguvu, tegemeo ni gani ?

Ukingo, mwamba wa mkristo ?

Na heshima yake ni gani 

???

Hatarini, matesoni ?

Ni lile Neno la Bwana.

Wimbo 246 — kipande 2

Upanga mkali ni upi

Wa kuhukumu waovu,

Uliovunja silaha nzito,

Utengao viungo vya mwili,

Ufunuao siri zote ?

Ni lile Neno la Bwana.

Wimbo 246 — kipande 3

Nani avumaye vema,

Nyakati zituliazo ?

Nani aimbaye tumaini,

Mapendo pia na salama,

Siku za huzuni, taabu ?

Ni lile Neno la Bwana.

Wimbo 246 — kipande 4

Neno lake liwe kwangu,

Chemchemu na ngao yangu,

Silaha ya kupiganisha,

Nguzo ya roho inayochoka !

Niwe daima mushindi

Kwa lile Neno la Bwana !

 

247.             Wimbo 247

Wimbo 247 — kipande 1

Twakungoja, Bwana, kuliko hata zamu,

Twakesha usiku, twangoja asubui ;

Kuamka kwa ndani ya mioyo miaminifu,

Nyota yaangaza kutoka mbinguni.

Wimbo 247 — kipande 2

Umekataliwa sasa umeinuliwa,

Siku ile wewe waitarajia

Karamu ya Kondoo, Bwana arusi, yaja,

Twakuelekezea naziri za pendo.

Wimbo 247 — kipande 3

Na kanisa lako, lakuabudu, ee Bwana,

Lahitaji kuwa nawe na kukuona.

Ndani yake, Roho anaamusha kabisa

Wimbo wa imani na wa tumaini.

Wimbo 247 — kipande 4

Kuja na utwae hazina hii mbinguni

Iliyo duniani ikikungojea,

Ukiweka juu ya taji ya zahabu,

Lulu nzuri sana, linaloangaza !

 

248.             Wimbo 248

Wimbo 248 — kipande 1

Kando yako, Mungu,

Kando yako

Sauti ya imani :

Kando yako

Hata katika taabu

Ijaayo kama muto,

Niwe Kando yako

Mungu wangu !

Wimbo 248 — kipande 2

Kando yako Bwana,

Kando yako

Nishike zikini,

Kando yako

Hata mateso mengi

Yafanya kazi yake,

Unilinde mimi,

Kando yako !

Wimbo 248 — kipande 3

Milele na wewe

Kando yako

Unisaidie,

Nihimize

Shetani angurume,

Nipo pendoni mwako

Milele na wewe,

Kando yako.

Wimbo 248 — kipande 4

Kando yako Mungu,

Njiani tuu !

Unilinde wewe

Unishike.

Msafiri, jipe moyo!

Safari inakwisha.

Kando yako Mungu,

Kando yako.

 

249.             Wimbo 249

Wimbo 249 — kipande 1

Mungu Mukuu ! Unaniona vema ;

Ulinijua, toka mbinguni.

Nawezaje kimbia nuru yako

Jicho lako lanifwata pote.

Wimbo 249 — kipande 2

Nikitembea wala kusimama,

Tazama popote wanishika ;

Na nikiwa tayari kwa kusema,

Umejua nitakayo yasema.

Wimbo 249 — kipande 3

Nikitaka kukimbilia mbali,

Na shimoni kutafuta giza,

Kupanda juu : Pote, Mungu wa nuru,

Utanipata kwa mwanga wako.

Wimbo 249 — kipande 4

Kwa imani, nafika mbele yako :

Kwa pendo,Yesu alinikomboa ;

Nimepokelewa usoni mwako,

Nikiwa nimesafishwa mimi.

Wimbo 249 — kipande 5

Unipime, ee Mungu muaminifu,

Unitazame, unitakase ;

Niongoze katika njia yako

Ukinipatia kukusifu.

 

250.             Wimbo 250

Wimbo 250 — kipande 1

Kuna chombo baharini,

Kwa wakati muzuri ;

Ikiendelea mbele

Kwa njia ya amani.

Kwa gafla upepo ukaja,

Wingu zikatoweka

{Na zoruba kunyanguka

Zaleta woga kweli.} (bis)

Wimbo 250 — kipande 2

Kweli mashaka ni mengi

Ya wasafiri hao ;

Na katika uzaifu

Wana imani ndogo

Kuna asiye waacha

Hata akisinziya,

{Ni lazima kumuamusha ?

Si rafiki mupendwa ?} (bis)

Wimbo 250 — kipande 3

Ee Bwana hautujali ?

Sasa twaangamia !

Wewe unaweza vyote,

Twakusihi utuokowe !

Akaja karibu nao

Kukemea upepo !

{Na akaihamakia

Imani yao ndogo.} (bis)

Wimbo 250 — kipande 4

Mara nyingi maishani,

Upepo unavuma,

Hata Yesu akituombea

Na kumaliza shida.

Tutegemee upendo :

Yeye habadiliki ;

{Kila siku ni mchungaji

Wa kondoo mashakani.} (bis)

 

251.             Wimbo 251

Wimbo 251 — kipande 1

Mukimbizi ! bila makimbilio,

Wakimbia Mungu bila sheria,

Wataka kuonja Injili, salama ?

Mupotevu, rudia nyumbani !

Wimbo 251 — kipande 2

Saa zapita, umilele wakuja ;

Ni wakati wakuokolewa ;

Usimame na ukitumaini,

Mupotevu, rudia nyumbani !

Wimbo 251 — kipande 3

Kuja ili upate kanzu nzuri,

Na uponyaji wa maovu yako.

Ingia karamuni kwa furaha ;

Mupotevu, rudia nyumbani !

 

252.             Wimbo 252

Wimbo 252 — kipande 1

Munaokosa salama,

Muje, Yesu aitoa ;

Upendo na wema wake,

Havifukuze mutu

Aingiapo moyoni

Analeta uheri

Woga inakimbia :

Sifa kwake Yesu !

Wimbo 252 — kipande 2

Ninyi munaosumbuka,

Muje, Yesu awapenda ;

Kwa kusaidia wanyonge,

Alikuja mwenyewe.

Aingiapo moyoni,

Analeta uheri ;

Hakuna fazaiko :

Sifa kwake Yesu !

Wimbo 252 — kipande 3

Ninyi mutetemekao

Munaogopa kufa,

Muje, Yesu Mukombozi

Alishinda mauti.

Na yeye tutaishi,

Naye tutatawala,

Kifo hakitakuwa :

Sifa kwake Yesu !

 

253.             Wimbo 253

Wimbo 253 — kipande 1

Habari njema moja

Yasikika,

Yesu anakuita ;

Kuja kwake !

Ukiogopa sheria,

Kwa makosa yako,

Bila woga, kukawa,

Njoo kwa Yesu !

Wimbo 253 — kipande 2

Muone pale Kalvari

Akikufa,

Kajitoa mwenyewe

Msalabani.

Kwa damu ioshayo

Mutu mupotevu,

Umutumainiye !

Njoo kwa Yesu !

Wimbo 253 — kipande 3

Na kwa rehema yake

Yesu atoa.

Apatia muovu

Musamaha.

Fanya haraka sasa,

Muda unapita

Leo siku ya neema,

Njoo kwa yesu !

Wimbo 253 — kipande 4

Kuja, usizuizwe,

Kuja sasa ;

Wokovu ni tayari ;

Yesu angoja.

Ukitaka Kuamini,

Umesamehewa,

Waweza imba : sifa

Kwake Yesu.

 

254.             Wimbo 254

Wimbo 254 — kipande 1

Yesu yupo, akuita :

Ataka heri yako

Jibu kwa sauti yake,

Ni Mungu Mukombozi.

Refrain : Njoo kwake, njoo kwake !

Kuja kwa Yesu leo.

Wimbo 254 — kipande 2

Kwa nini wamungojesha ?

Na ni tangu zamani

Wakataa kumusikia ;

Usikawe ! Yu hapo.

Njoo kwake, etc.

Wimbo 254 — kipande 3

Yupo, akitoa mema,

Musamaha wa bure,

Salama isiyopita,

Mbingu pia uheri.

Njoo kwake, etc.

 

255.             Wimbo 255

Wimbo 255 — kipande 1

Ni wakati ! wa uzima milele,

Sasa Mwana wa Mungu anakuita.

Ni Yesu ! Mujibu !

Kuja, uingie !

Wimbo 255 — kipande 2

Kwa karamu chumba kiko tayari ;

Waalikwa waenda kwa siku kuu.

Njoo pia, mujibu !

Kuja, uingie.

Wimbo 255 — kipande 2

Ni wakati ! Mulango yuko wazi,

Kwa Mwokozi njia ni wazi sasa.

Njoo pia, mujibu !

Kuja uingie.

Wimbo 255 — kipande 3

Kesho ! Wajua nini iletayo !

Wengi kwa bure watagonga mlango !

Milele kutengwa !

Kuja uingie.

Wimbo 255 — kipande 4

Usingoje kujibu kwa neema,

Leo kunabaki tena nafasi.

Sasa, kuja kwake !

Kuja, uingie.

 

256.             Wimbo 256

Wimbo 256 — kipande 1

Sauti inakuita,

Leo njiani sikia,

Ambamo washusha kichwa,

Pasipo kuona mwisho.

Refrain : Kuja kwa Mungu asamehe,

Utapata uheri.

Mungu hafukuzi mutu !

Ni Mungu Mukombozi.

Wimbo 256 — kipande 2

Leo Yesu akuita,

Neema yake, zawadi ;

Atahukumu muasi

Akataaye msamaha

Kuja kwa Mungu asamehe, etc.

Wimbo 256 — kipande 3

Na hadi kwa musalaba

Yesu alikutafuta ;

Alikubali hasira

Kwa kuziondosha zambi

Kuja kwa Mungu asamehe, etc.

Wimbo 256 — kipande 4

Hii sauti inadumu :

Amini Yesu leo !

Nafsi yako, kwa imani,

Ipumzike juu yake !

Kuja kwa Mungu asamehe, etc.

 

257.             Wimbo 257

Wimbo 257 — kipande 1

 

258.             Wimbo 258

Wimbo 258 — kipande 1

 

259.             Wimbo 259

Wimbo 259 — kipande 1

Yesu anagonga mlangoni :

Fungua ! Fungua leo !

Akuletea wokovu :

Fungua ! Fungua leo!

Akuletea neema ;

Anataka aketi kwako ;

Muda unapita mbio ;

Fungua ! Fungua leo !

Wimbo 259 — kipande 2

Fungua, anasamehe

Fungua ! Fungua leo !

Pokea alitoalo :

Fungua ! Fungua leo !

Achana na ubatili

Ataka akufungue ;

Ahadi zake ni kweli !

Fungua ! Fungua leo !

 

260.             Wimbo 260

Wimbo 260 — kipande 1

Mwana wake Mungu alikuja duniani,

Kutafuta na kuokowa wapotevu ;

Atakufungua na huu muzigo wa taabu

Unamjua ? (bis)

Wimbo 260 — kipande 2

Unajua mateso yake kwa Kalvari,

Na yaliyomupata juu msalabani ?

Kupitia kifo, unajuwa malipo,

Ya maovu ? (bis)

Wimbo 260 — kipande 3

Wajua samani ya damw'isafishayo

Nani aweza tosha zambi zako zote ?

Wajua kwa Mungu, damu isafishayo :

Ni salama ? (bis)

Wimbo 260 — kipande 4

Kama haujaona neema na nguvu

Ya Mwana Kondoo aliyetundikwa,

Njoo upesi na upate ukombozi kamili.

Umuamini ! (bis)

Wimbo 260 — kipande 5

Pokea musamaha, wokovu na kuishi

Vinavyopatikana katika damu

Umfuate hapa kwa njia barikiwa

Ya mbinguni ! (bis)

Wimbo 260 — kipande 6

Umjibu Mwokozi anayekualika ;

Na uonje furaha ya wateule ;

Jibu leo hii, saa zinapita mbio…

Umuamini ! (bis)

 

261.             Wimbo 261

Wimbo 261 — kipande 1

Kama mukijua Mwokozi wangu !

Ni rafiki Mzuri na mupenzi

Ajiunga nami, ananiombea.

Oh ! Ninataka awe vile kwenu.

Refrain : Mwokozi awapenda,

Mutafute kwake

Rafiki mupendwa,

Na Kimbilio.

Wimbo 261 — kipande 2

Mukijua salama nimepata

Iliyoletwa na Mwokozi !

Salama ya juu siyo ya duniani,

Yatiririka kutoka Golgota.

Mwokozi awapenda, etc.

Wimbo 261 — kipande 3

Na mukijua tumaini tamu

Linalotoka kwake Mungu !

Sauti yake yatuliza taabu,

Jicho lake linaleta furaha

Mwokozi awapenda, etc.

Wimbo 261 — kipande 4

Mutakapojua pendo la Yesu,

Mutakapoonja nira yake,

Musifiche hazina hii wenyewe,

Lakini mutangazie wengine !

Mwokozi awapenda, etc.

 

262.             Wimbo 262

Wimbo 262 — kipande 1

Muji ule, mtakatifu !

Nani atauingia ?

Nani atakubaliwa,

Pahali pale pa juu ?

Wimbo 262 — kipande 2

Mwenye zambi, ameoshwa

Kati damu ya Yesu,

Aingia milangoni :

Yeye ametakaswa.

Wimbo 262 — kipande 3

Akijaa na furaha,

Ataingia humo,

Kufurahia daima

Yesu na pendo lake.

Wimbo 262 — kipande 4

Ataona utukufu

Wa Kondoo wa Mungu ;

Na ataimba ushindi

Wake milele yote.

Wimbo 262 — kipande 5

Sifa kwa atupendaye !

Kwake nguvu, ushindi !

Utukufu kwake Yesu

Milele na milele !

 

263.             Wimbo 263

Wimbo 263 — kipande 1

Kuja kwa Yesu akupendaye,

Alijitoa mutini ;

Ataka kukupokea wewe ;

Atega mikono.

Refrain : Siku nzuri, Mwokozi mwema,

Tukikutegemea mkono,

Katika nyumba yake Baba

Tutatembea sisi.

Wimbo 263 — kipande 2

Ni kwa sasa akuitapo;

Pendoni mwake ni heri

Mugeukie moyo muasi ;

Atakuokoa.

Siku nzuri, Mwokozi mwema, etc.

Wimbo 263 — kipande 3

Muda wapita, saa zaisha ;

Sisi hatujui ya kesho ?

Yesu ni hapa muktanoni ;

Akutega mkono !

Siku nzuri, Mwokozi mwema, etc.

 

264.             Wimbo 264

Wimbo 264 — kipande 1

Kuja uliaye

Njoo kwa Mwokozi.

Kwa saa za giza

Mwambie taabu ;

Sema bila woga :

Na Bwana Yesu

Asikia shida.

Acha kulia !

Wimbo 264 — kipande 2

Kuja ! kwa mapendo

Rafiki huyu

Atosha huzuni,

Shaka na muchoko

Afariji mioyo

Ilemewayo.

Umuamini yeye

Acha kulia.

Wimbo 264 — kipande 3

Kwa nafsi zaifu

Utangaze pia

Neema kamili,

Pendo la Mungu.

Sema aamini

Jina la Yesu.

Kwake ni furaha :

Hautalia !

 

265.             Wimbo 265

Wimbo 265 — kipande 1

Duniani na mbinguni

Hakuna jina tamu,

Jina ninalolipenda

Kama lile la Kristo

Jina kuu ! Jina kuu

Lililo lake Mwana !

Jina kuu ! Jina kuu

Ni lake Emanueli !

Wimbo 265 — kipande 2

Iwe mtu mukubwa gani,

Hata awe mufalme,

Hata apewe jina gani,

Yesu ni mkubwa kwangu.

Jina kuu ! Jina kuu

Lililo lake Mwana !

Jina kuu ! Jina kuu

Ni lake Emanueli !

Wimbo 265 — kipande 3

Kwa mateso, anatuliza ;

Aponya muzaifu ;

Na analeta bidii

Kwa moyo uteswao.

Jina kuu ! Jina kuu

Lililo lake Mwana !

Jina kuu ! Jina kuu

Ni lake Emanueli !

Wimbo 265 — kipande 4

Analeta raha kubwa

Moyoni mwa muovu !

Hakuna hapa duniani

Uheri kama huu.

Jina kuu ! Jina kuu

Lililo lake Mwana !

Jina kuu ! Jina kuu

Ni lake Emanueli !

 

266.             Wimbo 266

Wimbo 266 — kipande 1

Muje kwa Bwana wa uzima,

Muje kwake Bwana Yesu !

Anawaalika leo ninyi

Kwa Neno na Roho wake

Refrain : Ategemeaye wema

Wake hawezi kutupwa,

Wake hawezi kutupwa.

Wimbo 266 — kipande 2

Yesu Kristo ni haki yetu,

Ametufungulia mbingu ;

Kwani pale musalabani

Alijitoa kwa zambi.

Ategemeaye wema etc.

Wimbo 266 — kipande 3

Muje basi kwa uhakika

Mpate uzima, salama ;

Mukiwa mumeokolewa,

Mtapata heri milele

Ategemeaye wema etc.

 

267.             Wimbo 267

Wimbo 267 — kipande 1

Yeye ni mwamba imara,

Kwangu ninayechoka,

Kama kinga yenye nguvu

Ya Mungu mawimbini.

Refrain : Mwamba wangu, ngome yangu,

Ni kimbilio langu,

Msaada matatizoni,

Ni Yesu Mukombozi.

Wimbo 267 — kipande 2

Bahari inanguruma ;

Wimbi lanizunguka :

Juu ya Kristo, mwamba wangu

Tumaini na imani.

Mwamba wangu, ngome yangu, etc.

Wimbo 267 — kipande 3

Kwa bure wimbi lavuma

Hakuna hata mwanga ;

Wa salama mawimbini,

Mwanga wafwata giza.

Mwamba wangu, ngome yangu, etc.

Wimbo 267 — kipande 4

Katika hatari kubwa,

Umepata hii kinga ?

Ushike mkono wa nguvu

Wa Yesu Mukombozi

Mwamba wangu, ngome yangu, etc.

 

268.             Wimbo 268

Wimbo 268 — kipande 1

Ninapumzika kwako,

Ee Yesu Mwokozi !

Tena yafaa nini

Kwa mtu mwenye zambi ?

Akiongozwa na nuru,

Alindwa pendoni,

Kwenda nyumba ya Baba

Kwenda kila siku,

Refrain : Ninapumzika kwako,

Ee Yesu Mwokozi !

Tena yafaa nini

Ili aonje heri ?

Wimbo 268 — kipande 2

Kwa nyakati mbaya

Unabaki nami,

Ukinipa bidii

Waongeza imani ;

Ni kati moyo wako

Unaponificha ;

Na kwa bure shetani

Ataka anitoshe.

Ninapumzika kwako, etc.

Wimbo 268 — kipande 3

Kwako nina ushindi,

Salama, uhuru ;

Nitakusifu wewe

Katika milele.

Kama heri ipitayo

Yaweza komeshwa,

Neema yako yatosha

Kwa kui na kufa !

Ninapumzika kwako, etc.

 

269.             Wimbo 269

Wimbo 269 — kipande 1

Njoo, wewe mpotevu

Njoo kwa Mwokozi

Ona mkono wake

Na kuushika

Anakualika :

Umusikie ;

Kama unasita,

Ona msalaba.

Wimbo 269 — kipande 2

Alikukomboa

Alikufia ;

Pokea neema

Kwa imani tu.

Utapata kuishi

Milele yote ;

Njoo, anasamehe

Kwa damu yake.

Wimbo 269 — kipande 3

Mwokozi apenda

Muwe pamoja.

Akutambulisha

Pendo lake kuu

Kuja kwa imani ;

Umtegemeye,

Awe tumaini

Na mema yako.

270.             Wimbo 270

Wimbo 270 — kipande 1

Wewe una tangu leo

Tumaini lililo hai ?

Umepata kwa uhakika

Tegemeo kwake Yesu ?

Ninaye Mwokozi ;

Anatosha kwangu

Ninaye Mwokozi

Tumaini langu ni kwake.

Wimbo 270 — kipande 2

Kama wewe umechoka,

Na furaha ikitoweka

Ni nani atakufariji ?

Rafiki yako ni nani ?

Ninaye Mwokozi ;

Anatosha kwangu

Ninaye Mwokozi

Kweli Neno lake ni tamu

Wimbo 270 — kipande 3

Kwa leo na hata jana,

Ukihuzunika vikali,

Ukichukizwa na maisha,

Unategemea nani ?

Ninaye Mwokozi ;

Anatosha kwangu

Ninaye Mwokozi

Nategemea pendo lake.

Wimbo 270 — kipande 4

Ungalipata nafasi

Katika mikono ya Yesu !

Na kupokea neema yake !

Rafiki, njoo utaishi.

Ninaye Mwokozi ;

Anatosha kwangu

Ninaye Mwokozi

Heri yule amtazamaye.

271.             Wimbo 271

Wimbo 271 — kipande 1

Kuja kwake, akuita,

Akuita leo.

Siku nyingi uliasi :

Leo kuja kwake.

Wimbo 271 — kipande 2

Akupenda, akupenda,

Akupenda leo.

Hata kwa unyonge wako,

Leo kuja kwake.

Wimbo 271 — kipande 3

Asamehe, asamehe,

Asamehe leo.

Pokea wokovu wake ;

Leo kuja kwake !

Wimbo 271 — kipande 4

Aondosha, aondosha,

Zambi zako leo.

Hii ni siku ya neema ;

Leo kuja kwake.